Mjamzito wa Miaka 11 Agoma Kutoa Mimba Nchini Uruguay

Kugoma kwa mjamzito wa miaka 11 kutoa mimba kumesababisha utata.

Hivi karibuniTuliandika kuhusu msichana wa miaka 10 aliyekuwa mjamzito nchini Paraguay kwa kudaiwa kubakwa na baba yake wa kambo na namna alivyoshindwa kutoa mimba hiyo kwa sababu sheria za nchi hiyo zinazuia utoaji wa mimba. Sasa, nchini Uruguay, ambako utoaji wa mimba unaruhusiwa ndani ya majuma 12 ya mwanzo ya ujauzito, tukio la msichana wa miaka 11 aliyegoma kutoa mimba limeishangaza nchi.

Msichana huyu, anayesemekana kuwa na ulemavu wa akili, alibakwa na babu wa dada yake wa kambo mwenye miaka 41. Mwanaume huyu kwa sasa yuko kizuizini na anashitakiwa kwa makosa ya ubakaji, wanasema maafisa wa Uruguay walipozungumza na Agence France-Presse.

Wanafamilia, madaktari, mashirika ya kijamii, na vyombo vya habari vimemshawishi msichana huyu kuitoa mimba hiyo. Wameishinikiza serikali kujaribu kumlazimisha kufanya hivyo, kwa mujibu wa jarida la Pangea Today. Majibu, hata hivyo, hayajawaridhisha:

“Hakuna hatari yoyote kwa maisha yake wala mtoto, kwa hiyo hatuwezi kumlazimisha kutoa ujauzito huo,” mkurugenzi wa INAU, Monica Silva, alisema.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.