Mnamo Octoba 26, 2013 maelfu yaa wanawake wa ki-Saudi wameapa kuvunja amri ya Ufalme kuwazuia wanawake kuendesha magari.
Katika toleo la GV Face wiki hii, tunakutana na mwanablogu wa Jeddah na mwandishi Tamador Alyami, anayeunga mkono kampeni ya #WanawakeWataendesha.
Tumezungumzia kampeni hiyo, maisha ya wanawake nchini Saudi, na jinsi wanaharakati walivyowachukulia wapinzani wa kampeni hiyo kama alivyofanya mhubiri mmoja siku za hivi karibuni aliposema, “tumegundua kuwa wale [wanawake] wanaoendesha magari wanajifungua watoto wenye vilema vya aina mbalimbali.”
GV Face inaandaliwa na Mhariri Mtendaji Solana Larsen na Mhariri Msaidizi Sahar Habib Ghazi.
Pia unaweza kusoma:
Septemba 2013 Imamu wa Saudi aeleza Sayansi mpya ya sababu ya wanawake kuzuiwa kuendesha
Sep 2013 Octoba 26: Siku ya kuvunja amri ya Saudi kuwazuia wanawake kuendesha
Octoba 2012 Saudi Arabia: Kampeni ya Wanawake Kuendesha Yapamba moto; Yalaumu sera za serikali
Novemba 2011 Saudi Arabia: Hasira dhidi ya Makofi 10 kwa dereva mwanamke
Juni 2011 Saudi Arabia: Wanawake kwenye Usukani
Mei 2011 Saudi Arabia: Wanawake Wawekwa kizuizini kwa Kuendesha
Mei 2011 Saudi Arabia: Mwanamke Apingana na sheria kwa Kuendesha mjini Jeddah