Mazungumzo ya GV: Kura ya Maoni Inayoongozwa na Raia wa Hong Kong Kuhusu Haki ya Upigaji Kura

Wanaharakati na wanazuoni wa Hong Kong wamefanya kazi pamoja kwa miaka miwili kuandaa kura ya maoni inayoongozwa na raia na kuwezeshwa na teknolojia juu ya haki ya kupiga kura iliyofanyika mwishoni mwa mwezi wa Juni. Takribani watu 800,000 –karibu asilimia 20 ya idadi ya watu wenye sifa ya kupiga kura nchini humo–walijitokeza kupiga kura zao katika kuunga mkono haki ya kimataifa ya kupiga kura kwa raia wote wa jimbo hilo maalum la kiutawala la China.

Katika toleo hili la Mazungumzo ya GV, mhariri wa GV wa China na mtetezi wa haki za vyombo vya habari Hong Kong Diwan Lam wanajadili mkakati na mchakato ulio nyuma ya kura hiyo na wanatudokeza nini hasa kinafuata kwa watetezi walio msitari wa mbele katika harakati hizo la haki ya kupiga kura jimboni Hong Kong.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.