Costa Rica Yakumbwa na Tetemeko la Ardhi wa Ukubwa wa 7.6

Wananchi wa Costa Rica wametoa maoni kwenye mtandao wa Twita kuhusu tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.6 (Mercalli) lililoikumba nchi hiyo tarehe 5, mwezi wa Septemba, 2012, saa 8:42 za mchana. Mshindo wa tetemeko hilo lililoathiri zaidi sehemu ya Guanacaste, ulifika mpaka kwenye miji ya jirani ya Liberia na San Jose.

Watumiaji wa mtandao wa Twita nao wanaripoti kwamba tetemeko hilo la ardhi lilidumu kwa muda mrefu kiasi. Raia watumiao mtandao wanatumia alama habari za #temblorcr na #terremotocr kujadili tukio hilo.

Kama Ariel Arburola (@arielarburola) [es] alivyotangaza kwenye Twita:

@arielarburola: Casi corro pero me dió tiempo de poner #temblorcr

@arielarburola: Karibu nikimbie, lakini bado nilipata fursa ya kuandika #temblorcr

Taarifa kuhusu madhara ya tetemeko zinaingia, hata kupitia Twita. Sergio Pacheco (@lafoto) [es] aliandika mistari kadhaa kuhusu uharibifu wa nyumba ya dadake mjini Montezuma, karibu na kitovu cha tetemeko hilo:

@lafoto: la casa de mi hermana en Montezuma en Guanacaste con el piso levantado #temblorcr

@lafoto: Sakafu katika nyumba ya dadangu huko Montezuma Guanacaste imeinuliwa #temblorcr

Baadhi ya mitandao ya simu za mikononi zimezimwa, Cristian Cambronero (@cambronero) [es] anavyoripoti::

@cambronero: Caída la red de Movistar, el ICE funciona parcialmente #terremotocr

@cambronero: Mtandao wa Movistar umezimwa, TUK [Taasisi ya Umeme ya Kosta Rika] inafanya kazi nusu nusu #terremotocr

Fabián Calvo (@FabianCalvo) [es] akajibu:

@FabianCalvo@cambronero Acá por el contrario, yo tengo Movistar y puedo llamar a Claro y a líneas fijas del ICE, a los celulares Kolbi no puedo del todo

@FabianCalvo@cambronero Huku, ni mengine, nina Movistar na ninaweza kuwasiliana na simu za Claro na simu za mezani za TUK, siwezi kuwasiliana na simu za Kolbi katu

OVSICORI (Taasisi ya Kosta Rika ya Kuchunguza Volkeno na Mitetemeko ya Ardhi) imeripoti kwamba mwambao wa Rasi ya Nikoya inaweza kuinuka kwa urefu wa mita moja kwa ajili ya mtetemko wa ardhi, El Periódico ya Kosta Rika (@elperiodicocr.com) [es] inaripoti:

@elperiodicocr.com: Terromoto levantó la Penínzula [sic] de Nicoya en por lo menos un metros, dice Marino Protti, del OVSICORI.

@elperiodicocr.com:Mtetemeko wa ardhi uliinua Rasi ya Nikoya kwa urefu wa mita moja au zaidi, Marino Protti wa OVSICORI akasema.

Signali hai za idhaa zinasikika kwenye ADNfm radio [es], ambapo watu wanapiga simu kuripoti ukatizaji wa huduma za umeme, kuanguka kwa paa za vigae, na uharibifu, ingawa vifo bado havijaripotiwa.

Tahadhari ya moja kwa moja ya tsunami imetolewa kwenye sehemu ya Pasifiki na Chile pia, lakini Tume ya Kitaifa ya Mambo ya Dharura (CNE) imeibatilisha kwenye ufuko wa Pasifiki wa Costa Rica.

Kupitia Twita na vyombo vya habari, kama vile idhaa ya ADN.fm, raia watumiao mtandao wanawasihi wenye habari kutumia mitandao ya jamii kama Twita kuhabarishana.

Rais wa nchi, Laura Chinchilla (@Laura_Ch) [es] aliondoka ili aende kutafuta habari kutoka kwa Tume ya Kitaifa ya Mambo ya Dharura:

@Laura_Ch: Ante dificultades en el sistema de telecomunicaciones me dirijo a CNE para recibir informe sobre seismo q sacudió al país.

@Laura_Ch: Kwa sababu ya matatizo kwenye mfumo wa mawasiliano ya mbali ninaelekea kwa CNE ili nipate taarifa kuhusu mtetemeko wa ardhi ulioathiri nchi.
Hospital Monseñor Sanabria in Punta Arenas, Costa Rica, after September 5th earthquake. Image by Twitpic user @tapachiche

Hospitali ya Monseñor Sanabria, mjini Punta Arenas, Costa Rica, baada ya tetemeko hilo la ardhi lililotokea tarehe 5, mwezi wa Septemba. Picha imechukuliwa na mtumizi wa Twitpic @tapachiche

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.