Venezuela: Utata na Mashambulizi Wajadiliwa kwenye Mtandao wa Twita

Wakitumia alama ashiria #UcabCaracas na #SOSColectivosDelTerrorAtacanUCAB [SOS vikundi vya kigaidi vya mashambulizi UCAB], maoni na picha ya mashambulizi kwa wanafunzi kwenye maandamano ambayo inaonekana yalitokea katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Andrés Bello [es] mjini Caracas zimeonyeshwa sana. Miongoni mwa wale wanao twiti ndani ya chuo kikuu hicho, kilchosimamisha shughuli zake za kitaaluma, kuna kundi la harakati za wanafunzi wa UCAB [es] wakiweka habari na picha za wanafunzi waliojeruhiwa .

05:24 hali ya wasiwasi inaendelea katika chuo kikuu cha UCAB mjini CARACAS. Doria inaendelea kuja na kwenda katika lango kuu la chuo kikuu.

Kwa alama ashiria hizo hizo, mfululizo wa twiti na wafuasi wa chavismo walijaribu kukanusha habari, au kukosoa maandamano ya wanafunzi. Pia, kwa #SocialismoProductivo [Ujamaa wa uzalishaji] kundi hili linmetengezwa kuonyesha kile wanachokiona kama maandamano yasiyostahili kuwa na kulaani vitendo vya vurugu.

Hawa ni watoto ambao huamini kwamba hatua ni kuhamasisha vita bila kuwa na ufahamu wa madhara ya vitendo vyao.

Kuna ripoti ya maandamano katika vyuo vikuu vingine katika mikoa na wale ambao waliamua kujiunga na maandamano wamekosolewa kwa ukali. Haya yote yanaonyesha taarifa ya mchafuko na muono tofauti, mada kuu ya vita nchini Venezuela.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.