Kitabu-pepe Kipya cha GV: Sauti ya Kiafrika ya Matumaini na Mabadiliko

Hapa ni zawadi sahihi kabisa ya kuukaribisha mwaka mpya: kitabu-pepe kipya tulichokiandika kwa heshima yaEneo la Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. “Sauti ya Kiafrika ya Matumaini na Mabadiliko,”  kinakupa mtazamano wa kipekee kuhusu watu na habari za eneo hilo la Afrika kupitia posti zetu zilizo bora zilizoandikwa kwa lugha ya Kiingereza kwa mwaka 2012. Kutoka idadi ya takribani posti 800 zilizoandikwa kwa mwaka katika eneo hilo, tulichagua posti 13 zinazoangazia nchi kama Senegali, Uganda, Msumbiji, Guinea-Bissau, Ghana, Ethiopia, Nigeria, Mauritania, Kenya, Angola pamoja na nchi nyingine.

African Voices of Hope & ChangeUnakaribishwa kukipakua (download) hapa. Unaweza hata kutuma nakala yake (katika mfumo wa PDF, ePub au Mobipocket) kwa ndugu ay marafiki zako kokote walipo duniani, labda kama zawadi ya mchango wao kwa GV. Kilicho muhimu zaidi, tafadhali sambaza ujumbe kwa watu wako, kupitia mitandao ya kijamii na namna yoyote unayoona inafaa!

Sauti ya Kiafrika ya Matumaini na Mabadiliko ni ushahidi zaidi wanguvu ya kufanya kazi pamoja‘, jitihada za pamoja zinazojielekeza kwa watu na mahali ambapo mara nyingi “husahauliwa” na vyombo vikuu vya habari duniani kote, ingawa ni kweli Afrika ni kubwa lakini bado kuna matumaini ya maendeleo katika miaka ijayo. Kama ilivyosemwa katika utangulizi wa kitabu-pepe kicho, “Katika mwanzo wa mileniam mpya, ilionekana kama bara la Afrika lilikuwa limeachwa na jumuiya ya kimataifa….[lakini] takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kuwa uchumi wa nchi nane unaokua kwa kasi zaidi duniani uko katika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara.”
Na wakati wataalamu wengi wakiamini kuwa athari chanya za muda mrefu zinazotokana na teknolojia mpya zitakuwa kwenye sekta ya elimu, ‘pia lililo muhimu ni uwezo wa kuitumia teknolojia kwa faida katika maeneo kama uwazi wa jumla na uwajibikaji, kama inavyoonyeshwa na miradi inayojishughulisha na vyombo vya habari vya kijamii na kiraia kwa ajili ya kufuatilia chaguzi za mahali mahususi au kufanya takwimu za serikali kupatikana kwenye mtandao wa intaneti.”

Ikiwa imelengwa kupanua mukhtadha na kukuza malengo ya Global Voices, this mkusanyiko huu wa posti za mwaka 2012 utajaribu kuelezea muundo huo changamani na kufungua upeo kwa ajili ya mwaka ujao. Sauti hizi zinatuambia juu ya kusogea mbele kwa matumaini na mabadiliko, fikra za waandishi zinafunua njia iliyowezeshwa na jitihada na ushirikiano.

Shukrani kwa Mohamed Adel kwa msaada wa kitaalamu na wale ambao kwa namna moja ama nyingine walichangia kwenye makala zizizochaguliwa kwa ajili ya kitabu-pepe hiki kipya: Afef Abrougui, Ahmed Jedou, Anna Gueye, Eleanor Staniforth, Endalk, James Propa, Kofi Yeboah, Lova Rakotomalala, Nwachukwu Egbunike, Richard Wanjohi, Sara Gold, Sara Moreira, na Ndesanjo Macha.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.