Mbali na Kusikia Habari za Boko Haram Nchini Niger, Fahamu Jangwa la Ténéré

Arbre du Ténéré in 1961.CC-BY-SA 2.0

Mti wa Ténéré mwaka 1961. CC-BY-SA 2.0.

Kwa sasa, mgogoro na Boko Haram huko Kusini Magharibi mwa Niger ndio unaotawala vichwa vya habari vya nchi hiyo.  Mapema Machi 3, Boko Haram waliwaua raia 19 katika shambulizi lililotokea katika vijiji viwili vya, Kiu Keleha na Toubu Buka, vilivyopo pembezoni mwa ukanda wa mto Chad uliopita nchini Nigeria. Kufutia tukio hili, wanajeshi wa Nigeria waliungana na majeshi ya nchi nyingine za jirani katika kukabiliana na kundi la Boko Haram.

Hata hivyo, pamoja na juhudi zote hizi, sehemu ya Kusini Magharibi mwa Niger bado ni sehemu hatari na iliyotengwa.  Mkakati mpya wa wanablogu wa Nigeria, Mapping for Niger, unasaidia kulitambulisha taifa kwa kuonesha maeneo mbalimbali ya miji, wameanza kuliweka katika ramani eneo la Niger ambalo watu wengi wanaoishi huko hawakuwahi kulifahamu.

Magharibi: Eneo lililotengwa na mahali palipo na mtoto mdogo wa mfalme

Kama ilivyo  kwa Mti wa Ténéré (ambao kwa muda mrefu umekuwa mti uliojitenga kuliko mwingine wowote ule duniani, ambao kipindi fulani uliharibiwa na dereva ambaye hakuwa makini), Niger ya Magharibi kwa kiasi fulani imetengwa ukilinganisha na sehemu nyingine yoyote ya nchi hii. Kutengwa huku kwa Niger ya magharibi kunafanya mikakati ya kukabiliana na Boko Haram kuwa migumu, na hivyo kulifanya eneo hili kushambuliwa kwa urahisi na magaidi. 

Hata vivyo, historia ya eneo hili, hususani mti wa Ténéré, ni wa kipekee sana.

Mti wa kihistoria wa Ténéré ulikuwa ni wa jamii ya acacia, uliojitenga katikati mwa jangwa, mti wa pekee ulio katika kipenyo cha jangwa cha kilomita 400 sawa na maili 250. Ulikuwa ni mti wa pekee duniani uliokuwa umejitenga, uliokuwa unatumiwa kama alama na safari za watu waliosafiri kwa magari kupitia Sahel, lakini pia ni mti uliopendwa sana na washairi, waliotokea kulipenda jangwa hili kama inavyooneshwa katika video hizi zilizowekwa na A. Décotte:

na B. Hofmans:

Katika picha za Google pamoja na picha za ardhini za Google, mahali palipo na mti wa Ténéré kunaoneshwa kwa picha ya kuvutia ya mti huu iliyoambatana na maneno ya”The Little Prince” (imewekwa na Pierre Destruel):

Le Petit Prince est de Retour - Photo mixé par Pierre Destruel

“Mtoto mdogo wa Mfalme amerejea: Kinacholifanya jangwa kuvutia ni kuwa kuna sehemu katika jangwa hili kuna chemmchem. Picha na Pierre Destruel.

P. Destruel ameweka picha ifuatayo katika kuelezea taswara aliyoijenga kati ya mti na mtoto mdogo wa mfalme, akitumia kifungu cha maneno kutoka kwenye kitabu cha Antoine de Saint-Exupéry:

Iangalie kwa makini ili baade uweze kuitambua vizuri endapo siku moja utasafiri katika jangwa hili. Kama utafika mahali hapa, tafadhali, usiwe na haraka. Subiri kwa muda, sawia chini ya jua. Kama atatokea kijana mdogo akicheka, aliye na nywele za rangi ya dhahabu na akataaye kujibu swali lolote, hapo utakuwa umeshamtambua yeye ni nani. Kama hili litatokea, tafadhali, unifariji. Nitumie ujumbe kuwa tayari amesharejea.

Mradi— Kuchora ramani za kufuatilia matukio nchini Niger

Mradi wa kuitangaza Niger&nbsp, uliosaidiwa na ufadhili kutoka Rising Voices, unalenga kuboresha taarifa katika ramani ya Nigeria zitakazowezesha kuonekana kwa sehemu muhimu za uwekezaji pamoja na barabara kuu nchini kote. Mradi huu unaendeshwa kwa ushirikiano na idara ya Jiografia ya Chuo Kikuu cha Abdou Moumouni kilichopo Niamey, wanafunzi wake, Open Street Map, pamoja na Rising Voices. Mradi huu unatoa mafunzo stahiki kwa ajili ya mradi huu kwa wanafunzi pamoja na washiriki wengine wote.

Wakiwa tayari na ujuzi wa maarifa haya mapya ya uboreshaji wa ramani pamoja na uanahabari wa kiraia, washiriki wamekuwa wakitembelea vijiji vya karibu ili kuboresha katika ramani taarifa za maeneo muhimu kama vile shule, barabara pamoja na hospitali. Wameweza pia kutumia maarifa waliyojifunza kwa kuunganisha ramani walizoziandaa na mahitaji muhimu ya jamii. Kwa mfano, kwenye Siku ya Wanawake Duniani, mchango wa washiriki wanawake ulitambuliwa na kusherehekewa katika katika kituo cha mafunzo na mashirika ya ITECH CENTER, Fada Tech, na Femmes & Tic Niger (Umoja ulioanzishwa na Fatima Alher, ambaye ni mmoja wa wanachama wa Mradi wa Kuiweka Niger katika Ramani):

'atelier sur la Cartographie OpenStreetMap avec Femmes & TIC Niger via Mapping for Niger sur Facebook

Mafunzo ya OpenStreetMap ya uwekaji ramani na Femmes & TIC Niger (Iliyoanzishwa na Fatima Alher). PIcha Kutoka ukurasa wa Facebook wa Mradi wa Kuiweka Niger katika Ramani.

Hadi sasa, mradi huu umesaidia kuongeza na kuboresha ramani za Madaoua, Niamey, Dosso, Zinder, Kolmane, na Guidan Toudo. Mradi huu pia utazidi kupanuka taratibu katika maeneo mengine ya Niger. Mashirika mengine kama vile Search for Common Ground nalo litashiriki katika miradi kama hii ili kuboresha hali za wanajamii walio katika maeneo hatarishi. Pamoja na kuwa, katika hatua hii bado ni ushirikiano ambao siyo rasmi, Search for Common Ground linashiriki katika miradi mingine muhimu, ukiwemo wa jitihada za  kuleta hali ya umoja katika jamii na kuendeleza harakati za kuleta amani, hususani miongoni mwa vijana wadogo wa jamii ya Zinder:

Tulifanikiwa kuwapatia mafunzo vijana 172, wakiwemo wanawake zaidi ya 40. Washiriki walitoka katika matabaka tofauti ya kijamii, kuanzia wanafunzi wa vyuo hadi vijana wa magenge na wasiokuwa na elimu, na pia waliotokea katika makabila tofauti, marika tofauti na waliotoka katika taasisi mbalimbali. Vijana wengine 806, asilimia 10 wakiwa ni wanawake, walitoa mawazo yao kuhusiana na maarifa waliyojifunza na pia kutambua namna ya kutumia maarifa waliyoyapata katika mazingira yao. Mara baada ya mafunzo yetu, kiongozi wa kundi la vijana lililozaliwa upya aliomba kurudiwa kwa mafunzo hayo kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya ufundi iliyopo Zinder.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.