VIDEO: Wanafunzi wa Iran Wavuruga Hotuba ya Mgombea Urais wa Chama Tawala

Kikundi cha wanafunzi wa  Chuo Kikuu cha Amirkabir  kilichopo Tehran nchini Iran, kiliimba kauli mbiu za kuunga mkono Upinzani, huku wakibeba mabango na kupeperusha bendera ya Iran wakati wa hotuba ya mgombea aliyeshindwa mhafidhina ambaye alikuwa mpatanishi mkuu wa nguvu za nyuklia  Saeed Jalili  mnamo Aprili 14, 2014. 

Nyimbo hizo zenye maneno yanayotumiwa na wapinzani zilikuwa zinamwuunga mkono  Mir Hussein Mousavi na Mehdi Karroubi, ambao ni viongozi wa maandamano ya Green Movement yalifanikiwa sana nchini humo kufuatia kuchaguliwa kwa mara nyingine kwa kishindo kwa Rais  Mahmoud Ahmadinejad mwaka 2009. Waandamanaji waliyachukulia matokeo hayo kuwa ya kuchakachuliwa, na mamiliano waliandamana kumtaka Ahmadinejad aachie madaraka.

Hata hivyo, vyombo vya dola vilianza kupambana kwa nguvu na vuguvugu hili mapema mwaka 2010, na Mousavi pamoja na Karroubi, ambao wote ni wagombea wa urais, ikiwa ni pamoja na  mke wa Mousavi aitwaye Zahra Rahnavard ambao kwa pamoja  waliwekwa chini ya ulinzi na kuzuiliwa kutoka nyumbani kuanzia Februari 14, 2011. 

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Amirkabir waliimba, “Kura zetu tunampa Waziri Mkuu wa Imam,” wakimaanisha Mousavi, ambaye alikuwa waziri mkuu kuanzia mwaka 1980 mpaka 1988 wakati ambao Ruhollah Khomeini alikuwa madarakani kama kiongozi mkuu wa nchi hiyo.

Wakati huo huo, wanafunzi wahafidhina wa Basiji waliokuwa wamekaa kkwenye viti vya mbele, na wanaomwuunga mkono Jalili, nao walianza kuimba “unaanguka na Marekani.” Wanaweza kuonekana mwishoni mwa video hii ya YouTube, inayoanza na kuwaonyesha wanafunzi wanaounga mkono Upinzania:

Mada kuu ya hotuba ya Jalili ilikuwa ni  mafanikio ya kinyuklia ya nchi hiyo.

Alireza Taba alitwiti kwamba baadhi ya wanafunzi hao waliokuwa wanaandamana walikutana na adhabu ya utawala wachuo baada ya hapo: 

Takribani wanafunzi tisa walioandaman wakati wa hotuba ya Jalili waliitwa na kamati ya nidhamu.

Hanif Z.Kashani aliripoti:

Wanafunzi wanapinga “Chama Cha Nyuklia”, nyimbo zao zilimtoa Saeed jalili

Kwenye mtandao wa twita, mtumiaji amirHP alitwiti kuhusu maandamano hayo:

Jalili alikuja kwa ajili ya maaadhimisho ya siku ya nyuklia lakini nyimbo za vibwagizo vya watu wanaomwuunga mkono Mousavi ndio zimetawala

َUser Asame wrote:

Haijalishi kama ni  [Rais wa sasa wa Iran] Hassan [Rouhani] au Hussein [Mousavi], lakini vuguvugu linaendelea.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.