GlobalVoices katika

j nambiza tungaraza

Wasifu wa mwandishi · 269 jumbe · alijiunga 22 Julai 2008

Kiungo cha RSS kwa j nambiza tungaraza Kiungo cha RSS kwa j nambiza tungaraza
Anwani ya Barua Pepe j nambiza tungaraza

makala mpya zaidi ya j nambiza tungaraza

9 Aprili 2012

Malawi: Maoni ya Mtandaoni Kuhusu Kifo cha Mutharika

Soma makala hii.

Victor Kaonga anaangalia maoni ya mtandaoni kufuatia habari za kifo cha Bingu wa Mutharika. Mutharika alikuwa rais wa tatu wa Malawi. Alifariki baada ya mshtuko wa moyo asubuhi ya Alhamisi. Hii ni mara ya kwanza kwa Malawi kumzika rais aliyefariki akiwa madarakani.

11 Januari 2012

Afrika: TEKNOHAMA Kwa Ajili ya Wakimbizi na Watu Wasio na Makazi

Soma makala hii.

Barani Afrika na kwingineko TEKNOHAMA imeondokea kuwa nyenzo muhimu wakati wa matatizo wakati teknolojia kama vile Ujumbe mfupi wa Simu za Mkononi, VOIP, na Simu za mkononi zinapozidi kuwa na manufaa kwa wakimbizi na kwa watu waliokosa makazi.

8 Januari 2012

Zambia 2011: Matukio Mawili Yaliyotikisa Taifa

Soma makala hii.

Matukio mawili nchini Zambia yatatambuliwa kama matukio yaliyoitikisa nchi hiyo mwaka 2011. Tukio la kwanza lilikuwa ni kifo cha Rais wa pili wa Jamhuri Frederick Chiluba na tukio la pili lilikuwa kushindwa kwa chama cha MMD baada ya miaka 20 madarakani.

4 Januari 2012

Suluhisho la Kiradikali la Umaskini Duniani: Ufunguzi wa Mipaka

Soma makala hii.

Wataalamu kadhaa wanasema kuwa umaskini uliokithiri hauepukiki. Suluhisho la kiradikali zaidi la kupunguza umaskini kwa haraka duniani kwa wataalamu wengi wa uchumi ni kufungua mipaka kati ya nchi na kuruhusu wafanyakazi kuhamia sehemu ambazo nguvukazi inahitajika zaidi.

18 Mei 2011

Uganda: Polisi Wawanyunyizia Waandamanaji Rangi ya Waridi

Soma makala hii.

Polisi wa Uganda wameikabili kampeni inayoendelea kwa mwezi mmoja sasa ya Kutembea Kwenda Kazini kwa kuwanyunyuzia waandamanaji moshi wa machozi na risasi sa moto. Wakati wa maandamano siku ya Jumanne, walitumia mbinu mpya, ya kuwashambula waandamanaji waliokuwa wakijaribu kuandamana kuelekea viwanja vya katiba katikati ya jiji la Kampala kwa maji yaliyochanganywa na uji wa rangi ya waridi.

12 Mei 2011

Singapore

Repoti ya Unesco inaonesha ‘udhibiti wa hali juu' wa vyombo vikuu vya habari nchini Singapore huku ikizitambua blogu na tovuti za vyombo vyauanahabari mpya kuwa vinatoa “mazungumzo makini mbadala juu ya masuala muhimu ya kisiasa na jamii kama vile siasa za ndani ya nchi, haki za mashoga na wazee.”

Video jumbe
Singapore: Wanablogu Waikosoa Ilani ya PAP

Soma makala hii.

Chama kinachotawala Singapore, People’s Action Party (PAP), kilitoa ilani yake ya uchaguzi tarehe 17 aprili, 2011, ambayo mara moja ilikosolewa na wanablogu wengi kwa “kutokuwa wazi”. PAP tayari kimekuwa madarakani kwa miongo mitano. Uchaguzi mkuu nchini humo umefanyika tarehe 7 Mei.

10 Mei 2011

Nepal

Pradeep Kumar Singh anaweka picha na habari za kampeni ya hivi karibu ni ya Facebook iliyopewa jina la “Jitokeze. Simama. Ongea. Vinginevyo, kaa kimya. Takriban vijana 400 wa Nepali walijitokeza sehemu ya Maitighar Mandala tarehe 8 Mei, 2011 na kudai katiba mpya.

Video jumbe
Senegal: Harakati za “Imetosha Sasa Basi”: Kwanza Kwenye Mtandao, Na Sasa Ikulu

Soma makala hii.

Wakati vuguvugu la mapinduzi likiendelea Uarabuni, matukio kadhaa ya vijana wenye hasira yamezuka katika tovuti za Senegal. Tangu mwanzoni mwa mwezi wa tatu, uanaharakati huo umeachana na ulimwengu wa mtandao na kundi linalojiita “Y'en a marre” (Imetosha Sasa Basi) sasa limegeuka na kuwa alama ya vuguvugu la upinzani. Founded in January 2011, Y’en a marre arose from frustration built up during power cuts that brought Senegal to a standstill. The group hails from the Dakar suburbs and is led by several local rappers, including Fou Malad, Thiat (from the group Keur Gui) and Matador.

8 Mei 2011

Pakistan

Faheem Haider katika blogu ya Sera ya Nchi za Nje ya Pakistani anahoji kile ambacho Jeshi na Usalama wa Taifa (shirika la kijasusi) la Pakistani vilikuwa vinafahamu kuhusu gaidi mkuu Osama Bin Laden, ambaye aliingiliwa na kuuwawa huko Abbottabad, karibu na mji mkuu wa Pakistani.

Sehemu za Dunia

Nchi

Lugha