Namna Teknolojia Inavyosaidia Watu Kujifunza —na Hata Kuokoa—Lugha za Dunia

Makala haya yameandikwa na mwandishi mwalikwa Allyson Eamer, mwanazuoni katika kitivo cha stadi za jamii na lugha katika Taasisi ya Teknolojia ya Chuo Kikuu cha Ontario. Toleo la makala haya  lilichapishwa awali kwenye blogu ya Mradi wa Ethnos.

Moja wapo ya lugha zinazopotea kwenye sura ya dunia hufa kila baada ya siku 10 hadi 14. Katika jitihada za kuziokoa lugha hizi zisipotee, wasemaji, wanazuoni na wataalamu wa Teknolojia wanaungana kuchungua namna teknolojia za kidijitali zinavyoweza kutumiwa katika kuhuisha lugha. 

Lugha zimekuwa katika hatari ya kupotea kadri muda unavyokwenda na kadri wazungumzaji wake wanavyohamia kwenye lugha nyinginezo zinazoonekana kuwa na nguvu ya kisiasa na kiuchumi. Mara nyingi, mabadiliko hayo hutokea kwa sababu ya ajenda za kikoloni za kujitanua ambazo huwafanya wenyeji, tamaduni, na ardhi zikitekwa na wajenzi wa falme zao. 

Katika hali inayotia matumaini, baadhi ya wasomi hawafurahishwi na kile kinachoweza kuitwa “Ku-Darwinishwa kwa lugha”, au kubaki kwa lugha zenye nguvu na kupotea kwa zile zisizo na nguvu. Hoja yao kuu ni: Je, si rahisi ste tukizungumza lugha moja?

Sitafafanua namna kila lugha ilivyo na tofauti za kipekee kwenye mtazamo wa kidunia: namna msamiati wa lugha unavyoofunua tunu za watu wanaoizungumza, namna maarifa ya asili yanavyobebwa katika muundo wa lugha, na namna sanaa, kujieleza, historiam utamaduni, uchumi na utambulisho vinavyofungamanishwa na lugha. Badala yake ninaendelea kwa imani kwamba, kama nilivgo mimi, wewe ndugu msomaji unaamini kwamba kupotea kwa lugha ni janga na kwamba wenye lugha hizi za asili duniani kote wameshuhudia wakinyang'anywa vingi.

Miniature DNF Dictionary  by Tomasz Sienicki (CC-SA-3.0)

Kamusi ndogo ya mfumo wa DNFpicha na Tomasz Sienicki (CC-SA-3.0)

Teknolojia inaweza kuwaunganisha walimu na maudhui ya lugha na watu wanaotamani kujifunza lugha hizo duniani kote kwa wakati ule ule. Teknolojia inaweza kuhifadhi lugha zilizokwenye hatari ya kupotea kwa kutumia mfumo wa sauti. Inaweza kutengeneza na kusambaza mitaalama na zana za kujifunzia kirahisi na kwa wepesi. Inaweza kurahisisha kujifunza kwa kujitegemeea kupitia michezo, kupakua programu na viwezeshi vingine. Ianweza kuwaunganisha walimu na wanafunzi wa lugha kwa namna mbalimbali.

Watu wenye fikra za kuleta mabadiliko wanaunganisha nguvu za kiteknolojia kuzileta lugha kutoka kwenye hatari ya kupotea, na katika hali nadra sana, kuzifufua lugha zilikwisha kufa.

Hapa ni pitio fupi la namna mbalimbali ambazo teknolojia ya kidijitali zinavyotumiwa katika jitihada hizi:

Ulaya

Marekani Kaskazini

  • CD-ROM ya kozi ya kujifunza mwenyewe  imeundwa katika lugha ya Navajo, inayozungumzwa kusini magharibi mwa Marekani
  • Wanaojifunza Kicherokee, lugha inayozungumzwa Marekani Kusini Kati, wanaweza kuwasiliana bila kuonana.
  • Jamii ya Ojibwe huko Manitoba, Canada, wanatumia zana ya simu za iPhone kuhuisha lugha zao, kama wanavyofanya Wawinnebago wa Marekani ya Magharibi

Afrika

  • Maktaba zinaundwa kwa ajili ya lugha zinazozungumzwa tu nchini Kenya.
  • Hadithi za kale zinarekodiwa katika lugha za asili nchini Mali.
  • Kampuni ya kujifunza lugha mtandaoni inatoa kozi ya lugha za miluzi kwenye visiwa vya Canary nchini Uhispania.

Marekani ya Kati na Kusini

Asia

Ncha ya Kaskazini

  • Mfululizo wa masomo ya mtandaoni  yanapatikana katika lugha ya Inuktitut, moja ya lugha ya nchi za ncha ya kazkazini mwa dunia.

Mashariki ya Kati

  • Masimulizi ya mtandaoni katika lugha ya Chaldean, inayozungumzwa nchini Irak, inaweza kuwasaidia wazungumzaji kujifunza kwa usahihi lugha hiyo.

Nchi za Bahari ya Pasifiki

Kwa habari za karibuni zaidi kuhusu teknolojia kuhusu matumizi ya elimu ya lugha za asili, angalia kwenye tovuti ya hifadhi ya maudhui ya Allyson Eamer

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.