Pakistan, Usiingilie Vita vya Ndani ya Syria

Siku moja baada ya dondoo ndogo ya habari yenye kichwa cha habari, “Saudi Arabia ‘inatafuta uungwaji mkono kwa waasi wa” ilipoonekana kwenye magazeti ya Pakistani, mwanablogu wa siasa Ahsan Butt aliposti tahadhari kali kwa watunga sera ya mambo ya Kimataifa wa nchi ya Pakstani kuachana na mambo ya ndani ya Syria.

Katika makala ya “Hii siyo vita yetu (Toleo la Syria)” kwenye blogu ya Five Rupees, Ahsan anaandika:

Kile ambacho Pakistani inakifanya kinyume cha Syria ni moja wapo ya mambo ya kijinga kabisa kuwahi kufanywa na Pakistani kwa muda mrefu, na ambalo linatuma ujumbe muhimu. Vita vya wenyewe kwa wenyewe Syria, hatika hali mbaya ilivyo, haihusu Pakistani kwa vyovyote vile. Pakistani haina maslahi yoyote kwenye mgogoro huo. Hakuna.

Saudi Arabia iko kwenye mazungumzo na Pakistani ili kutoa ndege na roketi za kivita zilizotengenezwa Pakistani. Ahsan anaonya:

Hivi ni busara na inashauriwa kweli kujiingiza kwenye vita vya ndani ya nchi iliyo kwenye umbali wa maili elfu mbili?[…]

Hebu saili mwenendo wa ghasia hizi katika muongo uliopita.

Anaeleza kuwa hatua yoyote ya kuingilia mambo ya Syria itailazimisha serikali ya Pakistani kuanza kutazama kwa makini kukua kwa ghasia za kidini ndani ya nchi:

Yepi ni madhara yanayowezekana kutokana na sera za aina hiyo linapokuja suala la ghasia za kidini nchini Pakistani? Je, inawezekana ikachochea misuguano ya kidini au kinyume chake?

Ahsan anaorodhesha maswali manne ya kufikirisha zaidi ambayo unaweza kuyasoma hapa.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.