Kocha Mfaransa Ateuliwa Kuongeza Bahati ya Kenya Kwenye Kandanda

Mnamo, tarehe 29, mwezi wa Agosti mwaka 2012, mwenyekiti wa Shirikisho la kandanda(Football Kenya Federation-FKF), bwana Sam Nyamweya alitangaza kuwa mchezaji na kocha wa zamani Mfaransa Henri Michel ameteuliwa kocha wa timu ya taifa. Uteuzi wake umefuatia mfululizo wa matokea mabaya na baada ya timu ya Kenya kukosa nafasi ya kushiriki mashindano ya Kombe la Mataifa ya Africa (ACN) mara mbili mfululizo na pia kushindwa kufika kwenye fainali za mashindano ya kandanda na katika ukanda wa Afrika Mshariki na Kati.

Wanablogu walikuwa na maoni yao kuhusu uteuzi huu wa Henri Michel. Chenga Funga anasema haya katika posti yake ‘Kanuni za yanayofahamika’:

Mtanziko wa njia tatu. Ndicho kimeifanya FKF kumchagua Henri Michel. Kwa maneno rahisi, je ungependa yule anayejulikana sawia, yule anayejulikana lakini hajulikani au yule asiyejulikana kabisa? Kufuatia bahati mbaya ya Harambee Stars kwa mchezo huu mzuri, washika dau wamekuwa wakiwasilisha majina ya makocha kutoka nchi mbalimbali kwa nafasi ya ukocha wa timu hiyo ya taifa. Mtanziko kweli! Kwa siku zilizopita wengine kama, Francis Kimanzi, Ghost Mulee, Antonio Hey na Zico wamepatiwa nafasi hiyo lakini matokeo yao hayajapendeza. Hivyo basi Sam Nyamweya na FKF waliona wabahatishe kati ya wale wanaojulikana lakini hawajulikani kama Raymond Domenech, Claude Leroy, Oto Pfister, Adel Amrouche na mfaransa Michel. Wengi kati yao wamekuwa na mafanikio yanayoonekana katika uongozi wa timu zao na hivyo basi ikaonekana kuwa jukumu hili wataliweza. Pia, zingatia kuwa timu yetu ni kadi isiyoeleweka. Na imekuwa hivyo kwa muda sasa. Kwa namna ndogo sana, NDOGO SANA, mazingira yetu hayana tofauti na timu ya Uingereza, inayoongozwa na Roy Hodgson; Kuna uwezakano mkubwa wa ushindi lakini ushindi wenyewe haupatikani. Lazima, tuwe na shukrani kwa makocha ambao tumekuwa nao kwa timu yetu ya taifa, lakini lazima maisha yaendelee na usukani ni wa Henri Michel.

Blogu ya MutuaMaundu pia imeongeza maoni yake kuhusu Michel:

Nchi yote imekuwa na fadhaa kuhusu swala hili. Kwa wengi, Henri Michel ndiye yule mkombozi wa mchezo wa kandanda nchini Kenya, ambao umeonekana kudodora zaidi. Mfaransa huyu, anaweza kuwa amefaulu kwa mengi, lakini kama nchi tumeumia sana kwa sababu ya uchezaji mbaya wa timu ya taifa. Hivyo basi, tunapaswa kupunguza matarajio yetu – tusitarajie mengi sana.

Mfaranza Henri Michel, ambaye anatumia mbinu za kuheshimika, amefurahia ushindi mkubwa katika kilele cha mchezo huu. Kama mchezaji na kocha aliongoza Les Bleus, timu ya taifa ya Ufaransa hadi ikawa nambari tatu huko Mexico mwaka wa 1986. Hapo baadaye akakuwa  maarufu Morocco, alipowaongoza Atlas Lions hadi Kombe la Dunia lililotwaliwa na Ufaransa mwaka wa 1998. Pia aliwaongoza Carthage Eagles wa Tunisia hadi wakafikia Kombe la Dunia nchini Japan mwaka wa 2002. Alikuwa kocha wa Ivory Coast wakati wa Kombe la Dunia la mwaka wa 2006 nchini Ujerumani.
Hata hivyo, tusisahau kuwa utawala wa tasnia ya kandanda umekuwa mbaya, kukiwa na ufisadi mwingi, na kwa sababu ya mambo kama haya haifai kabisa kutarajia mengi kutoka kwa kocha huyu mpya. Hakuna miongozo mizuri ya kukuza talanta kwa kujitayarisha kwa utumishi kwa nchi.
Ligi Kuu ya Kenya, ililazimika kujitenga na kuunda chombo chake huru mwaka wa 2003. Jambo hili lilitokea baada ya FKF ilipokaribia kabisa kuutupilia mbali huu mchezo. Ingawaje kuna viongozi wapya FKF, matumaini ya Kenya ni madogo. Michezo ya nguvu, imeondoa imani yetu kwa wanakandanda wetu. Ni marehemu Reinhardt Fabisch tu ndiye aliyefanya vizuri katika timu hiyo ya taifa akiwa na Mjerumani Benrard Zgoll katika miaka ya themanini. Ukiacha hao wawili, wageni wengine Bernard Lama wa Ufaransa na Mjerumani Antoine Hey hawakudumu, na walipata misukosuko mingi. Na baadae wakalazimika kuondoka. Haya yote yalichangiwa sana na ahadi zisizotekelezeka za viongozi wa kandanda.
Visa hivi vilipaswa kuwa vimetufunza kutokuwa na matumaini makubwa kuhusu uteuzi wa Michel. Tunapaswa kulitazama hili kwa makini na kumpa Michel msaada wowote atakaouhitaji ili aweze kupata matokeo mema. Lakini pia yatunafaa kujiuliza kama kuna malengo ya muda mrefu ya kurudisha kandanda ya Kenya mahali pake. Uteuzi na mafanikio ya Michel yatakuwa tu kwa muda mfupi, hivyo basi yatupasa kuangalia mbele. Kwa Wakenya wanaopenda kandanda, msiwe na matarajio makubwa mno ili msijekupatwa na machungu ikiwa Henri hatabadilisha mambo kutoka katika hali tuliyonayo.
Alltimenews walikuwa wametabiri uteuzi wa Henri na pia kuongeza mfululizo wa mafaniko yake na kuangazia sehemu nyingine alikowahi kuwa kocha.

Kwa ufupi:

  • Mzinduzi mbinu wa zamani wa Ufaransa, atafahamika Jumanne, anaonekana kuwa ataongoza timu ya Kenya kuelekea kwenye mafanikio.
  • Michael mwenye miaka 64 alifuzu kuwashinda makocha wengine kutoka nchi mbalimbali kama Raymond Domenech na Tom Saintfiet.
  • Mfaransa huyu anajua mizengwe ya kandanda la Afrika kwa kuwa amekuwa hapa Afrika kwa zaidi ya miongo miwili tangu alipokuwa kocha wa Kameruni mwaka 1994.
Kocha wa zamani wa Ufaransa, Henri Michael atatangazwa wiki ijayo kama kocha wa Harambee Stars. Mwenyekiti wa FKF, Sam Nyamweya alilithibitishia gazeti la Nation kuwa Michel amekubali uteuzi wake na atatambulishwa na waziri mkuu Raila Odinga. Michel ambaye alikuwa nchini mwezi uliopita kwa mazugumzo, aliwashinda zaidi ya makocha 60 wa kigeni waliokuwa wameomba nafasi hiyo  iliyoachwa wazi baada ya Francis Kimanzi kuchaguliwa kuwa mkurugenzi wa ufundi kwenye shirikisho la kandanda nchini Kenye, FKF.
Uteuzi huu utagusa hisia za watu wengi. Kazi sasa ni kwa Michel. Matokeo mabaya ya Harambee Stars hasa kwa miaka minne ya hapa baadaye ni jambo ambalo mashabiki wengi wangependa kulisahau. Kwa kuwa mechi za kufuzu kushiriki Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2013  na Kombe la Dunia mwaka 2014 zinakaribia, mamlaka za kandanda Kenya wanangoja kuona tofauti gani ya maana ambayo Michel anaweza kuileta.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.