Win Tin: Mfungwa wa Kisiasa wa Myanmar Aliyefungwa kwa Muda Mrefu Zaidi Afariki Dunia

Win Tin, legendary Burmese journalist and activist died last April 21. Photo from @hrw (Human Rights Watch

Win Tin, mwandishi wa habari na mwanaharakati maarufu wa Burmese, alifariki Aprili 21. Picha kutoka kwa @ HRW (Haki dhibiti za Binadamu.

Mwandishi wa habari na mwanaharakati wa kidemokrasia mkongwe U Win Tin alifariki kwa matatizo ya figo mnamo Aprili 21, 2014 akiwa na umri wa miaka 85.

Kabla ya kuingia madarakani kwa serikali ya kijeshi ya Junta katika miaka ya 1960, Win Tin alikuwa mhariri wa gazeti maarufu la Myanmar. Mwaka wa 1988, alisaidia kuunda chama cha upinzani cha National League for Democracy (NLD) na kumwuunga mkono mgombea Aung San Suu Kyi.

Alishtakiwa kwa kuwa mkomunisti na kukamatwa mwaka wa 1989. Baada ya miaka mitatu, muda wake gerezani uliongezwa baada ya kushtakiwa tena kwa uchochezi. Mwaka wa 1996, alikutwa na hatia tena na kuhukumiwa tena miaka mingine saba katika jela baada ya yeye kutuma ripoti yenye kurasa 83 kwa Umoja wa Mataifa kuelezea hali ilivyo mbaya katika magereza ya Myanmar.

Hatimaye aliachiliwa mwaka wa 2008 baada ya kufungwa kwa miaka 19. Lakini hata baada ya kurejeshewa uhuru wake, aliendelea kuvaa shati la rangi ya bluu la wafungwa akiwakumbuka na kuwaunga mkono wafungwa wengine wa kisiasa.

Aliendela kuwa rafiki mwaminifu na mzuri wa Aung San Suu Kyi ingawa alikosoa baadhi ya maamuzi yake ya kisiasa ikiwa ni pamoja na ushiriki wa NLD katika uchaguzi.

Win Tin alikuwa mfungwa wa kisiasa aliyefungwa kwa muda mrefu. Tofauti na Aung San Suu Kyi ambaye aliwekwa chini ya kifungo cha nyumbani, Win Tin alikuwa kizuizini katika seli iliyojengwa maalumu kwa ajili ya kuwaweka mbwa wa kijeshi.

Zin Linn, mfungwa wa zamani wa kisiasa, alielezea kuhusu gereza la Win Tin:

Walimweka peke yake katika seli yake. Seli ilikuwa ya ukubwa wa futi 8.5 x 11.5. Kulikuwa na mkeka wa mianzi pekee juu ya sakafu. Kulala, kula, kutembea na kujisaidia haja vyote hivyo vilifanyika katika sehemu moja. Hakuweza kuona jua, mwezi au nyota. Alizuiliwa makusudi kupumua hewa safi, kuonja chakula bora na kunywa tone la maji safi. Jambo baya zaidi ni kukaa pekee katika kizimba hicho kwa miaka.

Alimtaja Win Tin kama ‘mwandishi wa habari hodari katika Burma':

Kwa Junta, U Win Tin kwa hakika ni mlima wenye miamba. Ingawa wanataka kuponda mlima huo, kamwe hawawatoweza kufanya hivyo. Lakini kama alivyokuwa jasiri dhidi ya watesi wake, huruma yake kwa wandugu wake na watu wake ilikuwa kubwa kupita kiasi. Kwa kweli anastahili heshima kubwa kwa ajili ya sadaka yake.

Kyaw Zwa Moe, mhariri wa jarida la Irrawaddy, alibainisha jinsi ambavyo Win Tin hakupata kamwe kuafikiana na serikali ya Junta licha ya afya yake kudhoofika:

Lakini kwa serikali yoyote yenye ukandamizaji, Win Tin alikuwa adui mkubwa. Kutokana na harakati zake za kisiasa, serikali ya zamani ilimfunga jela kwa karibu miongo miwili, walimtesa, kumnyima matibabu na kumpokonya nyumbani kwake. Hatimaye walipomwachilia huru mwaka wa 2008, aliombA abaki kwenye kifungo cha nje. Hata hivyo, licha ya shinikizo lao, kamwe hakuacha misimamo yake

Ye Htut, naibu waziri wa habari, alitoa taaarifa kwa niaba ya serikali:

Kisiasa hatukubaliani kimsimamo na Win Tin, lakini tunatoa heshima zetu kwa msimamo wake na imani ya kujitolea kwake. Ingawa hatukubaliani naye, tunathamini nia yake nzuri ya kufanya nchi hii iendelee kidemokrasia katika njia ya mafanikio aliyoiamini. Tunaamini kifo cha U Win Tin ni hasara kubwa si tu hasara ya sauti wazi ya upinzani katika siasa za Burmese, lakini pia vyombo vya habari vya Burmese vimepoteza mwandishi wa habari mwenye uzoefu na hekima.

Mya Aye, mwanachama wa 88 Generation Students Group, alimtambua Win Tin kama kiongozi mnyenyekevu na wazi :

Ni lazima tujivunie mtu huyu na kumwona kama mfano wa mwanasiasa wa kuigwa … Hakutaka kumsumbua mtu yeyote. Tena aliacha wosia wa kutaka mazishi ya haraka. Alikuwa mtu muwazi. Hakutaka mali yoyote kwa ajili yake mwenyewe, alitumikia nchi kipekee. Alistahili kuona yale ambayo yeye alijitolea kwa ajili yake.

Aung Zaw alimwelezea Win Tin kama mwanga elekezi wa harakati za demokrasia:

Win Tin alikuwa mwenye nia, jasiri katika kukosoa serikali hadi mwisho, na dhamira ya kuepuka vikwazo vyote vya Burma kwa safari ndefu ya demokrasia.

Bila ya mwanga wake kuongoza, ni vigumu kufikiria jinsi harakati ya kidemokrasia itakavyokumbwa na changamoto nyingi zijazo wakati huu wa kidemokrasia mpito usiotabiriki, ambapo bado kuna mbwa mwitu wengi waliovaa mavazi ya kondoo.

Kay Mastenbroek, aliyetengeneza video ya filamu kumhusu Win Tin, alimkumbuka marehemu huyo mwandishi wa habari kama mtu ambaye aliyejitokeza na kusema “hapana”, wakati wengine wote wakisema “ndiyo”:

Kwangu mimi, filamu inaelezea hadithi ya akili yenye nguvu na huru – mtu ambaye alijitokeza na kusema “hapana”, wakati wengine wote wakisema “ndiyo”. Mtu ambaye alipenda kuwa peke yake wakati mwingine, lakini pia alipenda kukaa na marafiki wengi aliokuwa nao wakati wa uhai wake. Mara kwa mara, alikuwa mkaidi na mwasi kidogo, lakini ni aina hii ya mtu inayofanya mambo yote kuvutia zaidi, nadhani.

Nitamkumbuka mjomba wangu kutoka Burma, kwa sababu ningelipenda kumfanya aonekane kuwa waandishi wa habari ambaye watengenezaji wa filamu watamuenzi na kufanya kazi ya uandishi wa habari kuwa bora zaidi katika nchi yake. Yeye angependa iwe hivyo.

Kenneth Roth, mkurugenzi mtendaji wa Haki za Binadamu, aliandika tanzia ya Win Tin:

U Win Tin alikuwa Mfano wa ujasiri wenye heshima na kanuni dhidi ya miongo kadhaa ya utawala wa kikatili wa kijeshi.

U Win Tin aliongoza kizazi chote cha wanaharakati ambao walikubali wito wake na mapambano ya kufanya Burma kuwa na haki za kuheshimu demokrasia.

Blogu ya US campaign for Burma pia ilikuwa na tanzia kwa Win Tin:

Kama harakati ya kuanzisha Burma huru zikiendelea, hebu tumuenzi mtu aliyejitolea maisha yake kwa sababu hiyo. U Win Tin alikuwa mwandishi wa habari, mfungwa, kiongozi, na mfano wa kuigwa. Ingawa hayupo tena nasi, tunatumaini kusaidia kujenga aina ya nchi U Win Tin aliyoitaka: moja inayowakilishwa na watu, watu wote, isiyo na utawala wa kimabavu.

Katibu mkuu wa shirikisho la Kimataifa la Haki za Binadamu (FIDH) Debbie Stothard alikumbuka jinsi ambavyo Win Tin hakuwahi kuacha kukosoa ‘dosari za mchakato wa mageuzi’ zilizofanywa na serikali ya sasa ya raia:

Wakati wengi walikuwa wanapongeza maendeleo ya hivi karibuni nchini Burma, tulihitaji Win Tin kutukumbusha ukweli wa dosari ya mchakato wa mageuzi ya nchi. Atakumbukwa sana na kwa kweli hatasahaulika kamwe.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.