Katika Kutetea Lugha za Malawi

Kufuatia uamuzi wa serikali ya Malawi kuanza kutumia Kiingereza kama lugha ya mawasiliano kuanzia darasa la kwanza, Steve Sharra anatetea lugha la asili na anajenga hoja yake katika kutetea matumizi ya lugha zaidi ya moja:

Walimu na wahadhiri katika shule zetu za sekondari na vyuo vikuu wanashuhudia mwenendo wa mambo unaoonyesha kuwa wanafunzi wa shule binafsi wanazungumza Kiingereza fasaha, lakini uwezo wao wa kufikiri, kuandika na uwezo wa kufanya mahesabu uko chini. Hili limeonekana kwenye ripoti ya Chama Huru cha Shule nchini Malawi (ISAMA) kuwa wanafunzi wanaochaguliwa kwenda kwenye vyuo vikuu vya Malawi wanatoka kwenye shule binafsi.

Watafiti wa lugha wamegundua kuwa watoto wanaozungumza lugha zaidi ya moja wanafanya vizuri zaidi kitaaluma kuliko watoto wanaofahamu lugha moja tu, bila kujali ni lugha gani. Hii ndiyo sababu sera yetu ya lugha ya kufundishia inatakiwa kukuza matumizi ya lugha zaidi ya moja, na sio kutumia lugha moja tu. Ni katika kipindi cha kizazi kimoja tu kilichopita ambapo Wamalawi wengi walikuwa wakizungumza lugha zaidi ya moja, kwa wastani wa lugha mbili au zaidi. Katika kizazi cha leo, wengi wanafahamu lugha mbili tu, Kiingereza na Ki-Chichewa, kwa wastani. Kama hatutaweka sera za kuendeleza lugha zetu za asili, vizazi vijavyo vya Malawi vitabaki na lugha moja tu, Kiingereza.

Kuzungumza lugha moja kunasababisha kuwa na mtazamo finyu, kuyatazama mambo kwa uelewa mdogo kwa sababu ya ukweli kwamba maarifa yote ayanayopatikana yanakuwa kwenye lugha moja tu. Hatari ya sera hii mpya, kama ilivyo, ni uwezekano wake wa kuathiri lugha za asili za Malawi. Sera hii pya itamaanisha kuwa nchi itatumia raslimali zake zaidi kwenye Kiingereza kwa gharama ya kulea na kuendeleza lugha za asili.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.