Mzee wa Kimasedonia Apambana Kurejeshewa Mali Yake

Mwanablogu na mwanaharakati wa kiMasedonia amelifunua suala la suala la Bw. Dushko Brankovikj [mk]. Brankovikj amekumbana na tahayaruki ya kujikuta mali zake zikitaifishwa mara mbili na serikali kwa miaka 65 iliyopita, na ingawa alishinda kesi mahakamani kuhusu suala hilo, bado taasisi za kiserikali zimeshindwa kutekeleza maamuzi hayo ya kimahakama na kumrejeshea mali zake.

Mzee huyo bado anahangaika kwa kudai haki yake mbele ya mahakama ya mwanzo jijini Skopje na anapanga kukata rufaa kwenye Mahakama ya Ulaya ya hai za Binadamu jijini Strasbourg.

Mwanaharakati wa kiMasedonia Nikola Pisarev alichapisha picha ya mzee huyo akiwa amebeba bango linalosomeka, “Inawezekanaje uamuzi wa manispaa ukawa imara kuliko uamuzi wa mahakama kuu? Imewezekana kwa Mahakama yetu Kuu. Kwa maamuzi haya tutaishia kwenye sayari ya Mars badala ya kutegemea Umoja wa Ulaya! Mahakama Kuu lazima iwe Msahihishaji, na sio kufanya masihara”:

Dushko Brankovikj protesting in front of Supreme Court in Skopje, Macedonia. Photo by Aleksandar Pisarev, published with permission.

Mzee akiwa mbele ya Mahakama Kuu jijini Skopje, Masedonia. Picha imepigwa na Aleksandar Pisarev, imechapishwa kwa ruhusa.

Pisarev vile vile alijumuisha maelezo zaidi ya picha hiyo kwenye blogu yake:

Индивидуалниот активизам често има за цел решавање на лични проблеми што е легитимно, особено кога повеќе луѓе се засегнати од еден ист проблем (како во случајов нефункционланоста и „неправедната“ правда на судството во Македонија). Затоа овој човек заслужува респект и поддршка од сите нас кои веруваме во моќта на активистичкото граѓанско делување.
Во отсаство на медиуми и во отсаство на институционална правда само протестот ни преостанува!
Човеков не го познавам, го запознав некни, индивидуално протестира пред суд скоро секој ден, ја бара правдата уште од 1973. Како што ми објаснуваше и тоа што ми покажа од материјали човеков е во право. За жал нефункционалната локална самоуправа му го загорчува животот и најгрубо му го крши правото на приватна сопственост.

Респект за чинот чичко.

Uanaharakati binafsi mara nyingi huanza kwa lengo la kutatua tatizo binafsi, jambo ambalo ni sahihi, kama ambavyo wengine wengi wanaweza kuwa wanaguswa na jambo lile lile (kwa mukhtadha huu utendaji usioridhisha wa mfumo wa kimahakama wa Kimasedonia unaosababisha haki ‘isiyo haki’). Kwa hiyo, mzee huyu anastahili haki na msaada kutoka kwetu sote tunaoamini katika nguvu ya hatua za kiraia.

Katika kimya cha vyombo vya habari na kutokuwepo kwa haki ya kitaasisi, jambo pekee linalowezekana kufanyika ni kuandamana!

Sikuwa namfahamu mzee huyu kabla. Nilikutana naye siku chache zilizopita, anapinga kuonewa akiwa peke yake mbele ya mahakama karibu kila siku, akitafuta haki tangu mwaka 1973. Kwa mujibu wa maelezo yake na nyaraka alizonionesha, yuko sahihi. Kwa bahati mbaya, serikali za mitaa zisizofanya wajibu wake zinafanya maisha yake kuwa machungu na kwa kweli inafanya iwe vigumu kupata haki yake.

Heshima kwako kwa kitendo ulichokifanya, mjomba.

Hivi karibuni ripoti ya Idara ya Haki za Binadamu ya Marekani kuhusu Masedonia, ilichapishwa tarehe 28, 2014, inabainisha masuala yafuatayo ya msingi, katika mengi, yanayoitafuna nchi hiyo:

“Mfumo wa mahakama una sifa ya kuingiliwa na siasa, utendaji usioridhisha, upendeleo kwa watu fulani fulani, michakato mirefu ya kimahakama, na ufisadi.”

Kama matokeo ya wasifu wa Pisarev kwenye blogu yake na mitandao ya kijamii, mashirika kadhaa huru ya habari yalichapisha habari za kesi ya Brankovikj na watu sasa wameanza kutoa maoni si tu kuhusu suala hili pekee bali na masuala mengine ya kimahakama ya Masedonia na mfumo wa kiserikali kwa ujumla kwenye mitandao ya kijamii na kwingineko.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.