ISIS Yaonesha Video ya Mauaji ya Mwandishi Steven Sotloff

The Islamic State in Iraq and Syria has shared a second gruesome video which allegedly shows the beheading of American journalist Steven Sotloff. Photo shared widely on social media

Dola ya kiislam ya nchini Iraq na Syria imeweka tena hadharani video nyingine ya mauaji ya kutisha inayoonesha kukatwa kichwa kwa mtu anayedhaniwa kuwa ni mwandishi wa habari wa Marekani, Steven Sotloff. Picha hii ilisambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii

Video ya pili ikoneshayo mauaji ya kukatwa kichwa mwandishi wa habari wa Marekani, mauaji yaliyofanywa na dola ya Kiislam ya Raq na Syria(ISIS), dola iliyo na chimbuko lake kutoka kwenye kundi la Al Qaeda, kundi lililofanikiwa kutawala theluthi moja ya nchi ya Syria na robo ya nchi ya Iraq.

Video hii ya dakika tatu inadaiwa kuonesha kukatwa kichwa kwa Steven Sotloff, ambaye amekuwa akifanya kazi sehemu hatari katika maeneo mbalimbali ya Mashariki ya Kati kama vile Bahrain, Syria, Egypt, Libya na Uturuki.

Sotloff hakuonekana kuanzia mwezi wa Agosti mwaka jana akipasha habari kutoka Syria.

Video hii ya kutisha inakuja mara baada ya ile ya kuchinjwa kwa mwandishi wa kimarekani wa habari katika picha, James Wright Foley, ambaye hakuonekana nchini Syria kwa siku 636, kabla ya video iliyoonesha mauaji yake kuwekwa hadharani na ISIS mnamo August, 19.

Sotloff alitambulishwa katika video ya Foley, angalizo likitolewa kuwa, yeye ndiye atakayefuatia. Kwa mara nyingine tena, mateka mwingine, David Haines, raia kutoka Uingereza, inasemekana amejitokeza katika video hii.

DC-based journalist Zaid Benjamin aliye na masjani yake huko DC, atwiti kwa mashabiki wake wanaofikia 45.5K:

Kwa mujibu wa NBC News, Haines, aliyekuwa mmoja wa wanajeshi wa Uingereza, aliachana na jeshi na kufanya kazi na mashiririka yasiyo ya kiserikali, ambapo alifanya kazi za kulinda usalama.


Mshituko

Wengi waliipokea habari hii kwa mshituko.

Ruwayda Mustafah, ambaye ni Mkurdi Mwingereza, akiwa na watu 41K wanaomfuatilia katika mtandao wa Twita, alishikwa na butwaa:

Emile Hokayem, mchambuzi wa masuala ya Mashariki ya Kati katika Taasisi ya Kimataifa ya Mafunzo mkakati, alitoa ufafanuzi katika ukurasa wake wa Twita ulio na wafuatiliaji 15k akisema kuwa kuzagaa kwa video za kutisha za namna hii zikionesha madhambi yafanywayo na ISIS inazifanya jamii za Mashariki ya Kati kuchukulia matukio haya kuwa ni kawaida.Mideast analyst at the International Institute for Strategic Studies, explains to his 15K followers on Twitter saying the widespread of such horrific videos showcasing ISIS’ crimes desensitize Middle Eastern societies:

Aliendelea kufafanua kuwa, ISIS ipo makaini kusambaza video hizi ikiwa ni sehemu ya mkakati wake wa “kuwatisha” watu.


Washirika wake watuma salamu zao za rambirambi

Katika kurasa za Twita, wengi wamuelezea Sotloff kuwa ni mwandishi wa habari aliyekuwa makini.

Mwandishi wa habari katika picha, Mazen Mahdi kutoka Bahrain aeleza:

Anaongeza:

Mwandishi wa habari, Portia Walker alalama kufuatia kifo cha mwandishi huyu:

Kwa mara ya mwisho, Lauren Bohn alikutana na Sotloff jijini Cairo. Mwandishhi wa habari huyu asiye na mipakaThe multi-media journalist, ambaye kwa sasa yupo Istanbul, anakumbusha kuwarecalls:

Na mwaandishi wa Global Post, Jeb Boone alikutana na Sofloff nchini Yemen. Anakumbuka namna watu walivyokuwa wakishindwa kuwatofautisha:


#KuzuiwakwavyanzovyahabarivyaISIS

Kama ilivyokuwa kwa video ya Foley, wengi wanashinikiza habari za ISIS kuzuiwa. Badala ya kusambaza video ya ISIS ya mauaji ya kumkata mtu kichwa, watu wanawataka watu waomboleze kifo cha Sotloff kwa kumkumbuka kwa mazuri aliyoyafanya wakati wa uhai wake.

Miongoni mwao ni Zach Green, ambaye anasema:
Video ya

Tangu kuandikwa kwa Twiti hii, imeshasambazwa mara 800.

Kutoka Libya, Ismael atoa mchango wake:

Boone aongeza:

Na kutoka Lebanon, Elie Fares aelezea:


Kipi kinafuata?

Joshua Hersh, mwandishi wa habari anayeripotia Huffington Post Middle East aliye na maskanni yake New York, anasema kuwa, kuna juhudi hafifu kabisa katika kukabiliana na ukatili unaofanywa na ISIS:


Wakati haya yakiendelea..

Raia wa Syria, Razan Saffour anatukumbusha kuwa, hata waandishi wa habari wa Kiislam hawasalimiki wawapo mikononi mwa ISIS.

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.