‘Hali Mbaya’ ya Haki za Binadamu Nchini Vietnam

Mtandao wa haki za Binadamu illitoa ripoti yake ya 2013 kuhusu ‘hali mbaya’ ya haki za binadamu nchini Vietnam:

…. Hali ya haki za binadamu nchini Vietnam iligeuka na kuwa mbaya mwaka 2013. Idadi ya watu waliotiwa kizuizini kwa kutoa maoni ya kisiasa yaliyo kinyume na wale wa chama tawala iliongezeka sambamba na kuongezeka kwa ukatili wa polisi uliodhihirishwa na idadi kubwa ya vifo na majeruhi unaosababishwa na vurugu, na idadi ya wakulima ambao walinyang'anywa ardhi yao bila fidia ya kutosha nayo iliongezeka.

Ripoti ilibainisha kwamba rekodi mbaya nchini Vietnam ni kinyume na ahadi ya kukuza haki za binadamu baada ya kuwa mwanachama wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa na baada ya kuongezea dhana ya haki za binadamu katika Katiba yake.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.