Mghosya · Mei, 2013

makala mpya zaidi zilizoandikwa na Mghosya kutoka Mei, 2013

Ijue Mauritania kwa Jicho la Msanii wa Kireno

Msanii wa Kireno Isabel Fiadeiro anayeishi katika mji wa Nouakchott, Mauritania, ambako anachora na kuendesha maonyesho ya kazi ya sanaa. Fiadeiro vilevile huchora madhari kwa kuyatazama, hujaza blogu yake anayoiita Michoro nchini Mauritania na michoro ya maisha ya kila siku katika taifa hilo la Afrika Magharibi. Global Voices ilizungumza na Fiadeiro kuhusu kazi yake ya sanaa na namna michoro yake ilivyomsaidia kuifahamu Mauritania.

Lebanon: Mwanablogu Apata Kipigo kwa Kupiga Picha

Mwanablogu wa ki-Lebanoni Habib Battah anaeleza namna alivyoshikiliwa bila hiari, akilazimishwa kufuta picha katika kamera ya simu yake na kudhalilishwa mfululizo katika posti hii inayohusiana na ripoti ya Beirut. Aliporipoti suala hilo katika kituo cha polisi mahali alipokuwa, mafisa wanaohusika walimkana na kumgeuzia kibao yeye. Anaongeza: Walikuwa sahihi. Kama watu...

Kwa nini Mashirika ya Umma Yameshindwa Nchini Zambia

Elias Munshya, mwanasheria na mchungaji wa Zambia, anaeleza kwa nini mashirika ya umma yamedumaa nchini Zambia tangu uhuru: Mashirika ya umma hayajawahi kutengeneza faida tangu mwaka 1964. Yamekuwa yakiendeshwa kiholela bila utaalamu wa kibiashara bali kisiasa. Mashirika haya hayajawahi kuwa na wataalamu wanaoendesha bodi husika bali yamejaa wafanyakazi kwa misingi...

Botswana: Kuibwa kwa Kazi ya Sanaa ya “Bushman's Secrets”

MyWeku anaichambua filamu yenye maudhui halisi (documentary) inayoelezea wizi wa kazi ya sanaa ya Sana iitwayo “Bushman's secrets”: Filamu hii inachora picha inayosikitisha ya namna ambavyo Uniliver, kampuni inayojinadi kama “mzalishaji mkubwa tena nambari moja duniani wa barafu zitengenezwazo kwa maziwa maarufu kama ice cream,” sasa linatumia bila aibu maudhui...

Rais wa Chama cha Madaktari Msumbiji Akamatwa

Baada ya mgomo wa madaktari uliodumu kwa takribani juma moja nchini Msumbuji, Dr. Jorge Arroz, Rais wa Associação Médica de Moçambique, amekamatwa usiku wa Jumapili, Mei 26, 2013, kwa tuhuma za “uchochezi” (kuhamasisha watu kutokuridhishwa au kuiasi serikali). Kwenye mtandao wa Twita na Facebook, @verdademz, @canal_moz na ripoti nyingine za...