Mwanaharakati wa Misri Alaa Abd El Fattah Akamatwa — Tena

Alaa Abd El Fattah. Photo by Alaa And El Fattah via Wikimedia Commons (CC BY-SA 2.5)

Alaa Abd El Fattah. Picha kwa hisani ya Alaa And El Fattah kupitia Wikimedia Commons (CC BY-SA 2.5)

Mwanaharakati mashuhuri nchini Misri na mwanablogu Alaa Abd El Fattah alikamatwa akiwa nyumbani kwake takriban saa nne jioni mnamo Alhamisi, Novemba 28. Hati ya kukamatwa Abd El Fattah ilitolewa Jumanne iliyopita, kufuatia kusambaa kwa vurugu ya waandamanaji mjini Cairo. Baba mzazi wa mwanablogu huyo aliviambia vyombo vya habari nchini humo kuwa aliamini kukamatwa kulikuwa ni kutekeleza sheria mpya iliyotungwa kupiga marufuku maandamano mitaani nchini Misri. Takribani watu 51 walikamatwa siku hiyo, miongoni mwao wakiwemo wanaharakati kadhaa maarufu. Wengi walipigwa na kunyanyaswa kijinsia.

Alaa alichukuliwa na polisi licha ya kuwa alitangaza kwamba yeye ndiye angejisalimisha kwa polisi siku ya Jumamosi, kulingana na taarifa aliyoitoa na ambayo shangazi yake, mwandishi mashuhuri wa misri Ahdaf Soueif, aliiweka kwenye mtandao wa Facebook.

Kulingana na taarifa ya mkewe, polisi wa Manal walitumia nguvu na vurugu wakati kukamatwa:

Hakuna maelezo rasmi ya sababu ya kukamatwa kwake leo, hiyo ni kwa kuwa Alaa alikuwa ametangaza hadharani kuwa angejisalimisha mwenyewe siku ya Jumamosi.

Mkurugenzi wa Shirika la Utetezi wa Haki za Binadamu nchini Misri Heba Morayef alihusisha kukamatwa kwake na sheria ya kupambana na maandamano, ilitungwa mapema wiki hii:

Hesham Mansour alitoa majibu yake mwenyewe ya kejeli:

Usiulize nini Misri imefanya kwa ajili yetu. Uliza mara ngapi Misri imemkamata Alaa

Mwanaharakati Mona Seif, dadake Alaa, alitoa taarifa kwa wafuasi wake eneo ambalo kakake amewekwa kizuizini:

Sisi sasa tuna uhakika kwamba Alaa anashikiliwa katika kambi ya CSF katika Giza, mjini Cairo – barabara ya Alexandria

Alaa Abd El Fattah alifungwa jela chini ya utawala wa Hosni Mubarak kwa siku 45 na tena na Baraza Kuu la Vikosi vya Jeshi mwaka 2011, ambapo yeye alibakia jela kwa karibu miezi miwili. vilevile alikakabiliwa na mashtaka chini ya utawala wa Mohamed Morsi mwaka wa 2013, pamoja mwandishi maarufu anayetumia jina la uandishi Bassem Youssef, katika kile wengi walijua kuwa mashtaka ya kisiasa kutumika kama mbinu ya vitisho. Kila mara, #FreeAlaa alama ashiria huibuka kuonyesha mshikamano. Inaonekana kwamba hali hii imerudi tena.

2 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.