Je, Mwigizaji Maarufu Urusi Amempinga Vladimir Putin?

Russian actor Konstantin Khabensky. YouTube screenshot.

Mwigizaji wa Kirusi Konstantin Khabensky. Picha imepigwa kwenye mtandao wa YouTube.

Konstantin Khabensky ni mmoja wapo wa waigizaji maarufu zaidi nchini Urusi. Watazamaji wake wa kimataifa wanafahamu kwa kucheza kama mhusika mkuu kwenye filamu za Night Watch na Day Watch zilizoongozwa na Timur Bekmambetov. Pia alichea kama mshiriki kwenye filamu za kimagharibi kama Tinker Tailor Solider Spy na Wanted. Jana Machi 16, 2014, siku moja kabla ya kura ya maoni ya kujitenga kwa Crimea, ujumbe ulionekana kwenye ukurasa wa mtandao wa kijamii unaosadikiwa kumilikiwa na Khabensky, ambapo mwigizaji huyo alimpinga Vladimir Putin na kuonyesha kuiunga mkono Ukraine. Katika mabandiko yaliyofuata, Khabensky alibainishakuwa barua za chuki zilijazana kwenye sanduku lake la kusomea barua, baada ya kuonyesha kuwa shabiki wa Ukraine.

Katika nchi nyingi, matamshi ya kisiasa yanayomkosoa rais aliyeko madarakani ni jambo la kawaida. Nchini Urusi, ni nadra sana kwa mtu yeyote anayeonekana kwenye televisheni mara nyingi kumkosoa, achilia mbali kumpinga, Vladimir Putin. Kwa hakika, watu maarufu kama Khabensky wanauwezekano mkuba wa kumsifu Rais nyakati za migogoro ya kimataifa.

Kwa mfano, zaidi ya watu maarufu wa kiutamaduni wapatao mia tano hivi karibuni walitia saini barua ya wazi kuunga mkono msimamo wa Putin kuhusiana na “Ukraine na Crimea.” Barua hiyo, iliyokuwa na orodha ya watia saini ilichapishwa kwenye tovuti ya Wizara ya Utamaduni. Gazeti la Upinzani Novaya Gazeta mara moja  lilijibu> kwa kuandaa barua yake ya wazi pia, likikusanya saini kutoka kwa watu maarufu wanaopinga vita, ikiwa ni pamoja na waigizaji na wanamuziki, lakini pia likiwajumuisha waandishi wanaotaka mabadiliko.

Umaarufu wa Khabensky na lugha yenye ukakasi aliyoitumia kumshutumu Kremlin, hata hivyo ililifanya tamko lake kuwa maalumu. Lilikuwa tamko la mtu ambaye ni alama ya kweli ya utamaduni –na sio minong’ono ya baadhi ya tamaduni ndogo za Kirusi. Khabensky alisaidia kufanya michezo ya Olimpiki ya Sochi Olympics kuwa ya pekee, ambapo alitia sauti matangazo kwa ajili ya MegaFon na alionekana kwenye video ya Olimpiki iliyowahusisha waigizaji maarufu wa Urusi walioweka historia kwa nyakati tofauti nchini Urusi. Kwa hakika, tovuti ya habari ya NewsRu.com ililifanya tangazo la Khabensky kuwa habari kuu. (Wakati wa kuandikwa kwa posti hii, makala hayo bado inapatikana.)

Kuna sababu kubwa ya kuwa na mashaka, hata hivyo, kuwa Khabensky hakuandika makala hayo ya kuishabikia Ukraine, kumpinga Putin kwenye mtandao wa Vkontakte. Anuani husika inadai kuwa “ukurasa rasmi,” kwa kuweka alama angavu ya kijani, ingawa hii si namna ambayo mtandao wa Vkontakte hutambulisha kurasa maalumu. Chunguza sera za ukurasa huo na utaona kuwa Vkontakte inatambulisha kurasa maalumu kwa kuweka alama za bluu baada tu ya jina la mtumiaji wa mtandao huo upande wa kulia. (Tazama ukurasa wa Waziri Mkuu Dmitri Medvedev kuona mfano hai.)

Kwa maneno mengine, ukurasa wa Khabensky wa mtandao wa Vkontakte haujathibitishwa, lakini mmiliki wa anuani hiyo alitaka wasomaji wadhanie hivyp. Hiyo yapasa kuibua mashaka: huenda ukurasa huo ni batili.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.