The Global Voices Lingua project hopes to bring GV content to new linguistic audiences - Details

Also in:

Christian Bwaya Wasifu wa mfasiri

Kiungo cha RSS kwa Christian Bwaya

Picha ndogo ya mfasiri

Kuhusu Christian Bwaya

28 jumbe · alijiunga 2009-05-18

Ni mwanafunzi wa Baolojia, mpenzi wa lugha ya kiswahili. Muda wangu za ziada huutumia kusoma na kuandika. Ninayo blogu niitayo Jielewe (http://bwaya.blogspot.com) ambapo hujadili pamoja na masuala mengine falsafa, sayansi, dini na saikolojia. Nafikiri kutumia sehemu kubwa ya maisha yangu kuandika na kujitolea kwa ajili ya jamii yangu na ndio maana nikajiunga na Lingua Swahili.

Anwani ya Barua Pepe Christian Bwaya

2009-10-26

Cambodia: Tuzo yamuenzi aliyenusurika na utumwa wa ngonoVideo post

Sina Vann alikuwa na umri wa miaka 13 wakati alikupoja Cambodia kutoka Vietnam kwa kile kilichopaswa kuwa likizo. Badala yake, aliuzwa kama mtumwa kwa ajili ya ngono na alitumia miaka miwili iliyofuata ndani ya danguro. Alikombolewa wakati Somaly Mam, mwanaharakati wa kupinga utumwa na sura ya Taasisi ya Somaly Mam, ...

2009-10-25

Marekani: Wanandoa wa rangi tofauti wanyimwa cheti cha ndoa

Juma lililopita huko Hammond, Louisiana, wapenzi wawili walituma maombi ya kibali cha kufunga ndoa na walikataliwa kwa misingi ya rangi zao tofauti. Afisa wa kutathmini na kuandikisha nyaraka (Muamuzi wa Amani) alidai kuwa “ndoa baina ya watu wa rangi hazidumu” na alisema kuwa anafanya hivyo “kwa ajili ya watoto.”

2009-10-24

Uganda: Wanablogu wa Uganda Wajadili Muswada Unaopinga Ushoga

Muswada ambao utaufanya ushoga kuwa kingyume cha sheria nchini Uganda umewasilishwa bungeni na sasa unasubiri tu saini ya rais Yoweri Museveni. Wanablogu mashoga nchini uganda wanajadili.

2009-10-23

Ghana: Siku ya Kublogu mwaka 2009

Kwenye siku ya Kublogu Kwa Vitendo Duniani, Waghana waliwahoji viongozi wa dunia, walichachafya karatasi za Benki ya Dunia, walitambulisha tovuti mpya na walijiuliza ni kwa nini kulikuwa na majadiliano machache sana yanayohusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa nchini – na pia walitambua kwamba kuna mambo fulani nchi kama Ghana zinayafanya vyema.

2009-10-17

Big Brother Africa msimu wa IV: Mageuzi yameanza

Big Brother Africa 4: Mapinduzi ni mfululizo wa nne wa vipindi vya kituo cha televisheni vinavyoonyesha maisha halisi vya Big Brother Africa, vilivyoanza Septemba 6, 2009. Kipindi hicho kimeshaanza kuzua mijadala na maoni kwenye mtandao wa intaneti kutoka kwa wanablogu na wasomaji wao.

2009-10-12

Gabon: Upinzani waendelea kupinga matokeo ya Uchaguzi

Wapinzani wa kisiasa wa Gabon wanaonyesha muungano wa vyama vya siasa kupinga matokeo ya uchaguzi wa mwezi Agosti, ambayo yalimkabidhi urais mwana wa mtawala wa kiimla aliyepita, Omar Bongo. Wanasiasa na raia wanaikemea Ufaransa kwa kuingilia siasa za nchi hiyo.

2009-10-11

Australia: Wanawake wa Kenya wakataliwa haki ya ukimbizi

Wanawake wawili wanakabiliwa na uwezekano wa kutimuliwa kutoka Australia baada ya maombi yao ya kuomba hifadhi kukataliwa, pamoja na hatari wanayoweza kuipata ya kulazimishwa tohara ya kike ikiwa watarudishwa nyumbani.

2009-08-02

Iangazeni Naijeria: Imetosha Sasa Basi

Pamoja na kuwa nchi yenye utajiri wa mafuta, hali ya ugavi wa umeme nchini Naijeria hairidhishi. “Katika sehemu nyingi za nchi, giza linatawala na majenereta yamechukua nafasi kama vyanzo vya nishati ya umeme” Inasema blogu ya Adebayo. Sasa Wanaijeria wameanzisha kampeni kubwa ya mtandao wa intaneti inayopinga hali hii inayogharikisha kwa kutumia tovuti za kijamii, hasa kwenye Twita kwa kutumia anwani ya #lightupnigeria (#iangazenaijeria).

2009-07-29

Kenya: Ukame Uliokithiri Wachochea Mgogoro kati ya Binadamu na Wanyama Pori

Kenya inakabiliwa na ukame mbaya zaidi katika kipindi cha zaidi ya muongo mmoja kwa mujibu wa Idara ya Hali ya Hewa. Ukame huu umeathiri nchi nzima, lakini athari zake zimeonekana zaidi katika jamii ya Kimasai ambayo chanzo zhake cha kwanza cha maisha ni mifugo. Wakikabiliwa na hatari ya kupoteza mifugo yao ...

2009-07-27

Mauritania: Uchaguzi wenye udanganyifu?

Tarehe 18-07-2009, miezi 11 baada ya mapinduzi ya kijeshi yakiongozwa na Jenerali Mohamed Ould Abdel Aziz, Mauritania imemchagua Jenerali huyu kwa Urais, na kusababisha wapinzani wakuu wa Abdel Aziz kuukataa uchaguzi kwamba ni “kiini macho,” kwa mujibu wa Habari za BBC. Pitio la haraka haraka kwenye blogu za nchi za Saheli linaonyesha kwamba wapinzani wako katika ushirika mzuri.