Ukuta Wetu wa Berlin Nchini Syria

Wanafunzi wa Syria kwa Mustakabali Bora ni blogu ya WordPress inayoendeshwa na wanafunzi wa Syria wanaosoma kwenye Taasisi ya Teknolojia ya Illinois. Wanafunzi hawa wanasoma nchini Marekani kama sehemu ya Mradi wa Jusoor kuwasaidia wananchi wa Syria kuendelea na elimu yao ya juu nje ya Syria kupitia ufadhili. Blogu hiyo, ambayo ina makala yaliyo katika lugha ya Kiarabu na Kiingereza, inaakisi matumaini ya wanafunzi hao, mashaka yao, wasiwasi wao, mtazamo wao chanya, homa ya kukumbuka nyumbani na matarajio kwa ajili ya mustakabali bora watakaporudi nyumbani.

Safouh Takrouri aliandika makala yake aliyoiita Ukuta wetu wa Berlin nchini Syria akisema:

Baada ya Wajerumani kuungana tena, watu na jamii zilizianza kupanga maisha ya mbeleni. Maisha yatakayokuwa mbali kabisa na vita, damu na migogoro. Mustakabali uliojaa mafanikio na maendeleo.

Hivi sasa watu wa Syria wamegawanyika katika makundi mawili -na labda zaidi. Kila kundi lina maoni yake, na linaamini katika muono wao kwa mustakabali wa nchi. Kila kundi liko sahihi kwa mantiki nyingi tu, na kadhalika lina makosa kwa namna nyingi vile vile. Hapana shaka, kila kundi linaipenda nchi yake na wengine wako tayari kuyatoa maisha yao kwa hiari kwa ajili ya nchi. Wakati wahanga wengi sana wa ghasia hizi za kutisha na mateso hawajawahi kuomba maisha yao wala yale ya familia zao yaharibiwe. Kila raia na mkazi wa Syria ana haki ya kutoa maoni yake kwa ajili ya mustakabali wa nchi ambayo mwane ataaishi, lakini maoni haya -hata yakiwa tofauti kwa jinsi yalivyo – lazima yaheshimiwe. Mijadala ya wazi, ya haki, uaminifu na ya wazi lazima iwe ndiyo mbinu yetu ya kufanya kazi pamoja; hili lazima liwe ndiyo sheria ya kimaadili, na kwa hakika imekuw ahivi kwa karne nyingi nchini Syria. Leo, tunakabiliwa na kushuka kwa hali hiyo.

Pamoja na habari mbaya zinazokuja kutoka Syria, siwezi kuwa na mtazamo hasi.

cropped-syrians_iitsign_iit1

Wanafunzi wa Syria kwa mustakabali borae. Chanzo ni Blogu ya WordPress. Imetumiwa na leseni ya Creative Commons BY CC 3.0

Mariela Shaker ambayenbsp;anafanya shahada ya kwanza ya musiziki kwenye chuo cha Monmouth, na awali alisoma kwneye Chuo Kikuu cha Aleppo, alifurahi kkutana na wanafunzi wenzake wa ki-Syria. Akiwa na matarajio kwa Syria iliyo bora anasema:

Ninatarajia sana kuwa wanafunzi wote wa Syria wanafanya vyema kwenye vyuo vyao vipya, na wanaendelea kujitahidi zaidi ili waendelee kuiwakilisha nchi yetu vizuri kwenye fani zote, ili nchi ya Syria ijisikie fahari kuwa na watu wa aina yetu siku zote.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.