Habari kuhusu Kiarabu kutoka Novemba, 2013
Mwanaharakati wa Misri Alaa Abd El Fattah Akamatwa — Tena
Mwanablogu mashuhuri na mwanaharakati Alaa Abd El Fattah alikamatwa jana jijini Cairo usiku wa Alhamisi. Wanaomwuunga mkono wanahisi amekamatwa kwa kutumia sheria mpya ya kuzuia maandamano.
Udadisi wa Sami Anan
Mwanablogu wa Misri Zeinobia anatoa maoni yake machache kuhusu kuibuka tena kwa Sami Anan, Mnadhimu mkuu wa zamani wa Majeshi ya Misri. Je, ana mpango wa kugombea urais? Mwanahabari wa Sauti za Dunia Mtandaoni Victor Salama anasimulia zaidi.
Misri: “Morsi Hatarudi Madarakani”
Aliyekuwa rais wa Misri Mohamed Morsi hatarudi madarakani, anasema mwanablogu wa Misri Alya Gadi, kwenye mtandao wa Twita. Kuufanya ujumbe wake wazi, ametafsiri kwa lugha mbalimbali: مرسي لن يعود – Morsi is not coming back – Morsi no va a volver – Morsi ne reviendra pas – Morsi kommt nicht zurück...
Wimbo wa Mahadhi ya Kufoka Upendwao na Vijana nchini Tunisia
Ukiwa umetazamwa zaidi ya mara milioni 3 kwenye mtandao wa YouTube, wimbo wa Houmani umegeuka kuwa wimbo wa taifa kwa vijana wa Tunisia. Afef Abrougui anaeleza kwa nini,