Ghasia za Ukraine: “Kijana Alifia Mikononi Mwangu”

From the roof of Globus shopping center

The view over Independence Square from the roof of Globus shopping center in Kyiv, Ukraine (February 19)
Photo by Anastasia Vlasova © Copyright Demotix

Mwanafunzi jijini Kyiv, Ukraine alitwiti kuanzia alfajiri mpaka usiku wa manane wakati wa siku ya mapigano kati ya waandamanaji na polisi yalisababisha vifo zaidi ya 25 na mamia wengine wakijeruhiwa.

Siku ya leo, Februari 18, 2014, Bunge la Ukraine limeshindwa kudhibiti mamlaka ya Rais Viktor Yanukovych, mlengwa mkuu wa maandamano hayo yaliyoendelea kwa miaezi mitatu kwenye viwanja vya Maidan Nezalezhnosti.

Hapa chini ni twiti zilizochaguliwa na @Mira_mp ambaye ni shuhuda wa matukio hayo, na baadae akijitolea kuwasaidia wajeruhi hospitali.

Twiti zake za kwanza zinaonyesha sura kamili ya namna mapigano yalivyoanza:

Inaonekana kama nitavuta hewa iliyojaa moshi wa mabomu ya kutoa machozi, kwa mara nyingine.

Kwenye mtaa wa Hrushevskogo [ambako mapigano yalianzia mwezi uliopita] matairi yanachomwa tena)

Kwenye bustani ya [Mariinsky] watu wanapiga kelele “watumwa!” kwa titushki [wahuni waliokodiwa na serikali kuwapiga na kuwadhalilisha waandamanaji] na kuwaonyesha noti)) wanakasirika na kuondoka

Hema kwenye bustani ya [Mariinsky] linaungua sasa hivi. Kwa ujumla, haijulikani nini kinaendelea hapa na mtandao wa simu za mkononi unapatikana kwa shida.

Twiti zake zilizofuatia alizituma akiwa anaelekea hospitali. Muda halisi unaonyesha kwamba ilikuwa ni baada ya polisi na vikosi maalumu vya kutuliza ghasia vilipoanza kupambana na waandamanaji karibu na jengo la Bunge.

Tunaelekea hosptali. Marafiki wawili wa baba yangu wamejeruhiwa vibaya -mmoja kichwani na mwingine mononi. Mapinduzi haya yanageuka kuwa vita.

Kuna wasiwasi kuwa polisi wanaweza kuanza kuwakamata wale wanaotoa taarifa za majeruhi, na akatwiti:

Labda inawabidi kutokwenda hosptali. Waishie kwenye duka la dawa, watibu majeraha yao na warudi nyumbani.

Baadae, alirudi Maidan kufuatilia matukio yanayoendelea bungeni.

Sasa tumerudi Maidan. Ninaamini Bo amepata fahamu tena, ana jeraha kichwani.

Tulikuwa tunatazama matangazo ya moja kwa moja kutoka [bungeni]. Bibi mmoja anasema: “Hawa ni wapumbavu ambao wajirani zangu waliwapigia kura? leo watakuwa kwenye matatizo!” Ninawapenda watu wa namna hii!)

[Watu] wanafuatilia matangazo ya Maidan. Wanawake kwa wanaume bila [kofia za kukinga kichwa na nguo nyingine za kujikinga] hawaruhusiwi kuingia.

Rybak [Spika wa Bunge] amechukuliwa na gari la wagonjwa. Hasira za waandamanaji -hivi kuna anayejua gari hilo ni lipi? inabidi tusherehekee!

Watu watatu [waliripotiwa] kuuawa. Maandamano ya amani yamegeuka kuwa vita.

Berkut [kikosi cha kutuliza gahsia] wanaturushia risasi hovyo na wanarusha mawe kutokea kwenye eneo la maduka ya Globus.

Kundi kubwa la watu wako mtaani. Treni imesimamisha huduma zake, watu wengi wanatembea kuelekea Maidan.

saa 12 kasoro dakika 7 [saa ya mwisho ambayo serikali iliweka kwa waandamanaji kuondoka]. Ninajivunia bila kipimo kila mtu aliyeendelea kubaki Maidan! Kuna wazee na wanawake hapa!

Kwa jinsi polisi wa kutuliza ghasia wanavyoshambulia Maidan majeruhi kadhaa waliripotiwa maeneo yote. Waandamanaji waliwaomba wanawake na watoto kuondoka kwenye maeneo yenye ghasia.

Siwezi kukaa nyumbani. Naenda hospitali kwenye mtaa wa Shovkovycha.

Siwezi kuwadanganya wazazi na Dan. Lakini siwezi kukaa mbali na eneo la Maidan vile vile. Zima simu na hakuna swali litaulizwa.

Twiti yake iliyofuata ilikuwa ni wakati ametoka hospitali.

Madaktari hawajasema lolote kuhusu hali ya Bo. Siwezi kusoma habari mpya kwenye [twita] na betri yangu imekwisha. Nitakutana navyi huko

Tumekuja hospitali chumba namba 17. Kuna idadi kubwa sna ya majeruhi hapa! Wakazi wa jiji la Kyev wamekuja na kuwachukua wale wenye majeraha madogo

Damu inatiririka na miili ya watu waliokufa imetapakaa. Huu ni usiku wa kuogofya kuliko siku zote kwenye maisha yangu.

Kijana aliyepigwa risasi kichwani na tumboni amefia mkononi mwangu. Sitausahau usiku huu.

Posti hii ni sehemu ya habari zetu maalumu kuhusu Ghasia za Ukraine.

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.