GV Face: Maandamano Yazuiliwa na Waasi wa Houthi Nchini Yemen

Yemen iko kwenye mzozo wa kisiasa, bila kuwa na rais wala serikali, tangu waasi wa Houthi kuangusha taasisi za kiserikali na kuteka ikulu kwenye mji mkuu wa Sanaa. Februari 8, waasi hao walitoa waraka kupitia Wizara ya Mambo ya ndani kupiga marufuku maandamano yoyote nchini Yemen.

Maamuzi ya nchi ya Hauthi: Maandamano hayaruhusiwi tena nchini Yemen. Karibu kwenye demokrasia mpya

Kwa tangazo la “Azimio la Kikatiba” lilifanywa na wanamgambo hao wa Houthi, mabadiliko mapya ya kimadaraka yanatokea. Wa-Yemeni wanafikiri nini? Wanakielewaje kipindi hiki cha mpito chini ya utawala wa wanamgambo wa Houthi na yepi ni matatizo yao makubwa?

Tunaongea na wanaharakati kutoka Yemen We Baraa Shiban (@BShtwtr), Osama Abdullah (@PoliticsYemen), na@NoonArabia kwenye toleo hili la GVFace. 

Amira Alhussaini, mhariri wetu wa Afrika Kaskazini na Uarabuni, aliongoza majadiliano hayo akiwa nami. Tunasikitika kwa matatizo kadhaa ya kiteknolojia na usikivu usioridhisha wa sauti kwenye mazungumzo haya. Mwanaharakati wa Houthi Hussaini Bukhaiti (@HussainBukhaiti) alipaswa kuungana nasi pia. Tulimkaribisha Bukhaiti, Osama na Baraa kuandika kwenye tovuti ya Global Voices kutusaidia kuelewa undani wa masuala yanayoikabili Yemen na matumaini yaliyopo kwa siku za usoni. 

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.