Walebanoni Wazindua Kampeni ya Kuwatetea Wasyria Dhidi ya Ubaguzi wa Rangi

Kampeni ya kuwatetea Wasyria wanaokabiliwa na ubaguzi wa rangi (Kwa kiarabu: الحملة الداعمة للسوريين بوجه العنصريّة) ilizinduliwa mnamo Machi 21, 2014, katika siku ya kimataifa ya Kuondoa Ubaguzi wa rangiwas, “katika kukataa aina zote za unyanyasaji dhidi ya Wasyria waishio Lebanon, hotuba za kisiasa zenye sura ya ubaguzi na matangazo yanayohusiana na ubaguzi huo kwenye vyombo vya habari.” Kwa maneno mengine, inakusudia kukabiliana kile kinachoifahamika kuwa kukua kwa ubaguzi dhidi ya wakimbizi wa Syria wanaoishi Lebanoni. Wanasiasa wa Kilebanoni wanatuhumiwa na wanaharakati kwa kutumia migogoro kati ya wakimbizi wa Syria na wenyeji wa baadhi ya maeneo ya Lebanoni kwa makusudi ya kisiasa.

Baada ya kampeni ya “Mimi si Mhafidhina” kwa heshima ya Mohammad Chaar na kampeni ya “Mimi si uchi” kumwuunga mkono Jackie Chamoun mshindi wa Olimpiki wa Mchezo wa Kuteleza kwenye barafu na kisha dhidi ya Unyanyasaji wa Majumbani, kampeni ya kupinga ubaguzi wa rangi inatumia namna inayofanana (kwa sasa ni ile ile) ya kuonyesha upinzani mtandaoni kwa kuwaonyesha wananchi wakiweka habari na picha zao zenye kubeba ujumbe.

Akizungumza na gazeti maarufu la Kilebanoni linaloandikwa kwa lugha ya Kifaransa “L'Orient-le Jour”, mmoja wa wanaharakati wanaoshiriki kwenye kampeni hiyo alisema:

Les politiciens n'arrivent même pas à résoudre le problème de l'approvisionnement en électricité, des transports en commun, des violences à Tripoli, dans le Hermel, de la violence conjugale, de la cherté des télécommunications… Ces problèmes existaient avant l'arrivée des réfugiés syriens, et nos politiciens ne les ont pas résolus. Ils ne veulent rien résoudre, ils ne l'ont jamais voulu

Wanasiasa hawawezi hata kutatua matatizo ya msingi kama vile kuleta umeme na kuimarisha usafiri wa umma, kumaliza ghasia huko Tripoli na Hermel, unyanyasaji wa majumbani, gharama kubwa za mawasiliano ya simu…haya matatizo yamekuwepo kabla ya kuja kwa wakimbizi wa Syria na wanasiasa wetu hawakufanya lolote kuyatatua, wala hawajawahi.

Hapa ni baadhi ya mifano ya wale wanaoshiriki kampeni hiyo:

"And our house is your house if you're willing to accept us parents to parents, brothers to brothers

“Na nyumba yetu ni nyumba yenu kama mko tayari kutukubali kama wazazi na wazazi, ndugu kwa ndugu

I once met a Syrian who made us both proud

Nilikutana na Msyria mmoja aliyetuletea fahari

Above: The Humanist. Below: The Racist

Juu: Mtu athaminiye ubinadamu. Chini: Mbaguzi wa rangi

He didn't escape death [in his country] to die of humiliation [in your country]

Hakutoroka kifo [nchini kwake] ili aje afe kwa sababu ya kunyanyaswa [nchini mwenu]

Not every Syrian is a criminal and not every Lebanese is innocent

Si kila Msyria ni mhalifu na si kila Mlebanoni hana hatia

The Syrian refugee is like us: he can't live. Direct your anger towards the corrupt ruling class.

Mkimbizi wa Syria ni kama sisi: hawezi kuishi vizuri. Elekezeni hasira zenu kwa tabaka la mafisadi wanaotawala.

I'm a human before being a Syrian.

Mimi ni binadamu kabla sijawa Msyria.

Say no to racism. Lebanon is a small country, but with a big heart.

Kataa ubaguzi wa rangi. Lebanoni ni nchi ndogo, lakini ina moyo mkubwa.

90% of our houses are built by Syrians. Stay a racist and leave your house.

Asilimia 90 ya nyumba zetu zimejengwa na Wasyria. Kama ni mbaguzi wa rangi, ondoka kwa nyumba hizo.

Baadhi hata walienda mbali na kulaumu historia iliyoachwa na wakoloni.

Whoever divided these grounds for 'immigrants' to cross borders to another country... I won't say 'welcome' because this is not just my country.

Yeyote aligawanya ardhi kwa ‘wahamiaji’ kuvuka mpaka kwenda kwenye nchi nyingine…siwezi kusema ‘karibu’ kwa sababu hii si nchi yangu.

Na hata wananing'iniza bango kwenye barabara kuu:

Dear Syrian, welcome! welcome to Lebanon

Mpenzi Msyria, Karibu! Karibu kwenye moyo wa Lebanon

1 maoni

  • […] Walebanoni Wazindua Kampeni ya Kuwatetea Wasyria Dhidi ya Ubaguzi wa Rangi Kampeni ya kuwatetea Wasyria wanaokabiliwa na ubaguzi wa rangi (Kwa kiarabu: الحملة الداعمة للسوريين بوجه العنصريّة) ilizinduliwa mnamo Machi 21, 2014, katika siku ya kimataifa ya Kuondoa Ubaguzi wa rangiwas, “katika kukataa aina zote za unyanyasaji dhidi ya Wasyria waishio Lebanon, hotuba za kisiasa zenye sura ya ubaguzi na matangazo yanayohusiana na ubaguzi huo kwenye vyombo vya habari.” Kwa maneno mengine, inakusudia kukabiliana kile kinachoifahamika kuwa kukua kwa ubaguzi dhidi ya wakimbizi wa Syria wanaoishi Lebanoni. Wanasiasa wa Kilebanoni wanatuhumiwa na wanaharakati kwa kutumia migogoro kati ya wakimbizi wa Syria na wenyeji wa baadhi ya maeneo ya Lebanoni kwa makusudi ya kisiasa. Baada ya kampeni ya “Mimi si Mhafidhina” kwa heshima ya Mohammad Chaar na kampeni ya “Mimi si uchi” kumwuunga mkono Jackie Chamoun mshindi wa Olimpiki wa Mchezo wa Kuteleza kwenye barafu na kisha dhidi ya Unyanyasaji wa Majumbani, kampeni ya kupinga ubaguzi wa rangi inatumia namna inayofanana (kwa sasa ni ile ile) ya kuonyesha upinzani mtandaoni kwa kuwaonyesha wananchi wakiweka habari na picha zao zenye kubeba ujumbe. Akizungumza na gazeti maarufu la Kilebanoni linaloandikwa kwa lugha ya Kifaransa “L'Orient-le Jour”, mmoja wa wanaharakati wanaoshiriki kwe… Kusoma makala kamili  »  http://sw.globalvoicesonline.org/2014/03/walebanoni-wazindua-kampeni-ya-kuwatetea-wasyria-dhidi-ya-ubaguzi-wa-rangi/ […]

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.