Congo (DRC): Video zasaidia kumtia hatiani Thomas Lubanga kwa uhalifu wa kivita

Makala hii inatokana na maudhui yaliyochapishwa kwanza kupitia kampeni ya kukusanya ushahidi wa picha za video inayoitwa WITNESS.

Mnamo tarehe 14 Machi, 2012, Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ilimtia hatiani Thomas Lubanga, kiongozi wa zamani wa waasi huko Kongo Mashariki, kwa kuwatumia watoto katika mgogoro wa kivita – jambo linaloangukia miongoni mwa makosa ya kivita. Hii ni hatua kubwa muhimu katika historia ya utafutaji haki kimataifa, kwa wahanga walio nchini Kongo (DRC) na kwa mpango wa matumizi ya picha za video kwa ajili ya kuleta mabadiliko.

Huko Kongo Mashariki, ambapo vita vya wenyewe kwa wenyewe vimesababisha vifo vya zaidi ya watu milioni nne, watoto wadogo, wengine hadi miaka sita tu, walipatiwa mafunzo ya kijeshi na kufundishwa kuua. Inakadiriwa kwamba watoto, wengi wakiwa kati ya miaka minane na 16, wanakaribia asilimia 60 ya wapiganaji katika eneo hilo.

Video ya dakika 5 inayoitwa “Wajibu wa Kulinda” iliyowekwa na kampeni ya kukusanya picha za video za ushahidi inayofahamika kama WITNESS ilionyeshwa katika hatua za awali za kuendesha mashitaka hayo, na ilisifiwa na jaji kwa kuwa sehemu muhimu katika matokeo ya kesi hiyo pamoja na ushahidi mwingine wa picha. Inasimulia tukio la Mafille na January, wasichana wawili ambao walipewa mfunzo ya kivita. Picha hizo za video zinaonyesha madhara yanayotokea katika familia na jamii kwa ujumla kutokana na kuwafunza watoto mambo ya kivita.

Mmoja wa wafanyakazi wa kampeni hiyo ya WITNESS, Bukeni Waruzi, anayetokea Kongo Mashariki, ambaye pia ni mtetezi wa muda mrefu wa haki za binadamu, alikuwa mjini The Hague kusikiliza hukumu hiyo. Alishiriki pia katika kipindi cha Maswali na Majibu na waandishi wa habari kufuatia hukumu hiyo mnamo Machi 14 akieleza pamoja na mambo mengine umuhimu wa picha za video katika uendeshaji mashitaka.

Katika video hii hapa chini, iliyowekwa na kampeni ya WITNESS katika You Tube mnamo tarehe 13 Machi, siku moja kabla ya hukumu, Bukeni anazungumza na Madeleine, mtoto aliyepata kuwa “askari” huko Kongo Mashariki, ambapo alifanya mbinu za kumwondoa msichana huko kutoka kwenye vikosi vya wapiganaji akiwa na umri wa miaka 15 na kisha kumwasili. Mwaka 2007, alitoa ushuhuda wake kama askari mtoto mbele ya Umoja wa Mataifa.

Bukeni na Madeleine wanajadili matumaini yao kufuatia matokeo ya shitaka la Lubanga na wanatumaini haki itachukua mkondo wake kwa askari watoto popote walipo.

Unaweza kupata habari zaidi kuhusu kazi ya Bukeni na kampeni ya WITNESS kuhusu askari watoto kwa kutazama hapa. here.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.