Ethiopia: Maandamano ya Waislamu Yashika Kasi

Ishara za uanaharakati wa waislamu wa ki-Ethiopia kupinga serikali kuwangilia katika mambo yao ya kidini, zilionekana wazi pale walipopeleka kampeni zao mtandaoni mwezi Mei. Kadiri harakati hizo zikiendelea kukua na kusambaa nje ya mtandao wa intaneti, Jeshi la Polisi la nchi hiyo limeanza kutumia nguvu kupambana na waandamanaji.

Wanawake waislamu Ethiopia. Picha kwa hisani ya: Boyznberry Flickr page (CC BY-NC 2.0)

Kwa mujibu wa ukurasa wa mtandao wa Facebook wa wanaharakati hao uitwao Dimtsachin Yisema (Iacheni Sauti Yetu Isikike), Jeshi la Polisi lilitumia nguvu pamoja na kufanya vitendo haramu katika sehemu zinazochukuliwa kuwa takatifu misikitini katika jitihada za kupambana na waandamanaji hao. Mwanaharakati wa ki-Islamu wa ki-Ethiopia na mwandishi Merim Bint Islam aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook kwa dondoo ifuatayo:

 
Hivi ndivyo vichapo vya kikatili  walivyofanyiwa ndugu zetu, hapo jana huko Awuliya.
Habari Mpya Addis Habari @ AddisFocus # Vikosi vya Ulinzi vya Utawala wa Ethiopia bila haya waliteka zaidi ya mifugo mia moja (ng'ombe maksai) kwenye msikiti mjini Addis iliyokuwa tayari kwa sadaka

Video ya mtandao wa YouTube hapa chini inaonyesha waandamanaji wa ki-Islamu mwezi Aprili 2012:

Ingawa vitendo hivyo vya polisi viliripotiwa kuwa vya kikatili, wanaharakati katika ukurasa wa Facebook mara moja walitoa rai kwa wa-Islamu wenzao wawe na utulivu.  Ukurasa wa Facebook wa wa-Islamu wa Ethiopia ulionyesha alichokiona Ahmedin Jebel[amh]:

ሕዝበ ሙስሊም ሆይ! ሰላማዊና ሕገ መንግሥታዊ መብት የማስከበር እንቅስቃሴያችን ከተጀመረበት ጊዜያት ጀምሮ ላለፉት ስድስት ወራት በሚቻለን ሁሉ ሁከት እንዳይነሳ ጥረናል፡፡ ምክንያቱም ሁከት መነሳቱ መቼም ቢሆን ለኛ አይጠቅመንምና፡፡ የተለያዩ አካላት ሁከት ዉስጥ አስገብተውን ሂደታችንን ለማደናቀፍ የሚቻላቸውን ሁሉ ሞክረዋል፡፡ እየሞከሩም ነው፡፡ መንግሥትም ይሁን የትኛውም ወገን ቢተናኮሰን፣ ቢተኩስ፣ ቢያስር፣ መስጂዶች ቢደፈሩም ምላሻችን የችኮላና ህጋዊ ካልሆነ፣ ይበልጥ አላማቸውን የሚያሳካና ሕዝበ ሙስሊሙን ለአደጋ የሚያጋልጥ ከሆነ ለኛ ዉድቀት እንጂ ድል አይደለም፡፡

Kwa wa-Islamu wote ki-Ethiopia, tangu tulipoanza harakati zetu miezi sita iliyopita tumeweza kujitenga na mandamano yenye malengo mabaya kwa kufahamu kuwa vitendo kama hivi vingeharibu kile tunachokipigania. Vikundi tofauti vimekuwa vikijaribu kutufanya tuchukue hatua za kufanya ghasia kwa sababu ya matendo yao yanayokera. Wamefikia hata kufanya vitendo haramu kwenye sehemu takatifu kidini lakini tusimame imara kwa sababu kukizijibu hila hizo wanazotufanyia tutashindwa.

Wakati huo huo, Abiye Teklemariam aliandika kwenye mtandao wa Facebook:

Wanaharakati wanadai watu wa serikali wanaweza kwa makusudi kutengeneza maandamano feki  karibu na makao makuu ya Umoja wa Afrika ili kuwasingizia waislamu kuyaandaa.

Hali ya kisiasa na kidini huko Ethiopia inaonekana kutokuaminika huku tetesi kuhusu wapi alioko na afya ya Waziri Mkuu Meles Zenawi zikisambaa na maandamano ya waislamu yakiendelea kushika kasi.

Uislamu ndio dini ya pili kuwa na waumini wengi nchini Ethiopia nyuma ya Ukristo.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.