Tanzania, Ethiopia: Meles Zenawi ‘Atuma Twiti’ Kutoka Kilindi cha Kaburi

Taarifa rasmi iliyotoka Jumatatu ya Wiki iliyopita kuhusu kifo cha Waziri Mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi, ziliibua mishtuko miongoni mwa watumiaji wa zana za habari za kiraia nchini Tanzania, hasa baada ya twiti kuanza kutumwa kutokea anuani ya Twita iliyoaminika kuwa rasmi ya Zenawi mwenyewe.

Mjadala ulianza pale Zitto Zuberi Kabwe, ambaye ni Mbunge nchini Tanzania, alipotwiti ujumbe huu:

@zittokabwe: Natuma salamu zangu za rambirambi kwa wananchi wa #Ethiopiakufuatia kifo cha Waziri Mkuu #MelesZenawi.Ni matumaini yangu kwamba kutakuwa na muendelezo wa kidemokrasi huko Abbysinia.

Susan Mashibe alijibu:

@iMashibe: @zittokabwe Je, ni kweli kwamba jambo hili limetokea kwelikweli safari hii? Cc @SwahiliStreet

And Swahili Street alihitimisha:

@iMashibe Imetangazwa kupitia ETV. Ni taarifa rasmi @zittokabwe

Chambi Chachage alitwiti makala ya blogu yenye kichwa cha habari ‘Salamu za Meles Zenawi za Kuwaaga Viongozi Vijana wa Afrika‘ kutoka Kamisheni ya Uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa (UNECA) tarehe 16 Novemba 2006, ambayo pia ilitumwa kama twiti na watumiaji wengine.

Na kisha ghafla @PMMelesZenawi aliingilia kati, ikiwa ni bayana kabisa kwamba ‘alituma jumbe za twiti baada ya kifo chake’ akimlenga Mbunge wa Tanzania Zitto Kabwe:

@PMMelesZenawi: @zittokabwe Uwe kiongozi bora kuliko nilivyokuwa mimi. Huku juu hakuna utani, ninajiandaa kulipa kwa ajili ya makosa yangu http://www.ethiopianreview.net/index/?p=42267

Meles Zenawi ‏@PMMelesZenawi – akitwiti baada ya kifo chake. Chanzo Twitter Screen Shot

Twiti hii kwa Zitto Kabwe, ambaye ana zaidi ya wafuasi 29,000, ilisambabisha mizozo, ikifanya watu waanze kudadidi ikiwa anwani ya ‏@PMMelesZenawi ilikuwa imeibwa na wapinzani wake?

@zittokabwe: @hmgeleka anwani hii haionekani kuwa ya kweli hasa kwa sababu ya ujumbe huu @pmmeleszenawi

Zitto Zuberi Kabwe naye alihitimisha, na kisha aliendelea kusema:

@zittokabwe: @AnnieTANZANIA alitwiti kwa @PMMelesZenawi si akaunti halali. Zipuuzeni jumbe zinazotumwa nayo. Akaunti imeibwa na wapinzani wake

Omar Ilyas naye aliiunga mkono:

@omarilyas: Akaunti hii daima imekuwa si iliyo ya kweli toka mwanzo @PMMelesZenawi – ni aina ya watu wenye majivuno kupita kiasi kama yule jamaa anayeitwa @Julius_S_Malema @zittokabwe

Hata hivyo, mjadala kuhusu yale atakayokumbukwa nayo Meles Zenawi unaendelea kuunguruma kutoka wale wanaomhusudu Meles kwa uwezo wake ‘kufikia malengo katika kazi yake’ hadi kwenye uvumi kwamba Meles hakuwa mwanademokrasia:

@Htunga: @zittokabwe Hivi, huyu Meles ni nani hasa? Ninawaona Waethiopia wakikabiliwa na njaa na kufa kwenye malori … Nakumbuka pia kuuwawa kwa watu kwa kupigwa risasi mwaka 2010.

@zittokabwe: @Htunga Je, Watanzania hawakuwa wakikabili njaa na kufa wakati wa Nyerere? Lakini tunamkumbuka na kumhusudu kwa sababu alikuwa mtu wa kanuni. Ni hivyo hivyo hata kwa Meles’

@zittokabwe: @PMMelesZenawi Pamoja na makosa yake, #MelesZenawi anabaki kuwa mfano bora kwangu wa kuigwa. Mnao uhuru wa kumrejesha #TheDerg au Isaias

Anwani ile bandia ya Twita (inayohisiwa kuwa iliibwa) @PMMelesZenawi iliyosababisha kuibuka kwa mjadala huo hapo juu, vilevile inaibua swali kwamba kwa nini viongozi wengi wa umma na wanasiasa barani Afrika hawataki kuthibitisha anwani zao za Twita.

Kwa taarifa zilizopo, mara nyingi Twita huchukua muda mrefu sana, au pengine haijishughulishi kabisa kujibu maombi ya kuthibitisha anwani fulani fulani.

Twita ni maarufu sana nchini Tanzania kama chombo cha kubadilishana maoni na kuendesha mjadala na pia jukwaa la kutoa habari za papo kwa papo, au hivi punde. Twita, hata hivyo, inaweza kutumiwa vibaya kama ilivyokuwa kwa hii ya @PMMelesZenawi na pia inaweza kuleta vurugu na hisia mbaya kuhusu usahihi na kuaminika kwa chanzo cha taarifa fulanin.

Anwani nyingine za Twita zilizo bandia, zilizoibwa au korofi za Waafrika kwa sasa ni: @Hailemdesalegne, @Julius_S_Malema, @kabwezitto, @alfredmutua na @MwaiKibaki

Meles Zenawi alikuwa Rais wa Ethiopia kutoka mwaka 1991 hadi 1995 na baadaye alikuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo kutoka mwaka 1995 baada ya kufanyika Uchaguzi Mkuu mwaka ule. Waziri Mkuu katika nchi hiyo ndiyo nafasi yenye nguvu kabisa katika uendeshaji wa masuala yote muhimu.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.