Kwa nini Rwanda Inaituhumu Ufaransa Kusaidia Mauaji ya Kimbari ya 1994

Wakati Rwanda ikiwakumbuka waathirika wa mauaji ya kimbari yalitokea miaka 20 iliyopita, Rais Kagame anasema tena kuwa Ufaransa lazima “ikabiliane na ukweli mgumu” wa kukiri kushiriki kwenye mauaji hayo ya mwaka 1994 [fr]. Kama matokeo ya matamshi hayo, serikali ya Ufaransa imesusia matukio yote ya kukumbuka mauaji hayo na waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Ufaransa anamtaka rais Hollande kutetea Heshima ya Ufaransa na jeshi lake .  Rémi Noyon wa tovuti ya Kifaransa ya Rue 89 anaorodhesha sababu kwa nini Rwanda inaituhumu Ufaransa kwa kusaidia mauaji hayo ya kimbari [fr] :

 1) La France va « de facto » prendre le commandement de l’armée rwandaise face au rebelles du Front patriotique rwandais (FPR).

2) La France craint alors que l’offensive tutsi ne soit télécommandée via l’Ouganda par les Anglo-saxons, et ne vise à enfoncer un coin dans l’influence de la France sur la région

3) La France ne semble pas s’intéresser outre mesure aux négociations de paix.

4) Les soldats n’embarquent pas le personnel tutsi présent à l’ambassade de France (sauf une personne). Ils seront tous massacrés.

5) Quant à l’opération Turquoise, elle continue à diviser : elle a certainement permis de sauver des vies tutsi, mais l’armée est accusée d’être restée passive – et donc complice – face aux atrocités.

1) Ufaransa iliamuru baadhi ya matawi ya jeshi la Rwanda kuwavamia waasi wa RPF (Rwandan Patriotic Front).

2) Ufaransa ilikuwa na wasiwasi kuwa jitihada za kujikinga zilizofanywa na waTutsi zilifanyika Uganda kwa kuratibiwa na nchi zizungumzazo Kifaransa lengo likiwa ni kupunguza nguvu ya Ufaransa kwenye eneo hilo. 

3) Ufaransa haikuonekana kuvutiwa na jitihada za mazungumzo ya amano kabla ya mgogoro.

4) Wanajeshi hawakuwaondoa wafanyakazi wa kiTutsi waliokuwa kwneye jengo la Ubalozi wa Ufaransa (isipokuwa mmoja). Wote waliishia kuuawa.

5) Kama ilivyokuwa kwa Operation Turquoise, iliendelea kusababisha mgawanyiko: ilisaidia waTutsi kuishi, lakini jeshi linatuhumiwa kubaki kimya -na hivyo kuwa kama linawasaidia waliokuwa wanaendesha mauaji.

 

 

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.