Alama ya #AchaHofu Yatumika Kufuatilia Uchaguzi wa Mexico

"Quiero democracia". Fotografía de Marte Merlos bajo licencia CC BY-NC-ND 2.0

“I want democracy”. Picha na Marte Merlos chini ya leseni ya Creative Commons CC BY-NC-ND 2.0

Wakati uchaguzi wa Jumapili iliyopita nchini Mexico ukiwa unaendelea, taasisi ya kulinda uhuru wa kujieleza iitwayoARTICLE 19 iliendesha kampeni ya #RompeElMiedo (#AchaHofu) kwa lengo la kufuatilia usalama wa waandishi wa habari na wanaharakati wa haki za binadamu. Jitihada hizo zilijikita kwenye majiji ya Mexico City, Guerrero, Michoacan, State of Mexico, Oaxaca, Puebla, na Guanajuato (yote yakiwa ni maeneo yenye hatari kwa wanahabari hasa nyakati za uchaguzi kwa siku zilizopita).

Mtandao wa #RompeElMiedo , ambao hukusanya malalamiko kuhusiana na kubughudhiwa kwa waandishi wa habari na haki za wafanyakazi, umefunguliwa mara kumi 11 tangu mwaka 2013 ulipozinduliwa kwa mara ya kwanza.

La frecuencia de las agresiones sigue aumentando: en temporada electoral, una cada 10.6 horas. Durante la primera quincena de mayo, se registraron 34 agresiones contra comunicadores; de estas, ocho se relacionan directamente con la cobertura de actos de campaña o hechos relacionados con las elecciones. Estos ataques son ejemplo de la falta de condiciones para el ejercicio de los derechos a la libertad de expresión e información.

Desde su inicio, la red ha hecho un llamado directo a los gobiernos del Distrito Federal, de la República, así como a los diferentes gobiernos estatales y municipales, para que de manera pacífica y apegada a los estándares internacionales en materia de derechos humanos garanticen el adecuado desarrollo de las jornadas de protestas y el libre flujo de información en estos contextos.

Vitendo hivi vinavyosukumwa na hasira vinatokea mara nyingi. Katika kipindi cha uchaguzi, tafiti zinaonesha kunakuwa na tukio moja katika kila baada ya masaa 10.6. Wakati wa nusu ya kwanza ya mwezi Mei, mashambulizi 34 dhidi ya waandisi yaliripotiwa; nane kati yake yanahusiana na habari za kampeni na uchaguzi. Vitendo vya hasira ni mfano wa mazingira ya kukosekana kwa usalama linapokuja suala la uhuru wa kujieleza sambamba na uhuru wa kupata habari.

Tangu kuanzishwa kwake, mtandao huo umetoa wito kwa maafisa wa majiji, majimbo na hata kwa ngazi ya kitaifa kutoa ulinzi kwa waandamanaji na kuruhusu kusambazwa kwa habari kwa kigezo kwamba vyote hivyo vinafanyika katika namna ya amani na inayozingatia sheria, na kwa mujibu wa viwango vya kimataifa vya haki za binadamu.

Kama sehemu ya shughuli zake wakati wa zoezi la upigaji kura nchini Mexico’, ARTICLE 19 walichapisha habari kadri zilivyokuwa zikitokea kwenye mtandao wa Tumblr kuhusu hali halisi ya habari za uchaguzi, ikiwa ni pamoja na mapendekezo ya kiusalama kwa waandishi na wanaharakati waliokuwa kwenye maeneo mbalimbali. Jukwaa hilo pia lilitumiwa kutengeneza ramani ya kufuatiliavisa vya mashambuzi:

Mapa de agresiones durante la cobertura de las elecciones en México 2015. Red #

Ramani ya kufuatilia mashambulizi kwenye uchaguzi wa nusu muhula wa Mexico 2015. Mtandao wa #RompeElMiedo (KuvunjaHofu).

Kwa kutumia alama habari ya #RompeElMiedo (KuvunjaWoga), waangalizi wa uchaguzi waliweza, tena kwa haraka, kuweka kumbukumbu kuhusiana na ukiukwaji wa kanuni za uchaguzi pamoja na matukio ya matumizi ya nguvu:

Armando Rincón, afisa wa INE (Tume ya Uchaguzi) anazuia waandishi kufanya kazi zao.

Polisi wa Cholula police wamemrudisha mwandishi.

Mwandishi Azucena Rivas alidhalilishwa huko Lara Grajales na watu wa CTM (Shirikisho la Wafanyakazi nchini Mexico) waliokuwa wakiendesha gari likiwa na nambari za usajili SJ90830.

Mashambulizi dhidi ya @centronline yamekuwa makubwa tangu masaa ya asubuhi, Juni 7.

Pamoja na taarifa kwenye alama habari hii, unaweza kufuatilia habari za uchaguzi wa nusu muhula nchini Mexico kwa kutumia alama habari zifuatazo: #Elecciones2015 na #Votaciones2015.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.