Jamhuri ya Dominika: Mwanafunzi Auawa kwenye Maandamano

Makala haya yamechapishwa kwa kuchelewa kutokana na sababu za kiufundi.

Pendekezo la kubana matumizi lililowasilishwa kwa Bunge, ambalo lilikumbana na upinzani mkali kutoka katika vyama vya kiraia, sekta ya biashara na vyama vya wafanyakazi, harakati mbalimbali za kupinga kwa nguvu muswada huo zimepangwa. Maandamano yamekuwa yakitokea tangu Oktoba 4 2012, wakati rasimu ya muswada ilitangazwa hadharani. Hata hivyo, tangu Jumanne Novemba 6 2012, wananchi wamekuwa wakiandamana na siku kwa siku maandamano hayo yanashika kasi huku idadi ya waandamanaji ikiongezeka.

Mnamo Alhamisi, Novemba 8 2012, Chuo Kikuu cha Autonomous Santo Domingo, chuo pekee cha umma kikuu nchini, kiligeuka kuwa eneo mojawapo la maandamano haya ya kuipinga serikali. Lakini ilivyo kawaida -na licha ya kuwepo kwa sheria mbalimbali zinazozuia -wanafunzi hao walikuwa wanakabiliwa na kikosi cha polisi wenye silaha, na kusababisha kifo cha William Florian Ramirez mwenye umri wa miaka 21[es], mwanafunzi wa mwaka wa tatu  wa udaktari, aliyepigwa risasi kifuani.

El estudiante asesinado, Willy Florian, siendo llevado por encapuchados fuera de la zona de disturbios.

Mwanafunzi aliyeuawa, Willy Florián, alipokuwa anaondolewa kwenye vurugu hizo zilizoendeshwa na watu wenye skafu. Picha hii imesambazwa sana kwenye mtandao.

Haikuchukua muda mrefu sakata hilo lilihamia kwenye mitandao ya kijamii pamoja na kwenye redio bubu (zisizosajiliwa). Kiongozi wa Kisiasa Elizabeth Mateo, maarufu kama kiongozi wa kupigania asilimia 4 ya Pato la Taifa itumike kwa elimu, aliandika yafuatayo kwenye mtandao wa twita:

@ElizabethMateo: Condeno la muerte del estudiante de la UASD. Exijo justicia.

@ElizabethMateo:  Nalaani vikali mauaji ya mwanafunzi wa UASD. Nadai haki ifanyike.

Hali kadhalika, mpelelezi, mtaalamu-mshauri na mwandishi wa makala, Olaya Dotel, alisema:

Young man calls for civil mobilization.

Kijana akitoa wito wa kuhamasishaji umma. Imechukuliwa kutoka ukurasa wa kituo cha Bono na kuchapishwa kwa ruhusa.

@OlayaDotel: Los corruptos que hoy controlan el Estado no valen una gota de sangre de nuestros jóvenes… Ni uno más!!!

@OlayaDotel: Hawa watu wala rushwa wanaotamba wapendavyo serikalini hawana haki yoyote kumwaga tone la damu ya vijana wetu … si moja zaidi!!!

Mtanziko huu umeenea mno kiasi kwamba René, muimbaji maarufu katika kundi la Puerto Rican Calle 13,  alitoa maoni juu ya tukio hilo:

@Calle13Oficial: El mundo está mirando a República Dominicana esperando que se haga justicia por el asesinato del joven estudiante de medicina Willy Warden!

@Calle13Oficial: Macho ya dunia yote yanaitazama Jamhuri ya Dominika, kwa matarajio kwamba haki itafanyika kwa kifo cha kijana aliyekuwa mwanafunzi wa udaktari Willy Warden!

Matukio yote haya yamefanyika wakati ambao imebainika kwamba, wakati nchi hiyo ikipitia kipindi kizito cha mtikisiko wa kiuchumi pamoja na kukumbwa na matatizo ya kijamii, Waziri wa Elimu, Josefina Pimentel, aliongeza mshahara wake mwenyewe kwa asilimia 62 [es], kutoka RD $ 185,000.00 na kufikia RD $ 300,000.00 kwa mwezi, sawa na dola $ 7,500.

Young people hold up signs outside the National Congress, in protest against the Fiscal Reform.

Vijana washikilia mabango nje ya Bunge, kupinga sera ya kubana matumizi ya serikali. Imechukuliwa kwa ruhusa kutoka ukurasa wa kituo cha Bono na kuchapishwa kwa ruhusa yao.

Mchanganyiko wa haya na masuala mengine, mbali na kuwakatisha tamaa waandamanaji, yamewachochea kuwa na moyo wa kutaka mapinduzi. Kundi la watu karibu 100, likijumuisha watu maarufu na vyombo vya habari, walikusanyika mbele ya majengo ya taasisi ya Mfuko wa Kimataifa wa Demokrasia na Maendeleo [es] (FUNGLODE), taasisi iliyoanzishwa na rais wa zamani Leonel Fernández Reyna, ambaye anatuhumiwa kuifilisi nchi hiyo katika miaka yake nane ya kuwa madarakani (angalia video hapa) [es].

Waandamanaji waliweka mishumaa mitaani na kuimba kwa sauti ya juu sana nyimbo mbalimbali za kulaani vitendo hivyo. Mtandao wa twita ndio uliokuwa chombo cha habari kilichotoa habari za tukio hilo, na watumiaji wa twita walijiweka pamoja kwa kutumia ya alama habari ya #FrenteaFunglode. Mtangazaji Maribel Hernández aliandika haya kwenye akaunti yake ya twita:

@MaribelNexos: Policía Nacional una banda criminal, vocifera la masa #FrenteaFunglode.

@MaribelNexos: Polisi wa taifa, genge la wavunja sheria, jamani pigeni kelele kupinga hili #FrenteaFunglode

@MaribelNexos: La masa grita La Fundación Global verguenza nacional.  #FrenteaFunglode #FrenteaFunglode

@MaribelNexos: Umati wa watu ulipiga mayowe kupinga hii taasisi ya Global Foundation, wakiita aibu ya taifa #FrenteaFunglode

Lakini mambo hayakuishia hapo. Mashirika ya kiraia  na watu binafsi walimiminika katika mtandao wa intaneti kuonyesha ubunifu mkubwa, kupitia matangazo na picha nyingi zinazopinga chama kinachounda serikali pamoja na utawala wa sasa, kama hizi zilizowekwa hapa chini. Katika maduhui hayo hayo, uhamasishaji wa aina mbalimbali katika ngazi zote ulikuwa umepangwa kufanyika Ijumaa, Novemba 9 2012, na kuendelea kwa siku zilizofuata. Ninawaacha na baadhi ya kauli zenye kutoa wito wa maandamano na mifano ya michoro iliyojikita katika matukio.

 http://youtu.be/S6IskZCANfI

 

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.