Watu 36 Wauawa, Mtandao wa Intaneti Wafungwa Kongo DRC Kufuatia Maandamano ya Kumpinga Rais Kabila

Screen Shot 2015-01-25 at 2.56.29 AM

Mnamo Januari 19, Polisi wa Kongo jijini Kinshasa walitumia nguvu kubwa kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wanapinga kubadilishwa kwa sheria ya uchaguzi itakayomruhusu Joseph Kabila kubaki madarakani.  Waandamanaji 35, wengi wao wakiwa wanafunzi na polisi mmoja waliuawa. Jiji la Goma liliathiriwa na mapigano yaliyosababisha kukamatwa kwa watu wengi miongoni mwa maelfu ya waandamanaji. Kabila anaonekana kutumia mbinu zisizo za moja kwa moja kutafuta kugombea muhula mwingine wa Urais katika uchaguzi wa unaotarajiwa kufanyika mwakani, kwa kuandaa sensa ambayo kwa kawaida huchukua miaka mitatu kukamilika. Kabila anazuiwa na katiba ya nchi hiyo kugombea kwa kipindi cha tatu, ingawa kwa kampeni ya sasa itabidi andelee kutawala mpaka sensa itakapokamilika. Muda mfupi baada ya maandamano, mtandao wa intaneti na huduma ya ujumbe mfupi wa maandishi kwenye simu vilizimwa pamoja na shule nyingi zilizopo jijini kufungwa. Baadhi ya mabweni yalichomwa moto wakati wa ghasia.

Utawala wa Kabila unadai kwamba sensa ni zoezi muhimu na linalostahili kupewa kipaumbele ili kuhakikisha kwamba orodha ya wapiga kura inaandaliwa vyema kwa ajili ya uchaguzi ujao wa Rais na wabunge unaotarajiwa kufanyika 2016. Kanisa Katoliki lenye ushawishi mkubwa nchini humo limeunga mkono madai ya upinzani ya kusimamisha shughuli yoyote ya kupitia upya ratiba ya uchaguzi. Mabadiliko yanayopendekezwa yanafanywa na Baraza la Seneti.

Video ifuatayo ya kijamii iliyopigwa na Kininfos Januari 19 inayoonesha sehemu ndogo ya ghasia kwenye mji huo mkuu wakati waandamanaji waijaribu kufunga mitaa:

Paul Nsapu, katibu mkuu wa Muungano wa Kimataifa wa Haki za Binadamu Barani Afrika unaofanya kazi zake Kinshasa, anashangazwa na hatua kali zilizochukuliwa na serikali: 

Kwa kiasi kikubwa watu hawa waliuawa wakati wakielekea kuandamana. Hatukutarajia serikali iwafayie hivyo utafikiri ni kikundi cha waasi.

Video ifuatayo inatoa muhtasari wa matukio katika juma lililopita:

Ida Sawyer, Mtafiti wa Kongo DRC wa Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch, anaongeza kwamba vitendo vya kuzima maandamano vinapingana na haki za raia ambao lengo lao ni kujieleza: 

Vikosi vya usalama nchini Kongo vimerusha risasi za moto kwa makundi ya waandamanaji na matokeo yake ni wengi kuuawa. Watu lazima waruhusiwe kusema maoni yao na hata kuandamana kwa amani bila hofu ya kuuawa wala kukamatwa

Mratibu wa programu wa Afrika wa CPJ, Sue Valentine anasema kuzima mtandao wa intaneti na mawasiliano ya simu katika nchi hiyo ni kukiukwa kwa haki za msingi za wa-Kongo

Kwa kuzima mtandao wa intaneti na huduma za ujumbe mfupi wa maandishi na kufunga tovuti, serikali ya Kongo inawanyima raia haki zao za msingi za kuwasiliana na kupokea na kusambaza taarifa

Jason Stearns anaeleza kwa nini waandamanaji wana hisia kali kwenye blogu yake ya Congo Siasa:

Waandamanaji sasa wanatimiza wajibu wao muhimu kuliko ilivyokuwa mwaka 2011. Maandamano yameanzia kwenye Chuo Kikuu cha Kinshasa (UNIKIN), kichovamiwa na watu wa usalama wa taifa pamoja na Polisi. Kuna wanafunzi 30,000 wa Chuo Kikuu, na mamia ya maelfu ya wanafunzi nchini kote. Mjini Bukavu, hali kadhalika, wanafunzi wa Chuo Kikuu walikuwa mstari wa mbele kwenye maandamano yaliyoandaliwa jana. Siku za nyuma, mijadala ya kisiasa katika Vyuo Vikuu mbalimbali nchini humo ilizimwa kirahisi kwa sababu vyama vya wanafunzi viliingiliwa na wanasiasa. Safari hii mambo yalikuwa tofauti.

Joseph Kabila alitwaa madaraka mwaka 2001 kufuatia kuuawa kwa baba yake Laurent Kabila. Chini ya Sheria ya Kongo, Polisi wanawajibu wa kutoa ulinzi na kuhakikisha umma unafanya maandamano kwa utulivu. Mkuu wa Polisi nchini humo ana mamlaka ya kuwaita wanajeshi wa nchi hiyo kutoa msaada kama polisi wanazidiwa.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.