Global Voices na Connectas Watangaza Kushirikiana Maudhui

connectaspage

Picha ya tovuti ya CONNECTAS.org.

Global Voices na CONNECTAS [es], shirika lenye mwelekeo wa kiuandishi wa habari la Amerika Kusini lenye makazi yake nchini Colombia, wamefikia makubaliano ya kushirikiana maudhui yanayoandikwa na CONNECTAS kwenye mtandao wa lugha nyingi wa Global Voices.

CONNECTAS ni mradi usio wa kibiashara wenye mwelekeo wa kiuandishi wa habari [es] wenye lengo la kuhamasisha uzalishaji, ushirikishwaji, mafunzo na usambazaji wa taarifa zinazohusiana na mada ambazo ni muhimu kwa maendeleo ya bara hilo”:

CONNECTAS inajitokeza kwenye mkutaniko wa fursa nyingi katika eneo hilo, na hitaji la taarifa zenye ukweli wenye manufaa ya mataifa ya bara hilo. Katika nchi za Amerika Kusini, pamoja na kuwa kwenye eneo lenye utamaduni unaofanana, historia na hata lugha, lenye taasisi za kiraia zilizo hai na pia kuongezeka kwa biashara za baina ya serikali moja na nyingine, hakuna taarifa za kutosha na zenye kunufaisha mataifa hayo kwenye eneo hilo.

Ukiacha maudhui ya kiuandishi wa habari, CONNECTAS inawezeshesha waandishi wa habari kupata mafunzo hususani kwenye mbinu mahsusi na mada pamoja na kuandaa mikutano, majadiliano na mazungumzo na viongozi maarufu pamoja na watunga sera. Pia wanatangaza sheria zinazohusu upatikanaji wa habari kwenye eneo hilo ikiwa ni pamoja na kubadilishana kwa takwimu kwa ajili ya uchunguzi, uchambuzi, utafiti na uelekezaji. 

Tunaamini kwamba makala na taarifa zinazozalishwa na CONNECTAS zinasaidia pia kwenye habari zetu za Amerika ya Kusini.

Soma makala ya kwanza iliyochapishwa kwa kiingereza na CONNECTAS kwenye mtandao wetu wa Global Voices, “Namna Magenge ya Wahuni Yalivyogeuka Kirusi kwenye Vyombo vya Kiusalama nchini El Salvador” Sehemu ya pili itachapishwa muda mfupi ujao.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.