Habari kuhusu Kiarabu kutoka Mei, 2013
Wafanyakazi Wavamia Majengo ya Serikali Nchini Mauritania
Siku ya Jumanne asubuhi, Mei 28, 2013, maelfu ya vibarua, wanaolipwa ujira wao kwa kufanya kazi kwa siku, walianzisha maandamano makubwa [ar] huko Zouérat, mji mkuu wa jimbo la Tiris Zemmour kasikazini mwa Mauritania, wakidai mikataba inayoeleweka na haki zao nyinginezo ikiwa ni pamoja na kumalizwa kwa ukiritimba wa wafanyabiashara...
Mwandishi Habari za Kiraia wa Miaka 14 Auawa Akiripoti Mapigano Nchini Syria
Omar Qatifaan, mwanaharakati wa Habari mwenye umri wa miaka 14 ameuawa akiwa katika jitihada za kutangaza habari za mapigano kati ya vikosi vya kijeshi vinavyoiunga mkono serikali na vile vya waasi katika eneo la Daraa al-Ballad kusini mwa Sryria karibu na mpaka wa Jordan.