“Si rahisi kuwa Mhindi” nchini Marekani

Ricey Wild, Mmarekani wa asili anayeblogu kwenye blogu ya Indian Country Today, anandika kuhusu kuuawa kwa mbwa mwitu kwenye jimbo la Minnesota, Marekani.

[…]Rafiki yangu mpenzi Melissa alikuja kunichukua mwezi uliopita kwenda kwenye mkutano wa kupinga uwindaji wa mbwa mwitu kwenye jimbo la Mennesota na kwingineko. Tulipanda kaskazini na kuungana na wengine wanaojali na kukerwa na uuaji unaofanywa dhidi ya idadi ya mbwa mwitu.

[…]Ninamwangalia Mitzi wangu na siwezi kusema kuwa ndugu zake wa karibu wanajisikia vyema kuua kwa sababu tu ya kuua. Nikatafakari eneo la Mitzi likiwa linanyemelewa na ‘wawindaji’ na kushangaa kipi hasa alichowahi kuwafanya? Kwa nini wanawaua ndugu zake? Ndio, nililia na kuapa kuifanya sauti yangu na uwepo wangu uonekane bayana…

Posti yake ya awali, yenye jina “Si rahisi kuwa Mhindi”, ilichapishwa Desemba 2013 na unaweza kuipata hapa

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.