Ivory Coast: Mwanablogu na Mwandishi wa Habari Théophile Kouamouo Akamatwa Pamoja na Timu Yake Tangu Julai 13

Mnamo tarehe 13 Julai, blog ya Le Nouveau Courrier [Fr], iliripoti kwamba walikuwa wamepata ugeni wa ghafla wa polisi baada ya kuchapisha asubuhi ya siku hiyo sehemu ya kwanza ya mfululizo wa habari ya uchunguzi ya kina ambayo ingekuwa ikichapishwa kwa wiki nzima, uchunguzi huo unahusu shutuma za ufisadi katika biashara ya kokoa na kahawa inchini Ivory Coast (tazama makala hiyo ya Kifaransa hapa).

[…] le journal a publié aujourd’hui, à sa une, un dossier exclusif au sujet de l’enquête sur les détournements dans la filière café-cacao titré : « Le livre noir de la filière café-cacao, comment les barons ont pillé l’argent des planteurs ».

Le boom que ce dossier a créé au sein du lectorat ce matin a mis en branle les services du procureur de la République Tchimou Raymond. Sur instruction de celui-ci et sans aucun mandat de perquisition, des commissaires et lieutenants de la police criminelle ont débarqué à la rédaction de Le Nouveau Courrier avec pour mission, disent-ils, de récupérer le document de base ayant servi à la rédaction de l’article. Après avoir fouillé tous les ordinateurs de la rédaction, ils ont finalement emportés avec eux un ordinateur portable au lieu du fameux document.

[…] gazeti hilo limechapisha leo, katika ukurasa wa mbele, makala maalumu kuhusu uchunguzi wa matumizi mabaya ya fedha katika biashara za mazao ya kahawa na kokoa. Makala hiyo ilipewa jina: “Kitabu Cheusi katika biashara ya kahawa-kokoa, jinsi wafanyabiashara wakubwa walivyojichotea fedha za wakulima”.

Matokeo ambayo ripoti hiyo imekwishapata kwa maana ya idadi ya kusomwa mpaka asubuhi ya leo imemfanya mkurugenzi wa makosa ya jinai, Raymond Tchimou, kuchukua hatua. Kwa amri yake na pasipo kuwa na waranti ya upekuzi, maofisa wa polisi wa kuchunguza jinai waliibuka katika ofisi za Nouveau Courrier huku wakiwa na lengo, kama walivyodai wenyewe, kukamata nyaraka muhimu ambazo zilitumika kama chanzo cha makala yetu hiyo. Baada ya kupekua kwenye kompyuta zote katika ofisi ya uhariri mwishowe waliondoka na kompyuta ndogo ya laptop badala ya kupata nyaraka hizo maarufu.

Baada ya upekuzi usio na mafanikio katika ofisi za Le Nouveau Courrier, mchapishaji Stéphane Guédé, mhariri mtendaji Théophile Kouamouo na mhariri editor Saint Claver Oula walichukuliwa na kutupwa korokoroni baada ya kukataa kutaja na kuonyesha vyanzo vyao vya habari.

Nouveau Courrier ni gazeti jipya la kila siku ambalo limeanza kazi innchini Ivory Coast yapata miezi miwili sasa, yaani tangu Mei 25, lengo lake likiwa ni kutoa mtazamo mpya wa kina wa masuala yanayotokea katika jamii. Mhariri mtendaji, Théophile Kouamouo ni mmoja wa wanablogu wa mwanzo na walio maarufu zaidi katika ukanda wa nchi zinazozungumza Kifaransa barani Afrika na yeye pamoja na mke wake, Nadine Tchaptchet-Kouamouo, ambaye naye ni mwanahabari, ni wafadhiliwa wa mradi wa Rising Voices kwa ajili ya mradi wanaouendesha wa Abidjan BlogCamps ambapo kwa kupitia mradi huo wao hufundisha masuala ya kublogu nchini Ivory Coast. Yeye ni raia wa Ufaransa mwenye asili ya Kameruni na alipata kufanya kazi na gazeti la kila siku la Ufaransa la Le Monde. Alikuwa akiripoti kutokea mji mkuu wa Abidjan kwa zaidi ya muongo mmoja, na ni miongoni mwa waandishi wa habari wanaoheshimika sana na pia ni mhadhiri wa masuala ya uandishi wa habari nchini Ivory Coast na kwingineko. Kama anavyojieleza mwenyewe kwamba yeye ni mjasiriamali wa vipengele vingi vya mtandaoni, moja ya harakati zake zenye mafanikio sana ni pamoja na jukwaa la wanablogu wa Ivory Coast la Ivoire-Blog.

Wanablogu kadhaa pamoja na waandishi wa habari wameonyesha kumwunga mkono na wenzake wa kutoka timu ya Le Nouveau Courrier hasa kwa kupitia utetezi wa mtandaoni wakidai waachiwe huru mara moja, na vilevile kupitia Twitter na kundi la Facebook ambapo watu mbalimbali wamechangia maendeleo ya kesi hiyo. Kupitia kundi hilo la Facebook tumejua kwamba waandishi hao watatu wamekuwa korokoroni tangu Jumanne, wakiendelea kubanwa ili wataje vyanzo vyao vya habari, na kwamba Ijumaa Julai 16 kesi yao ilikuwa isikilizwe na hakimu. Yaelekea wamehamishiwa katika gereza la MACA (Maison d'Arrêt Centrale D'Abidjan, Gereza Kuu la Abidjan). Mwanablogu wa Ivory Coast, Manasse Dehe, aliyeanzisha ukurasa huo wa Facebook, leo aliandika:

il n'est plus question de les libérer , c'est là le problème. mais de trouver laquelle des fautes ils ont commis; c'est déjà décidé qu'ils doivent payer pr kkchose qu'ils n'ont pas fait. maintenant les …avocats luttent pour que ce qu'on va leur coller, soir la
plus petite des infractions : genre flagrant délit
Appelle le Président de la Republique à réagir sur ton mur ! Car lui qui est homme de Justice; il peut sortir les 03 journalistes du nouveau
courrier de cette souffrance qu'ils ne méritent pas !!!!

Tatizo siyo tena hasa kuwaachia huru. Tatizo ni kuhusu kupata wamekamatwa kwa kosa gani, tayari imekwishaamriwa kwamba walipe kwa ajili ya kitu ambacho hawakukifanya. Hivi sasa wanasheria wanapambana kuamua wawashitaki kwa jambo lipi, hata kama ni kitu kidogo. Mmpeni taarifa Rais wa Jamhuri achukua hatua, fanyeni hivyo kupitia kurasa zenu za Facebook! Maana yeye ni mtu wa haki, anaweza kuamuru waandishi hawa 3 wa Le Nouveau Courrier kuachiwa huru na kuondokana na mateso haya wanayopitia pasipo kuyastahili hata kidogo!!!

Saint-Clavier Oula akiwa kwenye chumba chake cha mahabusu leo hii

Hii ndiyo taarifa iliyotumwa mara ya mwisho kwenye ukurasa wa wa Facebook Le Nouveau Courrier's :

Théophile Kouamouo, Saint-Clavier Oula, Stéphane Bahi sont actuellement enfermés dans une cellule pleine à craquer. Attendant leur tour devant le juge. Oula est très affaibli. Il a commencé une grève de faim et refuse aussi de prende ses medicaments…

Théophile Kouamouo, Saint-Clavier Oula, Stéphane Bahi wamefungwa katika chumba cha mahabusu kilichofurika. Wanasubiri zamu yao ya kufikishwa mbele ya hakimu. Oula anaonekana dhaifu sana. Alianza mgomo wa kula na pia amegoma kabisa kumeza dawa zake ….

Tangu habari za kukamatwa kwao zisambae Jumanne iliyopita, waandishi hawa wa habari wamekuwa wakipata uungaji mkono kutoka kwa wenzao na vilevile kutoka kwa wanablogu ndani na nje ya Ivory Coast.

Waandishi wa Habari Wasio na Mipaka walitoa taarifa siku ya Jumatano Julai 14 wakisema:

imepita miaka mingi tangu waone njia za namna hiyo zikitumiwa na mamlaka nchini Ivory Coast. Tuhuma za wizi haziwezi kusimama. Ni lazima itambuliwe kwamba kuweka siri ya vyanzo vya habari ni kanuni ya msingi katika taaluma ya uandishi wa habari, na hasa katika suala nyeti sana kama hilo linalohusisha ufisadi katika biashara ya kahawa na kokoa.

Katika ukurasa wa Facebook, baadhi ya wanahabari walisema kwamba Kifungu cha Kwanza katika Mwenendo wa Maadili ulio Rasmi kwa ajili ya waandishi wa habari wa Ivory Coast kama ulivyochapishwa na Wizara ya Mawasiliano (tazama nakala halisi katika Kifaransa hapa) inataja haki za waandishi wa habari nchini Ivory Coast kama:

Tout journaliste doit revendiquer les droits suivants :
Article 1 : La protection de ses sources d’information.

Pia kinaeleza wajibu wa waandishi wa habari, miongoni mwake ni:

Article 8 : Ne jamais révéler les circonstances dans lesquelles le journaliste a connu les faits qu’il rapporte, et ce, pour la protection de l’auteur des informations qu’il a pu recueillir.

Leo asubuhi chama cha magazeti ya Ivory Coast (Gepci) kilitoa tamko [Fr] ckikishutumu kukamatwa huko na kushambuliwa huko kwa uhuru wa kujieleza nchini Ivory Coast:

Emprisonner des journalistes pour les contraindre à violer leur propre déontologie en livrant leur source d'information n'est pas acceptable. Surtout que la loi 2004-643 du 14 décembre 2004 portant régime juridique de la presse n'autorise plus qu'un journaliste soit privé de sa liberté pour des faits, en rapport direct avec l'exercice de son métier, tels que ceux reprochés aux responsables et aux journalistes du quotidien Le Nouveau Courrier.

Zana ya Ukusanyaji taarifa kuhusu uandishi wa habari wa kiraia nchini Ivory Coast katika Avenue 255 [Fr], ambao wamekuwa wakifuatilia sakata hili tangu Jummane, waliripotikwamba umoja wa magazeti umetangaza nia ya kuchapisha sehemu iliyobaki ya ripoti ya uchunguzi kuhusu biashara ya kahawa na kokoa endapo waandishi hao wa habari hawataachiwa leo.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.