Mazungumzo ya GV: Nini Kimewakuta Wanablogu wa Iran?

Katika siku za mwanzo za kublogu, wanablogu wataka mabadiliko wa Iran walikuwa maarufu sana kwenye vyonbo vya habari vya kimataifa. Nchi ilikuwa changa, watu wakiwa na uelewa wa mtandao wa intaneti na ilikuwa ya kwanza kufanya mijadala ya kisiasa mtandaoni. Hivi karibuni, mambo yamekuwa kimya. Iran inafamika kwa ubabe wake linapokuja suala la kufuatilia na kudhibiti yanayoandikwa mtandaoni. Je, wanalogu hao wamenyamazishwa? Au hiki kinachoonekana kuwa kushuka kwa kublogu ni kwa sababu ya kubadilika kwa utamaduni na uandishi wa kiraia?

Waandishi wa taarifa mpya iliyoandaliwa na Mpango wa Vyombo vya Habari vya Iran wa Shule Kuu ya Annenberg, “Hali ya Blogu za Mashariki ya Kati: Tathmini ya Mabadiliko ya Mitando ya Mashariki ya Kati” (PDF) wanaungana na Global Voices kwenye mazungumzo ya GVwiki hii kujadili matokeo ya utafiti wao.

Arash Kamangir na Laurent Giacobino wanazungumza na Solana Larsen.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.