Mwandishi Mwandamizi wa Kichina Akosolewa kwa Kujifungulia Marekani

Mmoja kwa waandishi wa wanaoheshimika nchini China na mgwiji wa televisheni, Chai Jing, amesababisha moto mkali mtandaoni baada ya kujifungulia Marekani, huku watumiaji wengine wa mtandao wakimwita “msaliti” au “mnafiki”.

Baada ya picha za Chai akiwa amembeba mwanae mchanga uwanja wa ndege kuchapishwa mtandaoni, taarifa zilisambaa kwamba alikuwa amejifungua mtoto wa kike nchini Marekani mwezi Oktoba 2013. Ilivyo, faida ni kwamba mtoto huyo anakuwa raia wa Marekani.

Mtangazaji huyo anayeheshimika sana nchini China, Chai anafahamika kwa weledi wake, ufuatiliaji na mbinu yake ya kuhoji bila kona, na kujielekeza kwenye hoja moja kwa moja. Amejitengenezea jina kwa kutangaza habari za mlipuko wa mafua ya ndege (SARS) mwaka 2003 na tetemeko la Sichua mwaka 2008.  

Chai Jing holding a newborn baby at an airport (Picture from Sina Weibo)

Chai Jing akiwa amembeba mwanae alipokuwa uwanja wa ndege. Picha ya Sina Weibo

Kitendo cha Chai kujifungulia nchini Marekani kimewakatisha tamaa mashabiki wake wengi, huku wengi wakimwita mnafiki.   

Mtumiaji wa mtandao ajiitaye “Tan” aliandika:

我们应该明白一点,公知们抨击或批评这个生他养他的国家,不是爱这个国家而是为了有天有扑向美欧等国家怀抱的资本。什么人批评这个国家的不足才是真心的?只有永远是中国人的我们。

Tufike mahali tuelewe kuwa hawa watu maarufu wana tabia ya kushambulia na hata kuzikosoa nchi zao walikozaliwa, si kwa sababu wanaipenda nchi hii lakini kwa sababu siku moja wanaweza kujikuta wakihamia Marekani, Ulaya na hata kwenye nchi nyinginezo. Watu gani wanaoikosoa nchi hii wanamaanisha? Ni wale tu ambao siku zote watabaki kuwa wa-China.

Hata hivyo, idadi kubwa ya watu waliunga mkono kitendo hicho. Wengine wakisikitishwa na tabia inayoshika kasi ya kuhama nchi miongoni mwa watu wa tabaka la kati, wakitoa mwito kwa viongozi waandamizi nchini China kutafakari:

不懂怎么念燊微博达人:非常现实,高层应该反思为何这样,柴静看到未来,她有能力为自己孩子选择一个更为公平公正,制度健全的国家,别人没道理评论。想想自己有能力会不会加入美国籍就懂了。

Ni ukweli kabisa, kwamba vigogo wajitafakari kwa nini mambo yamekuwa hivi. Tunapotafakari siku za mbeleni, (Chai) anaweza kuchagua nchi yenye mfumo wa haki, usawa na unaoeleweka kwa ajili ya mwanae. Hili si suala la mtu yeyote kulitolea maoni. Kama una uwezo, je ungependa kuwa raia wa Marekani? Tafakari sana na utaelewa.

文人医生:自己不能改变现状,手中没有选票,为什么孩子还不能改变?柴静在哪里生孩子是自己的自由和私事。

Sisi wenyewe hatuwezi kubadilisha hali ya mambo tuliyoizoea nchini humu, hatuna kura, sasa kwa nini tusifanye mabadiliko kwa watoto wetu? Ni uhuru wa Chai Jing na ni juu yake mwenyewe kuamua wapi mwanae azaliwe.  

Mchambuzi Liu Xuesong aliandika [zh]:

个人爱不爱这个国家,最重要的不是看他把孩子生在哪里,而是看他在这个国家的公民角色中,担了多少当,做了多少有益的事。这个国家值不值得爱,倒是与这个国家的集体意识中,是否展示了大爱的包容、和谐、友善等宽厚本色,是否将注意力放在了富强、公正、文明等向上向善的追求上有关。

Ikiwa ni uzalendo au sivyo, jambo la muhimu si kujua wapi mtoto alizaliwa, lakini muhimu ni kutazama wajibu wake kama raia wa nchi hii, na vingapi vizuri amevifanya kwa ajili ya nchi hii. Kwamba ni muhimu kuipenda nchi hii ni suala la dhamira ya jumla ya watu wa nci hii, kwamba inaonyesha upendo, ushirika, urafiki na ukarimu na ikiwa lengo ni mafanikio, haki na ustaarabu.

Mtumiaji mwingine wa mtandaoni aliandika [zh]:

有网民说,他只是希望孩子有比较正常的生活方式,无关爱国。也许,这才是为政者应该反思的问题。

Baadhi ya watu walisema kwamba [Chai] anataka mwanae awe na mtindo wa kawaida wa maisha, kitu ambacho hakina uhusiano na uzalendo. Labda, hili ndilo tatizo ambalo serikali yapaswa kulitafakari.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.