Assad atumia Ndege ya Kivita Kuwaua Raia Wake

Posti hii ni sehemu ya habari zetu maalumu za Maandamano ya Syria 2011/12.

Serikali ya Syria imefanya shambulizi kubwa la angani dhidi ya raia wa nchi hiyo -waliokuwa wamesimama kwenye foleni waisubiri mikate kwenye kiwanda cha kuokea mikate huko Halfaya, Hama. Inakadiriwa kwamba watu waliouawa katika shambulio hilo mjini humo ni kati ya 90 na 300, waasi wakisema kuwa watu hao walikuwa wamejitenga na vikosi vya Assad. Mtandaoni, wanaharakati wanashangazwa inakuwaje dunia inaendelea kutazama tu maisha ya watu wasio na hatia wakiuawa kwa mamia.

Picha za kutisha za miili ya maiti hao, pamoja na video za baada ya shambulizi hilo, zinasambazwa mtandaoni, kuonyesha kushangazwa sana na mauaji hayo. [Mwandishi Erin Cunningham alitwi kuingo cha video hizo hapa.]

Leila Nachawati Rego anaandika:

@leila_na: Mbinu mpya ya utawala wa Syria ni kulipua viwanda vya kuokea mikate. Watu 200 wameuawa leo mjini Hama. Mauaji ya raia. Inasikitisha.#Syria

M-Syria Rafif Jouejati alitwiti kwa hasira:

@RafifJ: Tunasubiri viongozi wa dunia kusikia watamaliziaje sentensi hii “Tunalaani vikali sana…” #Halfaya_Massacre #Syria

na akaongeza:

@RafifJ: Hebu vitabu vya historia vionyeshe kwamba Assad aliendesha mauaji ya kimbari na dunia ikitazama, ikirudisha mikono nyuma, na ilifanya kidogo zaidi tu ya matumizi ya lugha kali. #Syria

Na Razan Ghazzawi mwenye ghadhabu kubwakupitia blogu yake:

Angalia kwa macho ya Halfaya martyrs na uthubutu kuwaambia umechoshwa na “Waislaamu wenye msimamo mkali” nchini Syria. Thubutu kuniambia, wewe mjinga, eti unahofia “kuvunjwa kwa haki za binadamu na vikosi vya Assad,” unahofia “mapigano ya wenyewe kwa wenyewe,” unahofia Qatar na vikosi hivyo, na kwamba hiyo ndiyo sababu hutaunga mkono mapinduzi yanayoongezwa na watu.

Kwa hiyo unahofia. Ninaona. Hiyo inasema vingi. Bila shaka.

Habari za hivi punde: dakika ile umetelekeza watu wa Syria, watu wa Syria walikutelekeza pia na unachohofia habibi: wewe na ustaarabu wako hamna nafasi katika wakati huu. Imeishia hapo, kuwa wewe na mimi si ndugu wa kibinadamu tena tena.

Pia, mpatanishi wa amani Lakhdar Brahimi aliwasili Syria leo kama sehemu ya mpango wake wa “kutafuta ufumbuzi” katika nchi.

Hassan Hassan anabainisha:


@hhassan140
: Mauaji ya Halfaya, kusherehekea kuwasili kwa Brahimi mjini damascus, aibu kwenu wote mnaoendelea kudhani Assad anaelewa chochote zaidi ya nguvu ya bunduki.

na anaongeza:


@hhassan140
: Historia: mnamo siku ya leo, Lakhdar Brahimi anatembelea Damascus kwa mazungumzo na Assad aliyeamua kusema kwa sauti kubwa huko Halfaya kwa kuwaua watu 300 waliokuwa wamejipanga kupata mkate.

Posti hii ni sehemu ya habari zetu maalumu za Maandamano ya Syria 2011/12.

1 maoni

  • All the best wishes for you guys. May Allaah help you in your surggtle for dignity and freedom.On a side note,the green band at the top of the Syrian flag should be light green,not deep green. The light green one is the standard type used by most opposition groups,including the Syrian National Council,Free Syrian Army and most demonstrators inside and outside Syria.So was the pre-Baath flag. I think this deep green version you have got from Wikipedia,and this is erroneous. Plz see to this.Was salam

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.