Ucheshi na Harakati Kutoka Mexico

comedia

Picha na laranggio kwenye mtandao wa flickr. CC BY-NC-SA 2.0.

JM Casanueva, mwandishi wa blogu ya SocialTIC, anapitia mwelekeo mpya wa harakati nchini Mexico kwenye blogu na kwenye mitandao ya kijamii ambayo inatumia utani kuwafikia watu wengi zaidi:

El humor siempre ha sido una táctica exitosa para transmitir causas de manera empática (sí, que alguien que no seas tú o tus colegas activistas entiendan la problemática) y llegar a públicos más amplios (sí, más allá de lxs [sic] grupos de sospechosos comunes que siempre te retuitean). El activismo mexicano de 2014 ha tenido una muy buena dosis de humor por parte de comediantes que han aprovechado sus talentos, agudeza y compromiso social para buscar impactar en la sociedad.

Utani mara zote umekuwa ni mbinu inayofanikiwa sana kufikisha ujumbe (ndio, kwamba mtu fulani ambaye sio wewe au mwanaharakati mwenzako anaelewa tatizo) na kuifikia hadhira kubwa zaidi (ndiyo, zaidi ya makundi ya mtandaoni ya watu wanaokuhisi na kusambaza ujumbe wako). Wanaharakati wa Kimexico mwaka 2014 wamekuwa na dozi ya kutosha ya ucheshi kutoka wachekeshaji wanaotumia vipaji vyao, umakini na kujichanganya kwao na jamii kuleta manufaa kwa jamii.

Unaweza kufuatilia SocialTIC kwenye Twitter.

Posti hii ni sehemu ya saba ya #LunesDeBlogsGV (Jumatatu ya Blogu kwenye GV) tarehe 16 Juni, 2014.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.