Hotuba ya Obama kwenye Mahafali Yaibua Mjadala wa Maana ya Uraia

Makala haya yaliyoandaliwa na Rachel Wang kwa mara ya kwanza kabisa ilionekana kwenye jarida la Tea Leaf Nation siku ya Mei 13, 2013 na inasambazwa tena kwa makubaliano ya usambazaji [Mtindo wa uandishi umerekebishwa kurahisisha ufasiri].

Wiki iliyopita, hotuba iliyotolewa na Rais wa Marekani Barack Obama kuhusiana na uraia ilizua mjadala mkubwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii nchini China.

Mtumiaji mwenye ushaeishi mkubwa kwenye mtandao wa Sina Weibo @假装在纽约, au “kujifanya Nipo New York,” mchambuzi wa mambo aliye na wafuatiliaji wengi kutoka sehemu mbalimbali ambaye mara nyingi amekuwa akitwiti kuhusiana na Marekani na ambaye ukurasa wake unatembelewa na watu zaidi ya 470,000 alipendekeza [zh] hotuba hii kwa vijana wa China:

(Official White House Photo by Pete Souza)

(Picha rasmi ya Ikulu ya Rais iliyopigwa na Pete Souza)

奥巴马昨天在俄亥俄州立大学的毕业典礼上演讲,演讲的核心是“公民意识”。我把他的演讲稿匆匆翻译了下来,就是觉得,中国的年轻人,也许更应该接受这样在中国的课堂里接受不到的教育。

Kiini cha hotuba aliyoitoa Obama jana katika Chuo Kikuu cha Ohio wakati wa mahafali kilikuwa ni ‘fafsiri ya uraia, nilijitahidi kutafsiri hotuba yake kwa kuwa ninahisi kuwa vijana wa China kwa namna moja ama nyingine wanahitaji aina hii ya elimu ambayo hawaipati mashuleni nchini China.

Katika hotuba yake wakati wa mahafali yaliyofanyika Mei 5, 2013, Rais Obama alisema , ” Sisi siyo kusanyiko la watu tusiofahamiana… tunaunganishwa pamoja kwa kanuni mbalimbali za maisha, sheria na makubaliano.” Makala ya mtumiaji huyo ajiitaye ”Kujifanya nipo New York”, pamoja na tafsiri ya hotuba ya Rais Obama, iliwavutia zaidi ya watu 30,000 walioendelea Kutwiti makala hii pamoja na maoni takribani 6,000 kwa muda wa siku mbili.

Pamoja na kuwa, hii si mara ya kwanza kwa watumiaji wa mtandao nchini China kulinganisha hali ya mambo kati ya China na Marekani, wazo la “uraia” kwa mara nyingine tena limeibua mijadala sehemu mbalimbali kuhusiana na haki na wajibu wa watu wa China pamoja na hali ya kuikosoa serikali. Yin Hong (@尹鸿), Mkuu wa kitengo cha Uanahabari na Mawasiliano cha Tsinghua alitoa maoni [zh] yake:

虽然不算是一篇最好的讲演,但公民意识表述很清楚:每一个人都拥有天赋人权,所以每一个人也都具有天赋义务。这就是公民。没有人权,就就不能有义务。权力和义务是相对对等的。

Pamoja na kuwa hii siyo hotuba bora kabisa, ‘ufahamu wa uraia’ umefafanuliwa vizuri sana: kila mmoja ana haki zake za asili, na pia, kila mmoja ana wajibu wake wa asili. Huu ndio uraia. Bila haki za binadamu, kusingekuwa na wajibu. Haki na wajibu ni mambo yanayotegemeana.

Mtumiaji mwingine wa Weibo, “Niliwahi kuwa Bonge” (@曾经的胖胖胖胖), aliandika:

为什么中国人缺少公民意识,因为他们不觉得这个政府跟他们有关系,而且事实上这个政府也的确不是来自选票……

Kwa nini wa-China wengi wanakosa ufahamu wa uraia? Ni kwa sababu hawaoni lolote ambalo serikali inaweza kuwafanyia, na kwa hakika, serikali siyo chombo kilichochaguliwa.

“Dragon Ash” (@龙团一灰) alitoa maoni yake [posti ya asili kwa lugha ya ki-China imefutwa],

Kuwa katika nchi ya ujamaa, hatuwezi kuyawazia mambo ya namna hii, kadiri ya unavyoyatafakari mambo haya, ndivyo utakavyozidi kujisikia vibaya. Hali kadhalika kwa haki, chochote kinachosemwa na wafanyakazi wa umma kinapita.

Mitizamo ya watu kwenye maoni kuhusiana na hotuba ya Rais Obama ilionekana dhahiri kuvuka mipaka ya husuda, wivu na hali ya kusikitisha. Pia walihusisha mijadala kuhusiana na juhudi, changamoto na magumu ambayo vijana wa kileo wa China wanayokabiliana nayo. Mtumiaji wa Weibo “Big Guy Moving Like Dragon and Tiger” (@大背头龙行虎步 aliandika [original Chinese post deleted]:

Vijana wameanza kuwa na tumaini la ufahamu wa uraia, lakini mara baada ya kukutana na vizingiti mara kwa mara katika jamii, wanahamia kwenye kutegemea ndugu hususani katika kutafuta ajira. Hili ni “bakuli la supu ya soya” la ki-China, ambapo kila jambo linaishia kuharibika bila kujali namna ambavyo jambo hilo lilivyoanza. Kizazi kimoja baada ya kingine, huu ndio utamaduni wetu wa jadi: utawala wa mabavu, utawala wa amri pamoja na kukosa uvumilivu wa upinzani, madhara ya utamaduni yanaenda kutushinda, demokrasia inaweza kuwepo baada ya karne moja zaidi.

“Hula Baopei” (@呼啦啦啦宝宝_佩) aliwaza kuwa:

当国内大学生一毕业便面临高房价、物价而不得不屈服于现实失去梦想时,美国青年却可以以祖国未来为己任,被赋予强大的公民意识,坚定不移的实现自己的梦想、承担国家发展之重任,我在想中国的未来在哪里?下一代的未来在哪里?

Wakati wahitimu wa vyuo vya China wakishindwa kuukubali ukweli na kuzisahau ndoto zao kufuatia kukabiliana na gharama kubwa za vitu pamoja na kushindwa kulipia gharama za pango la nyumba mara baada ya kutoka vyuoni, vijana wa Marekani wanaweza kuuchukua mustakabili wa nchi yao kama sehemu ya mikakati yao; wameshajengewa ufahamu imara wa uraia, wanafikia malengo yao kwa haraka na pia wanawajibika kwa ajili ya maendeleo ya nchi yao. Ninashangaa, mustakabali wa China uko wapi? Mustakabali wa kizazi kijacho uko wapi?

Mambo haya yanaweza kuwa katika muda muafaka, kwani vijana wengi nchini China siku za hivi karibuni watahitimu mafunzo yao. Labda kwa wahitimu wa vyuo wa siku za hivi karibuni, jambo kubwa linalowakabili si namna ya kulibadilisha taifa, bali namna ya kuhimili hali ya uchumi inayosikitisha. Kwa hakika, mwaka 2013 unaaminika kuwa ni kipindi kigumu sana na mambacho hakikuwahi kushuhudiwa cha kutafuta ajira kwa vijana wengi wa kileo wa nchini China. Wakati takribani wahitimu wa vyuo milioni saba wanaingia katika soko la ajira, ajira mpya milioni tisa tu ndizo zilizoandaliwa, na wahitimu wa vyuo vya China ni lazima wagombee ajira pamoja na wanafunzi wanaorejea kutoka nchi za nje walikokwenda kusoma na pia wahitimu wa shule za upili na wale wa vyuo vya ufundi. Uwiano wa wahitimu wa vyuo na upatikanaji wa ajira ni kwa sasa unaaminika kuwa mdogo kabisa katika historia ya China. [zh].

Dhana ya uraia unaweza kuwa na maana zaidi ya kuwa na uhuru wa kufikiri na kuunda mawazo ambayo yanatofautiana na propaganda za serikali ya China. Zaidi sana, inawakilisha uwezo wa kuwa katika msawazo na kuwa huru pale unapokabiliana na mamlaka, uwezo unaotokan na hisia za kuwa sehemu ya mhamasishaji wa taifa, hat kama mtu ni modogo kwa kiasi gani. Kama kwa Ren Zhiqiang (@任志强), mfanyabiashara mkubwa wa mashamba aliye na wafuatiliaji kwenye Weibo wasiopungua milioni 14, alitoa maoni yake [zh],

总统的讲话从来不是必须学习的圣旨。而是一种常识。

Hotuba za Rais hazijawahi kuamrisha kuwa kila mtu anapaswa kusoma, bali kutumia akili binafsi.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.