Wanafunzi Waandamana Nchini Chile Kudai Mageuzi ya Kielimu

Protestas Chile

Maandamano Jijini Santiago de Chile. Picha na mtumiaji wa Flickrr NOtodoesARTE. CC BY-NC-ND 2.0.

[Viungo vyote vinaelekeza kwenye kurasa zilizo kwenye lugha ya Kihispania.]

Maandamano ya kwanza kudai elimu wakati wa utawala wa sasa wa Rais Michelle Bachelet yalifanyika Mei, 8, 2014, yakiwa na ruhusa.

Maandamano yalihudhuriwa na makundi kadhaa. Kuyataja kwa uchache ni pamoja na Shirikisho la Wanafunzi la Chile (Confech), Mkutano wa Taifa wa Wanafunzi wa Sekondari (ACES), Mratibu wa Taifa wa Wanafunzi wa Sekondari (Cones), Vuguvugu la Wanafunzi wa Elimu ya Juu (Mesup), Muungano wa Mashirikisho ya Sekta Binfafsi ya Elimu ya Juu (Ofesup) na Chama cha Maafisa wa Wizara ya Elimu (Andime).

Maandamano yalidai elimu inayotolewa kwa usawa na bure pamoja na ushirikishwaji wa moja kwa moja kwenye mageuzi ya elimu yanayoendelea hivi sasa. Gazeti la La Tercera liliandika:

Maandamano ya wanafunzi, nini hakiendi sawa sawa hapa? Rais wa Feuc anasema wanafunzi wanadai “kushirikishwa kwenye mageuzi”..

Maandamano yalifanyika wakati huo huo kwenye mji mkuu wa Santiago sambamba na maeneo mengine ya nchi hiyo. Ushiriki na uwepo wa idadi nzuri ya wanafunzi ulikuwa bayana:

Qué bueno ver que la marcha estudiantil fue masiva en #Santiago y regiones. Todos por una nueva educación, que construya un mejor #Chile

— René Naranjo S. (@renenaranjo) May 8, 2014

Inapendeza kuona kuwa maandamano ya wanafunzi yalikuwa makubwa jijini Santiago na kwenye maeneo mengine. Tumeungana pamoja kwa ajili ya elimu pya itakayoijenga Chile mpya.

Maelfu ya vijana walishiriki kwenye maandamano ya kwanza ya wanafunzi yaliyofanyika mwaka huu mwezi Machi huko Concepción.

Kulikuwa na maandamano kwenye miji mingine kwenye maeneo ya mashambani pia, kama vile  Iquique, Valparaíso, jiji ambalo ndiko liliko Bunge la Taifa, na Valdivia.

K abahati mbaya, kwenye baadhi ya maeneo maandamano yalikabiliwa na usumbufu wa hapa na pale, hasa uliosababishwa na watu wengine wasiokuwa wanafunzi na ambao hawakuwa na maslahi yoyote kwenye madai hayo.

Naschla Aburman, rais wa Feuc, aliviita vitendo hivyo vya usumbufu kama “matukio machache” na kusema kwamba vitendo hivyo havikuwa wajibu wa waandaaji.

Watumiaji wa Twita walitoa maoni yao kuhusu ukweli huo, wakisambaza picha na taarifa kuhusu matukio hayo:

AHORA: Intendente @orrego dice que “no hubo ningún incidente” durante marcha estudiantil. Sí “violentistas organizados” al final de ella

— Mauricio Bustamante (@tv_mauricio) May 8, 2014

2 maoni

  • Kiungo cha makala haya kutokea kwenye tovuti nyingine: Wanafunzi Waandamana Nchini Chile Kudai Mageuzi ya Kielimu | TravelSquare

    […] Wanafunzi Waandamana Nchini Chile Kudai Mageuzi ya Kielimu Maandamano Jijini Santiago de Chile. Picha na mtumiaji wa Flickrr NOtodoesARTE. CC BY-NC-ND 2.0. [Viungo vyote vinaelekeza kwenye kurasa zilizo kwenye lugha ya Kihispania.] Maandamano ya kwanza kudai elimu wakati wa utawala wa sasa wa Rais Michelle Bachelet yalifanyika Mei, 8, 2014, yakiwa na ruhusa. Maandamano yalihudhuriwa na makundi kadhaa. Kuyataja kwa uchache ni pamoja na Shirikisho la Wanafunzi la Chile (Confech), Mkutano wa Taifa wa Wanafunzi wa Sekondari (ACES), Mratibu wa Taifa wa Wanafunzi wa Sekondari (Cones), Vuguvugu la Wanafunzi wa Elimu ya Juu (Mesup), Muungano wa Mashirikisho ya Sekta Binfafsi ya Elimu ya Juu (Ofesup) na Chama cha Maafisa wa Wizara ya Elimu (Andime). Maandamano yalidai elimu inayotolewa kwa usawa na bure pamoja na ushirikishwaji wa moja kwa moja kwenye mageuzi ya elimu yanayoendelea hivi sasa. Gazeti la La Tercera liliandika: Marcha estudiantil: ¿Qué está en juego? Pdta de la Feuc dice que estudiantes quieren “participación en la reforma” http://t.co/kkESMigWrC — La Tercera (@latercera) May 8, 2014 Maandamano ya wanafunzi, nini hakiendi sawa sawa hapa? Rais wa Feuc anasema wanafunzi wanadai “kushirikishwa kwenye mageuzi”.. Maandamano yalifanyika wakati huo huo kwenye mji mkuu wa Santiago sambamba na maeneo mengine ya nchi hiyo. Ushiriki na uwepo wa idadi nzur… Kusoma makala kamili  »  http://sw.globalvoicesonline.org/2014/05/wanafunzi-waandamana-nchini-chile-kudai-mageuzi-ya-kielimu/ […]

  • Kiungo cha makala haya kutokea kwenye tovuti nyingine: Wanafunzi Waandamana Nchini Chile Kudai Mageuzi ya Kielimu | Placedelamode

    […] }); Wanafunzi Waandamana Nchini Chile Kudai Mageuzi ya Kielimu  » http:// sw.globalvoicesonline.org Maandamano Jijini Santiago de Chile. Picha […]

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.