Amnesty International: ‘Mfululizo wa Ghasia ni Tishio la Utawala wa Sheria Nchini Venezuela’

Shirika la kutetea haki za binadamu, Amnesty International limetoa taarifa inayo weka kumbukumbu sawa “kuhusu madai ya uvunjifu wa haki za bindamu na unyanyasaji uliofanywa katika mukhtadha wa maadamano makubwa ya umma tangu mwezi Februari.”

“Nchi hiyo iko kwenye hatari ya kuwa na mfululizo wa matukio ya ghasia kama hatua hazitachukuliwa kuzileta pande zinazosuguana kwenye meza ya mazungumzo. Hilo linaweza kutokea tu kama ande zote zinaheshimu kwa haki za binadamu na utawala wa sheria. Hilo lisipotokea, matukio ya vifo yataendelea kuongezeka na kuwaathiri zaidi watu wa kawaida,” alisema Erika Guevara Rosas, Mkurugenzi wa shirika la Amnesty International wa mabara ya Amerika.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, watu 37 wamepoteza maisha na zaidi ya 550 wamejeruhiwa:

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali mnamo Machi 27, watu 2,157 wamekamatwa wakati wa maandamano. Wengi wao wakiwa wameshaachiliwa lakini wakiendelea kukabiliwa na mashitaka.

Unaweza kusoma taarifa hiyo kamili hapa [es] kwenye tovuti ya toleo la lugha ya Kihispania ya shirika la Amnesty International.

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.