Mwandishi wa Habari wa Ethiopia Reeyot Alemu Amefungwa Jela kwa Siku 1,000

Machi 16, 2014 inakuwa ndiyo siku ya 1,000 ya kufungwa kwa mwandishi wa Ethiopia Reeyot Alemu. Anatumikia kifungo cha miaka mitano jela baada ya kutiwa hatiani katika mashitaka ya ugaidi mwezi Januari 2012.

Jailed Ethiopian journalist Reeyot Alemu.Photo source: Facebook page of Free Reyoot Alemu campaign.

Mwandishi wa Ethiopia aliyefungwa Reeyot Alemu. Picha kupitia ukurasa wa Facebook wa kampeni ya Kuachiwa kwa Reyoot Alemu.

Reeyot, mwalimu wa Kiingereza, alipokea Tuzo ya UNESCO-Guillermo Cano ya Uhuru wa Habari Duniani, Tuzo ya Hellman/Hammett, na Tuzo ya Mwandishi Jasiri ya Mfuko wa Habari wa Kimataifa kwa Wanawake.

Kwa mujibu wa Kamati ya Kulinda Waandishi (CPJ), serikali ya Ethiopia imehukumu waandishi na wanablogu huru wapatao 11 ikiwa ni pamoja na Reeyot na Eskinder Nega chini ya sheria ya kupambana na ugaidi tagu mwaka 2011. Katika waliofungwa ni pamoja waandishi wawili wa Sweden wanaotumikia kifungo cha miaka 11 kwa kudaiwa kukisaidia kikundi cha Waasi wa Kabila cha Kisomali.

Katika posti hii ya blogu, mwanablogu BefeQadu Z Hailu alielezea hatari ya kufungwa inawakabili waandishi wa habari wa Ethiopia:

Kama lengo la kifungo ni kuwasahihisha waliohukumiwa, basi kusisitiza kusoma na elimu yapaswa kuwa ni nyenzo ya kufikia lengo hilo. Katika gereza la Kality vyote hivyo vinaruhusiwa lakini si kirahisi kwa waandishi hawa na wengine waliohukumiwa kwa makosa yanayohusishwa na “ugaidi”.

Wafungwa hawa hawaruhusiwi kupata vitabu. Eskinder anasema, “Hususani vitabu vile vyenye vichwa vya habari vinavyounganisha maneno ‘Ethiopia’ na ‘Historia’ haviruhisiwi”. Hali ni hiyo hiyo kwenye gereza aliko Reeyot Alemu na wengine kama Wubshet Taye, Bekele Gerba, na kadhalika.

Magazeti na majarida huru yanayochapishwa nchini humo hayaruhusiwi gerezani; Eskinder alinieleza zaidi kwamba hata cheneli za TV kama BBC na Aljazeera haziruhusiwi kutazamwa kwenye maeneo ambayo yeye na wenzake wamefugwa.

Reeyot Alemu, baada ya mapambano magumu na utawala wa gereza na baada ya vyombo vya habari kufunua ukweli huo, sasa anaruhusiwa kupata masomo kwa njia ya masafa. Ila, bado ni vigumu kwake kupata vitabu vya ziada ukiacha vile anavyotumiwa moja kwa moja kutoka chuoni.

Watumiaji wa mtandao wa twita walituma twiti kwa kutumia alama habari  #ReeyotAlemu kuonyesha mshikamano wao kwa mwandishi huyo aliyefungwa. Hapa chini ni baadhi ya twiti zilizotumwa:

Naamini dunia inamjali pia! Bado nasubiri kuona kampeni yoyote!

Serikali ya Ethiopia inaendelea kuonyesha udhaifu na hofu wakati waandishi wa aina ya #ReeyotAlemu wanapowasha taa kuimulika. Mwachieni huru

Kwa nini madikteta wa dunia ya tatu wanawaogopa sana waandishi wa habari kuliko hata kifo? Ni dalili za udhaifu. Wanaogopa maoni mapya na watu wenye maoni.

Siku ya 1,000 kwa Mwandishi ReeyotAlemu gerezani leo. Amenyimwa haki ya kutembelewa na familia yake. Hivi kwa nini Umoja wa Ulaya iko kimya katika suala hili la Ashton?

Machi 16 ni siku ya 1000 ya kifungo cha ReenyotAlemu na inaonyesha namna Ethipia inavyotawala kiimla, uonevu na kwa unyanyasaji

Uandishi si ugaidi. Mwachieni huru mwandishi Reeyot Alemu aliyetunukiwa tuzo kibao, mpeni huduma za afya [kama mwanamke]

1 maoni

  • […] Mwandishi wa Habari wa Ethiopia Reeyot Alemu Amefungwa Jela kwa Siku 1,000 Machi 16, 2014 inakuwa ndiyo siku ya 1,000 ya kufungwa kwa mwandishi wa Ethiopia Reeyot Alemu. Anatumikia kifungo cha miaka mitano jela baada ya kutiwa hatiani katika mashitaka ya ugaidi mwezi Januari 2012. Mwandishi wa Ethiopia aliyefungwa Reeyot Alemu. Picha kupitia ukurasa wa Facebook wa kampeni ya Kuachiwa kwa Reyoot Alemu. Reeyot, mwalimu wa Kiingereza, alipokea Tuzo ya UNESCO-Guillermo Cano ya Uhuru wa Habari Duniani, Tuzo ya Hellman/Hammett, na Tuzo ya Mwandishi Jasiri ya Mfuko wa Habari wa Kimataifa kwa Wanawake. Kwa mujibu wa Kamati ya Kulinda Waandishi (CPJ), serikali ya Ethiopia imehukumu waandishi na wanablogu huru wapatao 11 ikiwa ni pamoja na Reeyot na Eskinder Nega chini ya sheria ya kupambana na ugaidi tagu mwaka 2011. Katika waliofungwa ni pamoja waandishi wawili wa Sweden wanaotumikia kifungo cha miaka 11 kwa kudaiwa kukisaidia kikundi cha Waasi wa Kabila cha Kisomali. Katika posti hii ya blogu, mwanablogu BefeQadu Z Hailu alielezea hatari ya kufungwa inawakabili waandishi wa habari wa Ethiopia: Kama lengo la kifungo ni kuwasahihisha waliohukumiwa, basi kusisitiza kusoma na elimu yapaswa kuwa ni nyenzo ya kufikia lengo hilo. Katika gereza la Kality vyote hivyo vinaruhusiwa lakini si kirahisi kwa waandishi hawa na wengine waliohukumiwa kwa makosa yanayohusishwa na “ugaidi”. Wafungwa hawa… Kusoma makala kamili  »  http://sw.globalvoicesonline.org/2014/03/mwandishi-wa-habari-wa-ethiopia-reeyot-alemu-amefungwa-jela-kwa-siku-1000/ […]

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.