Mgomo wa Nchi Nzima Wamshitua Rais wa Malawi

Rais wa Malawi ametupilia mbali mashinikizo ya kumtaka ajiuzulu mara baada ya mamia ya maelfu ya wafanyakazi wa umma wanaoshinikiza mishahara yao iongezwe, kuingia katika mgomo wa majuma mawili, kufunga uwanja wa ndege wa kimataifa nchini humo pamoja na kuzorotesha huduma za hospitalini na mashuleni.

Wafanyakati wa sekta ya umma waliomba ongezeko la mishahara kwa asilimia 65 ili kukabiliana na kupanda kwa gharama za maisha zilizotokana na hatua za kurekebisha hali ya uchumizilizochukuliwa na Rais Joyce Banda, ikiwa ni pamoja na kuishusha thamani ya kwacha (sarafu ya nchini Malawi). Wakati wa mgomo huo nchini kote, shule zilifungwa na vituo vyote vya afya vilibaki bila ya wafanyakazi kwani madaktari, wauguzi, waalimu na wafanyakazi wengine wa umma hawakuonekana makazini.

Mapema, Waziri wa Fedha alisema kuwa, matakwa ya wafanyakazi, ambayo yanakaribia mara tatu ya malipo ya mishahara inayotolewa na serikali kwa sasa kutoka kwacha bilioni 97[takribani dola za kimarekani milioni 275] hadi kwacha milioni 276 [takribani dola za kimarekani milioni785], hayawezekani. Lakini maafisa wa serikali walikubali kusikiliza madai ya wafanyakazi na kukubaliana ongezeko la mishahara la asilimia 61 tarehe 21 Februari, 2013.

Wakati huu mgumu haujamsaidia Banda ambaye anayejiandaa kuchaguliwa tena mwaka ujao. Akiwa ni mwanamke wa kwanza kuwa Rais nchini humu, aliyerithi uchumi uliokuwa taabani kutoka kwa mtangulizi wake, hayatiBingu wa Mutharika, amekuwa akisababisha hasira kwa wananchi wake kwa kutekeleza bajeti zinazosabisha ugumu wa maisha pamoja na hatua zake za mabadiliko ya kiuchumi yenye maumivu makali kwa wananchi zinazoonekana kutafuta kuiridhisha jamii za kimataifa, ambazo misaada yake ni takribani kiasi cha asilimia 40 ya bajeti ya Malawi.

Pigo jingine la serikali ya Banda lilikuwa ni kauli ya Waziri wa Malawi Mpango wa Maendeleo ya Kiuchumi Goodall Gondwe, iliyotolewa wakati mgomo huo ukiendelea akiwatuhumu viongozi wenzake kwa kuwa wavivu.

Joyce Banda  speaking at the DFID conference in 2010. Photo shared on Flickr by DFID under Creative Commons (CC BY-NC-ND 2.0) .

Joyce Banda akiongea katika kongamano la DFID la mwaka 2010. Picha iliweka na kwenye mtandao wa Flickr na DFID chini ya Creative Commons (CC BY-NC-ND 2.0) .

Mwanablogu, Alick Ponje aliandika kwamba, Banda alijishushia imani kwa watu wake:

Ukweli ni kwamba, tunaongozwa na Rais ambaye hatupi nafasi ya kutosha ya kujieleza. Lazima akisie kile tunachokihitaji na kukifanyia kazi pamoja na kuwa hatakuwa amejua uhalisia wake. Hiyo kwa hakika ni hatari sana. Tunahukumiwa na Rais wetu mwenyewe na sauti zetu zinazimwa kwa nguvu kubwa ambayo alijitwalia haraka.

Katika siku za mwanzo alipokuwa akionekana malaika, [Joyce Banda] alituhadaa tukaamini kuwa yeye ni Rais msikivu ambaye wakati wote angekuwa akitusikiliza kwa kile tunachohitaji. Alifanya hivyo mwanzoni ili kuwa na mwanzo mzuri na kwa kila uungwaji mkono aliostahili.

Lakini mwanablogu Pearson Nkhoma alihoji kuwa kumtaka Banda ajiuzulu au kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye hakutatatua tatizo kwa kuwa bunge bado litakuwa na idadi kubwa ya wabunge waliokuwa wakimuunga mkono Rais Mutharika na ambaye ndiye aliyeipelekea Malawi kuwa na hali mbaya ya uchumi inayoshuhudiwa hivi sasa:

Tunataka kujenga picha kuwa [Joyce Banda] ameshashindwa vibaya. Kwa hakika, atakuwa ameshashindwa, lakini ni sisi wenyewe tulioshangilia “mafanikio” ya Bingu wa Mutharika huku wengine wakilia usiku na mchana kwa maumivu wakisema kuwa, udikteta wa Bingu umeiangusha Malawi, na kwamba Bingu alishaiharibu Malawi kiasi kwamba ingekuwa ni vigumu kuiokoa tena. Sasa wakati [Banda] anapata wakati mgumu wa kuirudisha Malawi kutoka kwenye uharibifu uliokwishatokea. Sisi, tusioukubali uongozi wa Banda, kwa kiasi kikubwa, ndio tunaopaswa kujilaumu kwa hali hii tete.

Akizungumzia moja kwa moja mgawanyiko ulioko kati ya tabaka la watawala na wale wanaoongozwa, mwanablogu Alick Nyasulu aliandika makala iliyoonekana katika gazeti la The Nation kwamba serikali haitimizi mkataba iliyouweka kati yake na watu wa Malawi:

Moyo wa kufanya ujasiriamali upo na umezama vyema kwa mwananchi wa kawaida asiyelazimika kutumia vibaya upendeleo kwa kuwa msimamizi wa fedha za watoa kodi. Sidhani kama yeyote anastahili kuhubiri namna ya kufanikiwa kwa kigezo tu kuwa alishapata fursa ya kujigawia utajiri asiostahili kwa gharama ya imani ya umma kwake. Tusipochukua hatua za kuwazuia watu waliochaguliwa na wananchi na wasaidizi wao, hali ilivyo kwa sasa inatia wasiwasi sana, mazungumzo yote ya namna ya kupandisha hali za maisha ya watu hayatakuwa na maana yoyote na yatakuwa porojo za kikoloni. Sisi siyo watu wavivu, bali tunastahili kupata zaidi zaidi.

Mwanablogu Watipaso Mkandawire, anaandika kuwa, kila tabaka katika jamii ya watu wa Malawi, kuanzia wa ngazi ya juu hadi ya chini kabisa linashindwa kutimiza kabisa wajibu wake, akitoa wito kwa wafanyakazi wa umma kuongeza ufanisi katika kazi zao kwa kuwa tayari mishahara imeongezwa. Labda kwa kufanya hivi, serikali ya Banda itaheshimu ahadi zake kwa wananchi linapokuja suala la mpango wa kuimarisha uchumi, lakini pia, inaweza kuwa tofauti, aliandika:

Kwa kweli, uhalisia ni kuwa, hili ni jambo la wazi kabisa la kisaikolojia. Uchumi wa Malawi upo kwenye hali mbaya na kuwa kuna “vurugu zilizoandaliwa” miongoni mwa wale wanaojaribu kutekeleza Mpango wa Kuboresha Uchumi. wanamkataba na watu wa Malawi, lakini hawana mpango wa kuutekeleza mkataba huo kwa sababu eti hauwahusu na hata hawajali.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.