Niger: Njaa ya Kimya Kimya

Janga la njaa ambalo kwa kiasi kikubwa haliripotiwi ipasavyo huko Sahel limechukua sura kubwa ya kutisha kufuatia kiasi cha watu milioni 2.5 nchini Naija hivi sasa kuathirika na uhaba wa chakula. Mpango wa Kimataifa wa Chakula wa Umoja wa Mataifa (WFP) umeamua kuongeza hatua za dharura Wanablogu nchini Naija wanatafakari janga jingine la chakula baada ya lile la mwaka 2005, baa la njaa la mwaka huu ambalo ni matokeo ya upungufu wa mvua mwaka jana.

Waume wakielekeza nyuso zao katika Jangwa la Sahel imepigwa na Nawal _kwa leseni ya Creative commons kwenye Flickr

D. Evariste Ouédraogo aliandika yafuatayo kuhusu namna wanasiasa wanavyojaribu mara zote kupindisha mabaa ya chakula nchini Naija kwa namna ambayo huwaweka wao katika mwanga mzuri zaidi [Kifaransa]:

En 2005, les autorités avaient toujours tenté de convaincre l’opinion que la menace de famine était une simple rumeur malveillante, déshonorante. [..] Quelques jours après, son Premier ministre (PM), dans des propos non moins fallacieux, appelait pourtant à l’aide, la Communauté mondiale, pour cause de …famine [..] Aujourd’hui, la vérité est toute nue : dix jours seulement après le changement de régime au Niger, on apprend, dans une déclaration télévisée du chef de la junte au pouvoir, que la famine “menace l’existence de millions de Nigériens dans quasiment toutes les régions”. Le déficit en vivres est alors estimé à 400 000 tonnes. Tout le contraire donc des péroraisons de Mamadou Tandja, qui était allergique à l’idée de risques de pénurie alimentaire.

Mwaka 2005, mamlaka yalijaribu kupenyeza mawazo ya ushawishi kwamba tishio la njaa lilikuwa ni uvumi tu ulioenezwa bila ya aibu [..] Siku chache baadae, waziri mkuu, katika hali ya kujipinga hoja mwenyewe, bado aliomba msaada wa jumuiya ya kimataifa kwa sababu ya …njaa. Mwaka 2010, ukweli unajitokeza tena: siku 10 baada ya mabadiliko ya utawala nchini Naija, tunasikia kutoka kwa mkuu wa utawala wa kijeshi kwenye luninga kwamba njaa inatishia mamilioni wa wananchi wa Naija kutoka mikoa yote ya nchi hiyo. Uhaba wa chakula ulikadiriwa kuwa tani 400 000. Kinyume kabisa cha kauli iliyotolewa na Mamadou Tandja ambaye alikuwa anakerwa na habari za hali mbaya ya chakula.

Grioo.com inauliza kwa sauti kubwa swali gumu lakini lililo bayana kwamba Wanaija wengi wanashangazwa kuhusu: ““fedha zilizopatikana kutoka kwenye biashara ya madini ya Uranium zilikwenda wapi?” ” [Kifaransa]:

Qu’on se rappelle les tiraillements entre l’ex-chef de l’Etat du Niger et les premiers responsables d’AREVA à propos du renouvellement des contrats d’exploitation de l’uranium. [..] On ne dénoncera jamais assez ces slaloms qui permettent à des délinquants à col blanc d’extorquer impunément les fonds publics qui devraient servir à sauver de nombreux concitoyens en manque de nourriture, d’eau et de soins de base. Les masses d’argent tirées des ressources minières ne profitent généralement pas à la majorité silencieuse. Un paradoxe africain qui n’étonne guère. Mais aussi un scandale qui doit prendre fin en ce début de millénaire. A croire que les ressources minières n’apportent que misère aux populations africaines. Et il en sera tojours ainsi tant qu’elles ne seront pas utilisées à développer les cultures céréalières.

Na tukumbuke shinikizo kati ya wakuu wa nchi wa zamani nchini Naija na viongozi wa eneo la Areva kuhusu kupitiwa upya kwa mikataba ya kuchimba Uranium […] Hatutaweza kupingana vya kutosha na mbio hizi zinazosaidia magenge ya watu wenye kazi za ofisini kufakamia hazina za umma ambazo zinapaswa kuchangia katika kuwasaidia raia ambao wanakosa chakula, maji na huduma za afya ya msingi. Kiasi cha fedha kutoka kwenye rasilimali za madini kamwe hakiwasaidii walio wengi ambao hawana sauti. Vioja vya Kiafrika ambavyo havitushtui tena. Hata hivyo, kashfa hii inapaswa kuisha sasa katika mwanzo wa Milenia mpya. Inaonekana kana kwamba utajiri wa madini unaleta dhiki tu kwa idadi kubwa ya Waafrika. Itakuwa hivyo mpaka vyanzo vyote vitakapokoma kutumika kuwa mashamba ya kulimia.

Kathryn Richards at Care anatushirikisha mawazo machache na ushuhuda wa “majira ya njaa” kadri idadi kubwa ya watu wa vijijini wanavyojikuta wakiwa kwenye uhitaji mkubwa wa mifugo ya kuchunga::

Naija ni nchi ya vinyume. Tajiri katika madini na mafuta yaliyogunduliwa siku za hivi karibuni lakini watu wake ni masikini wa kutisha. [..] Chakula kinapatikana katika soko –lakini kwa bei iliyopaa sana ambayo ni watu wachache tu wanaweza kuimudu. Familia zinauza mifugo yao kwa bei ya chini ili kununua chakula. Mohammed Gusnam alikuwa mmoja wa watu hawa: “ Ni vigumu . Kama wafugaji tulikuwa kama wana wa mfalme, wenye kiburi. Sasa ardhi ya kuchungia inapotea na tumekwama huko kijijini. Kijiji ni kama gereza kwangu.”

Mwitiko wa sasa wa janga la chakula, hata hivyo, unaonekana kuwa na kasi kubwa zaidi kuliko ilivyokuwa mwaka 2005. Cyprien Fabre, kiongozi wa kitengo cha eneo maalumu wa Tume ya Ulaya ya Misaada ya Kibinadamu (ECHO) anatoa tathmini ifuatayo [fr]:

Des mécanismes d’alerte précoce et d’intervention sont en place dans la plupart des pays touchés, et des fonds ont été alloués rapidement. Les opérations sont en bonne voie au Niger, au Burkina Faso et au Mali. Le Tchad a besoin de plus d’acteurs pour une intervention efficace.

Viamshi na miundo ya kutoa misaada inafanya kazi katika nchi nyingi zilizoathirika na mafungu ya fedha yalitengwa kwa utendaji kazi kama ipasavyo. Operesheni zinaendelea katika nchi za Naija, Burkina-Faso na Mali. Chadi inahitaji mawakala zaidi kwa ajili ya ufanisi wa zoezi la utoaji misaada.

Bado mashirika mengi yanaamini kwamba vitendea kazi bado vinawasili kwa uchelevu sana. Mashirika hayo yanabainisha sababu mbili za uchelevu huo: 1) kuhakikisha kwamba wafadhili wanakuja na fedha za ufadhili na 2) changamoto za kuifikia idadi kubwa zaidi ya watu katika maeneo yasiyofikika kirahisi. Wengi wanafikiri kwamba kutoa fedha taslimu inaweza kuwa ni njia ya haraka na ya ufanisi zaidi katika kipindi kifupi kuliko kutuma (misaada hiyo kwa namna ya) chakula [Kifaransa]:

Au cours de discussions avec les membres des communautés, davantage de personnes ont dit préférer les espèces aux semences. Les communautés ayant accusé les pertes de récoltes les plus importantes ou qui vivent plus loin des marchés tendent à opter pour les semences ; celles qui ont accès aux marchés, ont accusé des pertes de récoltes moins graves, ou ont un accès limité aux terres tendent au contraire à privilégier le cash.

Wakati wa mazungumzo na wanajamii hizo, watu wengi walisema kwamba wangependelea kupata fedha taslimu badala ya mbegu za nafaka. Jamii zilizokuwa zimepoteza mazao mengi au wale wanaoishi mbali na masoko wanachagua mbegu za nafaka; wale wenye uwezekano wa kufika kwenye magulio hawajapoteza sana ama wanayo ardhi isiyotosha, hupendelea kupata fedha taslimu.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.