Uganda: Wananchi Wakasirishwa na Kukamatwa Kikatili kwa Kiongozi wa Upinzani

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Dk.Kiiza Besigye alikamatwa tena katika mji mkuu wa Kampala kutokana na kushiriki kwake katika Kampeni yaKutembea Kwenda Kazini usiku mmoja baada ya kuachiwa huru kwa dhamana.

Besigye alipewa dhamana kwa sharti kuwa asijihusishe na kampeni ambayo imeuweka utawala wa Uganda kwenye vichwa vya habari kwa majuma matatu sasa. Maandamano hayo yaliyoongozwa na upinzani yanalenga kwenye bei kubwa za mafuta ambazo zimepelekea kuwa na bei kubwa za vyakula na Rais Museveni ametia kiburi kwamba hataingilia kati ili kupunguza bei hizo. Maandamano hayo ya upinzani mpaka sasa yamesababisha vifo vya watu watano na na dazeni wengine kujeruhiwa kwa risasi.

Leo Besigye alikamatwa kwa mara ya nne, na mara hii kulikuwa na utumiaji nguvu zaidi kulikofanywa na wanajeshi pamoja na polisi. Dirisha la gari la Besigye lilivunjwa kwa vitako vya bunduki na bomu la machozi pamoja na upupu wa pilipili vilipeperushwa kwenye gari kabla ya Besigye kutupwa kwenye gari la polisi. Baadaye mshindani mkuu huyo wa Rais Museveni alipelekwa kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kasangati ambako aliachiwa kwa dhamana isiyo ya fedha taslimu ya Shilingi za Uganda milioni 5 (Takriban Dola za Kimarekani $2,100).

Matukio ya upinzani yalizuka tena leo dhidi ya kukamatwa kikatili kwa Besigye, na zaidi ya watu 100 wamejeruhiwa na polisi. Taarifa zisizothibitishwa zinaashiria kuwa pengine watu watatu wamefariki.

Waganda walio kwenye mtandao wanaripoti kwa uangalifu mkubwa kuhusu Kampeni ya Kutembea Kwenda Kazini. Watumiaji wa Twita na Facebook walikasirishwa na namna ambayo Besigye alikamatwa.

On Facebook

Watumiaji wa Facebook walielezea wasiwasi wao kuhusu unyama unaoongezeka wa polisi.

Don Wanyama alisema:

Je umeona picha za kukamatwa kwa Besigye? Sijawahi kuona aina hii ya uonevu. Unavunja gari ya mtu halafu unampulizia zaidi ya makopo matano ya mabomu ya machozi?? No mbaya zaidi ya kubaka na uhaini pamoja na mambo mengine yote aliyokwisha chapwa nayo. Inasumbua. Mpaka lini Besigye ataendelea kubeba maumivu ya watu ambao wanaonekana kuwa wameridhika na dhiki yao, ambao wamefyata?

Asiim Blessed Bryans aliripoti kwenye Facebook:

Polisi wanawatawanya watu wanofanya ghasia kule kibuli na eneo hilo linaonekana kurejea katika hali ya kawaida lakini maduka yote yamefungwa na polisi wameshadhibiti

Kwa mujibu wa Nicholas Lukyamuzi stesheni za Redio hazitangazi ghasia hizo:

Stesheni za Redio zinaogopa kufungiwa na kwa hiyo zinaendelea na program kama kawaida hakuna lolote linalotangazwa kuhusu ghasia

Godgfrey Holidays aliuliza, “Je nini kitatokea ikiwa tutakimbia kwenda kazini?“:

Wazo jipya tusitembee tena bali tukimbie kwenda kazini ninataka kuona ikiwa polisi wanaweza kukabili hilo….

Kwenye Twitter

Alama ya Twita ya #walk2work imekuwa ikitumika kutoa taarifa juu ya kampeni hiyo na tangu kukamatwa kwake asubuhi, ujumbe wa twita umekuwa ukija na taarifa mpya mbalimbali pamoja na maoni

@joydoreenbiira: Jinsi Besigye alivyokamatwa kwa mara ya nne – http://t.co/vJuyGLX VIA @ugandatalks KUPITIA @ugandatalks Hali yangu leo imedhoofu, SINA LA KUSEMA

@RedPepperUG: HABARI MPYA: Besigye kabla ya kukamatwa: “Sitaki kujito kuwa shahidi, Ninasisitiza tu haki yangu kama raia.” #walk2work

@Snottyganda: Kwa nini mtu amsukume kiongozi wa upinzani, Mtu ambaye aligombea kuwa rais chini ya viti vya gari la mizigo kama vile mhalifu #walk2work

@RedPepperUG: SHAHIDI: Barabara ya Mukwanor, na mitaa ya karibu ya viwandani watu ni wengi wanakimbia kutoka katikati ya mji #walk2work #ugandanews

@SMSMediaUganda: Kuna taarifa kuwa wafanyabiashara wa soko la Kisekka wanapinga na maduka yamefungwa. HABARI ZA KINA ZIKO NJIANI. Andika SUBNEWS & tuma kupitia namba 8198.

@dispatchug: Video ya kukamatwa kwa Besigye na polisi pamoja na askari kanzu. http://bit.ly/mmkO1T #walk2work

@SMSMediaUganda:
Besigye aachiwa: Kiongozi wa FDC Dk Kiiza Besigye ameachiwa kwa dhamana ya mahakama ya Shilingi milioni 5. Hapana http://tinyurl.com/3o7ozm8

@RedPepperUg: HABARI MPYA: MTN imethibitisha ‘kuharibika kwa mawasiliano ya simu’ inaeleza timu ya ufundi inayoshughulika kutafuta ufumbuzi wa suala hilo #walk2work #ugandanews kupitia @MTNUGANDACARE

Mwanasheria wa Besigye David Mpanga pia amekuwa akiandika ujumbe wa Twita kuhusu hali ilivyo. Unaweza kufuatilia habari mpya kama zinavyotokea hapa.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.