Paralympiki 2012: Mwanzo mzuri, Habari za Kukumbukwa

Makala hii ni sehemu ya makala zetu maalum kuhusiana na michezo ya Olympiki ya London, 2012 .
[viungo vyote vipo katika lugha ya Kifaransa, labda kama italekezwa tofauti]
Kuanzia tarehe 29, Augusti hadi Septemba 12, 2012, wanamichezo 4,200 kutoka nchi 166 watashiriki katika michezo ya 14 ya Paralympiki jijini London itakayohusisha nyanja ishirini za kimichezo.
Video ikionesha michezo mbalimbali kama ilivyowekwa na Televisheni ya michezo ya Paralympiki [en]:

Waandaaji walihitaji siku 15 ili kuandaa viwanja kwa ajili ya Paralympiki mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya London Olympiki, 2012.
Charles El Melieani katika jarida la JOL anaandika kuwa idadi kubwa ya tiketi iliyovunja rekodi zimenunuliwa kwa ajili ya mashindano haya.:

Londres a fait des efforts colossaux en matière de billetterie, mettant sans cesse en avant les Jeux paralympiques dans tous ses points de vente. Avec un résultat impressionnant : au total, ce sont déjà près de 2,3 millions de tickets qui ont trouvé preneur. Sur 2,5 millions mis en vente. En bref, ces Jeux pourraient bien se dérouler à guichets fermés : exceptionnel.

London imeweka juhudi ya kipekee kabisa katika njanja za utoaji wa tiketi na kuyatangaza mashindano haya, kurusha matangazo ya Paralympiki katika maeneo yote ya kuuzia bidhaa. Matokeo ya juhudi hizi yanatia moyo sana: kwa jumla, kati ya tiketi milioni 2.5 ambazo toka wali ndizo zilizokusudiwa, karibu tiketi milioni 2.3 tayari zimeshauzwa. Kwa mashindano haya, inastahili kwa tiketi zote kuuzwa: inashangaza kwa kweli.
The Burkina Faso delegation during the opening ceremony of the Paralympic Games

Wawakilishi wa Bukinafaso wakati wa sherehe ya ufunguzi wa michezo ya Paralympiki. Ni baadhi ya picha zilizopigwa kutoka kwenye video ya sherehe hizo iliyotolewa na Televisheni ya mashindano ya Paralympiki.

Washiriki wa michezo hii, siyo wote waliozaliwa wakiwa vilema. Jacqueline Mallet katika blogu ya ‘Province de l'équateur’ anaelezwa na kufafanua baadhi ya hadithi za kusisimua na sisizosahaulika katika makala hii ‘” Nilichukuliwa kama mfu: hatma isiyoelezeka ya wanamichezo walemavu”:‘:

Certains de ces sportifs ont grandi avec leur handicap, tandis que d’autres ont dû apprendre à le surmonter à la suite d’une guerre ou d’un accident. Frappés par le destin, ils ont trouvé dans le sport un moyen de se reconstruire.

Baadhi ya wanamichezo hawa wamezaliwa na ulemavu, huku wengine wakilazimika kujifunza namna ya kuzipokea hali hizi ikiwa ni matokeo ya majeraha wakati wa vita au ajali. Wakikubaliana na hali halisi, waliona kuwa kujihusishe na michezo kama njia pekee ya kuwajenga tena.

Pia, Mallet anaandika kuhusu safari ya wanamichezo kadhaa: Martine Wright, mhanga wa milipuko ya mabomu ya London; Vita ilimuengua mwanamichezo wa Afghanistani katika safari yake ya michezo ya London….’ Ilielezea habari ya Malek Mohammad, mwanamichezo wa Ki-Afghanistani aliyepoteza miguu yake miwili mwaka 2005 alipokuwa anatembea katika mgodi wa madini ulio karibu na nyumbani kwake mjini Kabul.

Afghan swimmer Malek Mohamed at home before the Paralympic Games.

Muogeleaji wa Afghanistani, Melek Mohammad akiwa nyumbani muda mfupi kabla ya michezo ya Paralympiki. Picha hii ilipigwa kutoka kwenye video ya Malek Mohamed iliyotolewa na AFP mtandao wa Youtube

Katika makala ya blogu ‘‘kutoka mhanga wa vita, na sasa shujaa wa Paralympiki’ ‘ [en], Damon van der Linde in Freetown, Sierra Leone, anatuambia kuhusu simulizi ya Mohamed Kamara, aliyekamatwa na waasi akiwa na umri wa miaka minne tu wakati wa vita vya kiraia . Katika harakati za kumshikilia kama mateka, walifikia hatua ya kumkata mkono wake mmoja.
Katika mtandao wa Kifaransa unaotoa taarifa kuhusu walemavu , Stéphane Lagoutière anaandika kuwa:

L'autre grande star de ces jeux seront bien sur les déficients mentaux, avec un retour après 12 ans d'absence.

Kwa hakika, matukio mengine makubwa yaliyo na changamoto kubwa kifikra katika michezo hii itakuwa ni kurejea kwa wanamichezo walioshiriki michezo hii ya Paralympiki takribani miaka 12 iliyopita.

Nchini Ufaransa, kituo cha Televisheni cha Mkoa ndicho kituo pekee kitakachoonesha kitakachoonesha matukio yote ya michezo ya Paralympiki..

Katika mtandao wa Twita, mtumiaji @ThePositive1 posted picha ya timu ya Jamaika..

Makala hii ni sehemu ya makala zetu maalum kuhusiana na michezo ya Olympiki ya London, 2012 .

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.