Kufanyiwa Kazi na Faida za Matokeo ya Utafiti, Tafiti za Vyuo Vikuu Zina Tija?

Mawazo ikiwa umma wa wananchi unathamini tafiti zinazofanywa na vyuo vikuu, yamewachokoza mwanazuoni César Viloria kutoa mwangaza kidogo kuhusu suala hili kwenye blogu yake.

Kuhusu utafiti, lazima tufahamu kwamba kuna aina mbili kuu: utafiti msingi na utafiti tumizi. Utafiti msingi hufanywa kwa minajili ya kuongeza au kuja na maarifa mapya ikiwa ni pamoja na kukuza na kuboresha kile kinachofahamika tayari. Kwa upande mwingine, utafiti tumizi hujikita katika matumizi na uhitajikaji wa maarifa kwa jamii. Tunaweza kuona tofauti hii kwa kuangalia muda pia. Utafiti msingi matokeo yake ni ya muda mrefu wakati utafiti tumizi matokeo yake huonekana baada ya muda mfupi.

Unaweza kuwa unafikiri sasa, vipi kuhusu zile kanuni zenye tarakimu zisizowezekanika? Blogu hiyo imejibu vizuri swali hilo:

Encontramos una gran cantidad de elementos en estos artículos que pueden dificultar la lectura si lo que queremos saber es “de qué trata” pero servirían de gran ayuda si somos investigadores relacionados con el tema y queremos saber el “cómo lo hicieron”. Sin embargo, generalmente en la introducción y las conclusiones de estos textos es posible comprender una idea general del “para qué sirve”.

Tunakutana na mambo kadhaa katika kanuni hizi ambazo wakati mwingine ni vigumu kusomeka, kama tungependa kujua “maana yake hasa”, lakini kanuni hizi huwa muhimu sana kama sisi watafiti wenyewe tunaelewa mada husika na tunataka kujua “naona ilivyotokea”. Mara nyingi, hata hivyo, kwenye utangulizi na hitimisho la maandiko haya, inawezekana kuelewa wazo la jumla la “hiki kina maana gani”.

Kwa taarifa zaidi, Uninorte amezindua mpango unaoitwa Sayansi inayofikika, kutufanya tujisikie sehemu ya jamii ya kisayansi.

Unaweza kumfuatilia César Viloria Núñez kwenye Mtandao wa Twita.

Posti hii ni sehemu ya toleo la Ishirini na Sita la #LunesDeBlogsGV (Jumatatu ya blogu kwenye GV) mnamo Oktoba 27, 2014.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.